Shellukindo na Kamati Yako Mmepatwa na Nini?


Usisahau na Lowasa naye anatoka mkoa huo huo wa Arusha, kwahiyo kila mkoa ungekuwa na Lowasa mmoja fikiria mwenyewe ni wapi tungekuwa.....
 
Usisahau na Lowasa naye anatoka mkoa huo huo wa Arusha, kwahiyo kila mkoa ungekuwa na Lowasa mmoja fikiria mwenyewe ni wapi tungekuwa.....

Mikoa si hoja, suala ni la binafsi na si la Mkoa mzima!
 
Mikoa si hoja, suala ni la binafsi na si la Mkoa mzima!

Ndio nilichokuwa najaribu kumuonyesha huyo aliyeleta mambo ya mikoa, kwamba tukiangalia mazuri kwa mikoa basi tuangalie na mabaya kwa mikoa pia
 
Kamati imepatwa na kigugumizi, kama kawaida CCM Oyeeeeeeee!

Chama ni kubwa kuliko wananchi, wananchi wenyewe hawajui kama wamewaajiri wabunge..

Mimi nilishasema elimu anza kwako mwenyewe chukia ufisadi, then wanao then tutakuwa na taifa nzuri as for now...revolution bado kitambo kidogo
 
Chama kimetumia busara ya hali ya juu. Amani na utulivu ni muhimu kuliko chuki na mabishano yasiyo na mwisho. Sasa tusahau yaliyopitia. Chama kimetukomboa tusonge mbele, tujenge Taifa.
 



You can cut the branch alright but can you fly ?



You can abandon ship alright but can you swim ?
 
nimejaribu kusoma vyombo vya habari katika mitandao sijaona kama Seleli na Mwakyembe walipata nafasi ya kuzungumza,hivyo ninahisi tutakuwa hatutendi haki tukiwatumbukiza wapambanaji wote kwenye kapu moja,nafikiri kunyamaza kwao kimya kuna mshindo mkubwa mbele,nimejaribu kuupitia ule waraka wa wapambanaji wa ufisadi wa CCM naanza kupata hisia kwamba lolote laweza kutokea....lets wait and see
 
Ni bora walinyamaza. Ole Sendeka alizungumza kwa vijembe vya hapa na pale hatimaye akaunga mkono hoja na kumsifu saana JK. Mwakyembe yeye alisoma taarifa ya Kiwira akaishia zake. Mshindi amebaki mmoja tu, EL na timu yake ya akina Hosea, Mwakapugi,...
 
Bahati mbaya sija soma post zote hivyo nikiwa narudi maoni ya mchangiaji mwingine mniwie radhi.
Hili dili la Richmond inaonyesha Lowasa hakulifanya bali ni dili la "serikali", sasa kwa sababu linaihusu "serikali" ndio maana maamuzi yake yanabidi yawe hivyo.
Kama alivyo sema Msabaha yeye ni Bangusilo. Na Lowasa akasema kama mnataka uwaziri wenu Mkuu haya chukueni.( ingawa mimi si shabiki wa Lowasa) lakini naweza kuiona picha.
 
inakosewaa sana kulinganisha mchango wa maoni kati ya Dr slaa na sendeka katika uchangiaji wa kuhitimisha hoja ya richmond.. Sendeka jamani hakuchangia chochote zaidi ya kelele za ukada wake!!!! jamani huu ndo wepesi wepesi...

Dr slaa yeye binafsi ndiye aliyepinga hoja kwa tafakuri la msingi..
 
Dr. Slaa for President

Karibuni nitaanzisha Petition hapa JF kumtaka Dr. Slaa Agombee Urais. Anaweza
 
Kinachonishangaza ni jinsi watu wengi walivyotegemea kuwa wanachama, viongozi na wabunge wa CCM wangekiua chama chao kwa ajili ya kutimiza matarajio ya waTanzania.

Labda niwakumbushe tu. Mh. Dr. W. Slaa na wenzake walipoanza kutoa majina na watuhumiwa wa ufisadi, CCM ilijiona kuumbuka na kukosa majibu ya kuweza kuwapa wananchi. Njia pekee iliyokuwa imebaki ni kugeuza kibano. Wakataka ionekane kuwa mapambano ya ufisadi ni ajenda yao, na wakajaribu kusema hivyo. Ila wananchi waliona kama wanaiba ajenda za vyama vya upinzani (imeshafanyika hivyo mara nyingi).

Hivyo wachache ndani ya CCM wakajitokeza na kufunika wachache nje ya CCM ambao walionekana kujizolea umaarufu kwa ajenda hiyo. Hilo limefanikiwa sana.

Wameweza kuwafanya wengi kuamini kuwa ajenda ya mapambano na ufisadi ni ya CCM (uthibitisho ni kauli za wengi kwenye post hii) Kwa kifupi akina Dr. Slaa wamekubali kutekwa ajenda yao.

Nadhani kama unajua siasa za Tanzania vizuri, utakubaliana na mimi kuwa walichokifanya Wabunge wa CCM kwa kusema hadharani mapambano yao na ufisadi ni kujitosa kwa kiasi kikubwa. Wasingeweza kufanya zaidi ya walichokifanya. Kumbuka, pamoja na kuwa wana mamlaka ya kutetea na kusimamia misingi bora na ya kisheria ya Taifa, pia wana wajibu wa kusimamia sera, ukuaji na ushindi wa chama chao. Compromise katika hilo ndilo linalowarudisha na kuamua tusivyotaka kusikia.

Hakuna mwanachama wa CCM anaeweza kusimama kwa ushujaa na kuipinga CCM na akabaki kuwa mwanachama wa chama hicho. Vivyo hivyo kwa vyama vingine vyote. Huwezi kuhatarisha usalama, ustawi na ushindi wa chama chako halafu wakakuacha tu huku wakiona chama chao kikidhalilika na wewe ukijizolea umaarufu wa binafsi kisiasa.

Naamini pia kuwa, Kamati ya usuluhishi wa Wabunge wa CCM iliyoongozwa na Mzee Mwinyi ilikuwa ni kutaka kuaminisha wananchi kuwa wapiganaji hao wamekiuka misingi na imani za chama chao. Hakuna lolote. Wananchi wamedanganyika na technicalities za kisiasa na wakaamini. Sasa wengi wanalalamika kuwa wapiganaji wamewatosa. Hawajawahi kuwa upande wenu jamani. Walitaka kulinda ustawi wa chama chao tu.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema, alisema yeye amefurahishwa na hatua ambayo Bunge limefikia ya kuamua kuachana na suala la Richmond na kulifunga kwani lilikuwa linapoteza muda.
Mrema ambaye siku za hivi karibuni ametangaza kugombea ubunge na kuachana na kugombea urais, alisema suala hilo lilichukua karibia miaka mitatu huku likiteka masikio na akili za watu wakati kuna mambo mengi ya msingi ambayo wabunge wanapaswa kuyajadili kwa ajili ya maslahi ya nchi.
“Nimefurahia sana na hatua iliyofikiwa, wabunge wamezingatia maslahi ya taifa. Jambo moja la Richmond liliteka akili za Watanzania kwa zaidi ya miaka mitatu, tuna mambo mengi ya kujadiliana juu ya mustakabali wa nchi yetu, hasa kwa kipindi hiki, ” alisema Mrema.


.....Huyu tumweke kundi lipi? Au anaganga njaa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…