Shemeji; Maneno yako ya dhihaka nimeyasikia

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
SHEMEJI; MANENO YAKO YA DHIHAKA NIMEYASIKIA.

Kwa Mkono wa, Robert Heriel.

Kwanza nikuambie tuu hapa nilipo nina shahada ya juu kabisa katika Chuo Bora hapa NCHINI, Elimu yangu sio ya kubahatisha japo unaniona ninaishi maisha ya Ndege Kwa sasa lakini tambua CV yangu kielimu ni wachache waliyonayo hapa nchini.

Tangu chekechekea matokeo yangu sio yakubeza, NILIFAULU Kwa kiwango cha juu tangu nikiwa najifunza Kuhesabu Kwa kutumia visoda, wakati mumeo huyu ambaye ni kakaangu akizungusha elimu ya sekondari, miye niliibuka na ufaulu wa daraja la Kwanza, sitaki niseme mumeo ni kilaza usije nifitinisha akanifukuza hapa nyumbani kwake.

Maneno yako ya Dharau na kejeli mara ya Kwanza kabisa niliyasikia Kwa mwalimu aa Historia Enzi zile nasoma sekondari, tena nikuambie tuu mwalimu Yule amekuzidi Kwa mbali mno Kwa maneno ya shombo yenye usongo. Hivyo maneno yako ni kelele za chura tuu ambazo hazinizuii kunywa maji hapa ndani.

Uvumilivu nilifundishwa shuleni na nikaenda pale Oljoro JKT Arusha kupewa na cheti kabisa. Hakika Mafunzo yale sasa naona umuhimu wake. Maana Shemeji yangu Kwa manyanyaso na Mateso hujambo na wala hauna Jambo dogo yote kwako makubwa.

Unichimbishe visiki, nafanya,
Uniosheshe vyombo, Fresh!
Unipikishe, Sawa.
Unidekishe, hewala
Mimi ilimradi nipate sehemu ya kujihifadhi nikiwa napanga Formation ya kutoboa kimaisha.

Ulinifanyia visa na mikasa Kama kasa wa Nungwi ili nikereke niondoke hapa kwenu lakini Mimi nilijikaza. Ukaona haitoshi,

Ukaanza mpango mkakati wa kunitega na hapo Kati patamu lakini ili nijinome Kwa utamu utakaonipeleka kuzimu siku Kaka akitukuta.

Kunivalia Taulo ulilobana kwapani tadhani Juma Kaseja aubanavyo mpira kwapani ukadhani nitacheza Faulu zako za kipuuzi.
Nikweli Shemeji unamatako makubwa na mapaja yaliyonona, hili sikupenda kulisema lakini maji yameshavuka shingoni na sasa yapo kidevuni.
Kunivalia kanga moko na ukiona haitoshi unajipitisha na Dera lako ambalo ndani hujavaa nguo ya ndani. Hayo yote niliyakwepa kuepusha ushetani wako na hila yako ya kunifukuza.

Labda nikuambie, nilipokuwa nasoma Chuoni nikichukua Shahada yangu ya juu kabisa katika Chuo kikuu Bora kuliko hapa nchini, walikuwepo Wadada machozi zaidi yako, wazuri zaidi yako, waliovurugwa kitabia ingawaje kiakili zilikuwa zinachaji.
Nikuambie hao wanafunzi walivyokuwa wanavaa!
Huyo Sakina ungewezaje kuvumilia akivaa kikaputra tadhani yuko beach. Mtoto tako lilikuwa limemwagika utadhani maziwa yanayochemka.

Huyo Ashura je? Alikuwa akija amevaa suruali nyepesi pasipo nguo ya ndani, Hali iliyofanya matako yake kutetemeka. Unafikiri hiyo mitego sikuipitia.

Labda sijakuambia habari za hosteli, huko ndiko mitego ilikuwepo sio wewe mitego yako ya kanga isiyoweza kumnasa hata Digidigi. Wenzako walibobea katika mitego mikubwa nasikia mpaka Tembo wakubwa walinasa. Husikilizagi habari magazetini au pengine hujui kusoma, je Taarifa ya habari Redioni au luningani husikiagi jinsi wahadhiri na wakufunzi wa Chuoni wanavyonaswa na watoto wabichi wa Chuoni.
Sisemi ni tamaa zao kuwalaumu, wala siwatetei Kwa kushindwa kujizuia, Ila wakati mwingine mitego ya Tembo iliyotegwa na watoto wa Chuo waliovurugwa sio lelemama.

Hivyo nikusema, nimesoma Bibi wewe! Mitego yako niliipata kozi nikiwa mwaka wa pili kwenda watatu nikiwa bado kijana mtanashati niliyekonga nyoyo za walimbwende waliowengi.

Maneno yako yalikuwa yamenifikia, lakini leo nimekukamata Red-handed macho yakiwa yamekutoka.

Ati najaza Choo!!!
Kwamba Mimi nakunya nusu ndoo kila siku ama! Usijesema sina lugha nzuri Kueleza haya Acha niseme makavu makavu pasipo kutumia tafsida wala tahasida.
Kwanza Mimi ni msomi WA elimu ya juu kabisa katika Lugha adhimu ya kiswahili, usinifundishe wapi na nini chakusema.

Kama ni kujaza Choo ingenichukua miaka hamsaini kwani kwa siku nakunya mara moja na kiasi kisichozidi gramu Mia tano yaani hata kilo moja sifikishi.

Hilo halijaniuma, lakini kuniambia Mimi ni joka la kibisa ambalo jogoo haoandi mtumbwi wangu limeniuma sana.

Wakati unasema maneno hayo Kwa Shostito wako akiwa anakusuka hapa sebuleni Mimi ndio nilikuwa narudi nyumbani, nikayasikia maneno haya nikiwa hapo mlangoni.
Tena umepanga njama ya kunishambulia Kwa sumu ukidhamiria kuondoa Uhai wangu, licha ya shostito wako kukuonya na kukutaka uwe na huruma lakini wewe umekaza fuvu Kwa roho mbaya Kama Shwetani.

Elimu yangu ingeisaidia jamii hilo hata wewe unalitambua, lakini kukaa kwangu nyumbani Kwa kukosa Ajira ndio kunaleta haya yote.
Umeona nimezubaa Kama Maziwa mtindi lakini juhudi zangu za kusaka kazi unaziona.

Nimeomba kazi kila Kona kwenye jiji hili, kila Mkoa WA nchi hii, wapi sijafika kutuma maombi ya kazi.
Nikasema niombe kujitolea Kwa bure kabisa kwenye mashirika yasiyo ya kiserikali, huko nimefanya mpaka unajua nimechoka sasa, hela hakuna nitajitolea mpaka lini ikiwa nimejitolea miaka minne, unataka nijitolee ujana wangu wote mpaka nguvu ziniishe ili niajiriwe uzeeni, Nani atakubali hayo?

Kama sikufanya ujitoamhangamali kwenye Machinga ungenilaumu, Nani asiyejua nimekuwa Machinga mpaka nikachizika, kutwa kuchwa kupigishana kelele Kama mwendawazimu tadhani sikusoma Mimi, tena kusoma Ile kusoma yenyewe kwa viwango vya juu kabisa.
Kuvuta vuta wateja kule Kariakoo na Karume ili wanunue bidhaa zangu yote hayo nimefanya, matusi yalikuwa fungu langu hasa hawa ninyi msioyajua maisha ya wasakatonge AKA Walia na Mungu.

Udalali nao nikafanya hiyo ndio kabisa pasua kichwa. Unafikiri napenda kukaa hapa Mimi.

Maneno yako ya dhihaka na kejeli yamevuka ukomo na sasa yananipa somo kuwa uvumilivu pia Una mipaka, na Kama uvumilivu umenishinda unafikiri nisingeweza kulala na wewe na kumkosea Kaka yangu.
Kama nisingekuwa mvumilivu Leo hii si ningekuwa nimeshaondoka nikiwa nimegombana na Kaka yangu.

Juzi nilisema tukiwa wote na Kaka nawe ukisikia kuwa naenda kuongeza Elimu ya juu kabisa ya uzamivu ukanicheka Kwa Dharau na kuniambia hiyo sio elimu ya uzamivu labda elimu ya juu ya maumivu.
Wote tulicheka lakini maneno yako Kwa kweli yaliniuma Sana.

Kaka akija nitamuaga niwaache na maisha yenu, nisikufanya utende Uovu mkubwa ulioufikiria.

Nakumbuka ulivyoenda Kwa walozi na waganga kuniloga ati ili nice lakini uwezo wa maulana ukanikinga, hayo yote ningeyajuaje Kama sio huyu rafiki yako kuniambia.

Kwa taarifa yako kutoka kwangu msomi WA elimu ya juu kabisa kutoka Chuo kikuu kikubwa kuliko, huyu rafiki yako ndiye anayenituliza Moyo wangu, yeye ndiye ananipa tende namung'unya , yeye ndiye msaada mkubwa kwangu.
Kila usemacho ananiambia hata siku Ile ulivyotaka kuniwekea sumu alinambia ndio maana nikakataa Kula licha ya kunilazimisha Kwa mapenzi yako ya kinafiki ati unanipenda Kama Shemeji yako kumbe ni ili Nile nife.

Sitajali utakavyosema Kama Nalelewa na Rafiki yako, ndio maisha ya sasa yalivyo, ukiniita Mario shauri yako maana hata Mimi nakuona changudoa unayeishi ndoani.

Kama ni kazi nimehangaika Sana kuzifanya,
Kama ni kujitolea nimejitolea mpaka nimechoka sasa, kipi sijafanya?
Nimesoma na Kuhitimu,
Nimetafuta kazi na nikakosa mpaka vibarua,
Nimejitolea mpaka wakanitoa,
Sasa siwezi Acha kuwa na rafiki yako Kwa maneno yako yasio na msaada.

Tena tayari tumeshafungua biashara hapo mjini ya nguo na inaenda vizuri.

Kwa heri Shemeji, Kaka akija mwambie nimekimbia maneno yako ya shombo.

(Ninatoka nikiwa nimemshika Mchumba wangu"rafikiake shemejiangu" nabamiza mlango. Kunakuwa kimya)

Niite Taikon wa Fasihi.

Robert Heriel
Kwa sasa Morogoro
 
Du aisee kukaa Kwa ndugu mashemeji wanazingua, mi nilipomaliza chuo nilitimka mazima home. Life likinipiga narudisha mpira Kwa kipa home Kwa wazazi. Mashemeji wachache sana waelewa hasa kwa muda upo home bila mchongo.
 
Ukiishi kwa ndugu tena awe kaoa ishi kwa akili. Japo napata tafsiri tofaut ya shemeji
 
Yaani unataka ukae bure bure kwa huyo nduguyo bila kusaidia shuguli yoyote kwake???
 
SHEMEJI; MANENO YAKO YA DHIHAKA NIMEYASIKIA.

Kwa Mkono wa, Robert Heriel.

Kwanza nikuambie tuu hapa nilipo ninashahada ya juu kabisa katika Chuo Bora hapa NCHINI, Elimu yangu sio ya kubahatisha japo unaniona ninaishi maisha ya Ndege Kwa sasa lakini tambua CV yangu kielimu ni wachache waliyonayo hapa nchini.

Mkuu, ulichoandika kinaakisi uhalisia au ndio kama kawaida yako ya kufikisha fasihi kwa jamii? Kwa nini hukuambatana na brother umsaidie shughuli zake hata kwa ujira mdogo? Ulichoandika (kama ni kweli) kinaweza kukufitinisha na bro, kwani wengine ni wagumu kuamini na hivyo kuonekana ni mchonganishi wa masuala ya ndoa na ndugu!
 
Ungempiga mbupu kabla ya kusepa au nipe connection nikusaidie hicho kipengele
 
Mkuu, ulichoandika kinaakisi uhalisia au ndio kama kawaida yako ya kufikisha fasihi kwa jamii? Kwa nini hukuambatana na brother umsaidie shughuli zake hata kwa ujira mdogo? Ulichoandika (kama ni kweli) kinaweza kukufitinisha na bro, kwani wengine ni wagumu kuamini na hivyo kuonekana ni mchonganishi wa masuala ya ndoa na ndugu!

Mkuu nimepunguza mengine, nikisema yote nchi itasimama
 
SHEMEJI; MANENO YAKO YA DHIHAKA NIMEYASIKIA.

Kwa Mkono wa, Robert Heriel.

Kwanza nikuambie tuu hapa nilipo nina shahada ya juu kabisa katika Chuo Bora hapa NCHINI, Elimu yangu sio ya kubahatisha japo unaniona ninaishi maisha ya Ndege Kwa sasa lakini tambua CV yangu kielimu ni wachache waliyonayo hapa nchini.

Tangu chekechekea matokeo yangu sio yakubeza, NILIFAULU Kwa kiwango cha juu tangu nikiwa najifunza Kuhesabu Kwa kutumia visoda, wakati mumeo huyu ambaye ni kakaangu akizungusha elimu ya sekondari, miye niliibuka na ufaulu wa daraja la Kwanza, sitaki niseme mumeo ni kilaza usije nifitinisha akanifukuza hapa nyumbani kwake.

Maneno yako ya Dharau na kejeli mara ya Kwanza kabisa niliyasikia Kwa mwalimu aa Historia Enzi zile nasoma sekondari, tena nikuambie tuu mwalimu Yule amekuzidi Kwa mbali mno Kwa maneno ya shombo yenye usongo. Hivyo maneno yako ni kelele za chura tuu ambazo hazinizuii kunywa maji hapa ndani.

Uvumilivu nilifundishwa shuleni na nikaenda pale Oljoro JKT Arusha kupewa na cheti kabisa. Hakika Mafunzo yale sasa naona umuhimu wake. Maana Shemeji yangu Kwa manyanyaso na Mateso hujambo na wala hauna Jambo dogo yote kwako makubwa.

Unichimbishe visiki, nafanya,
Uniosheshe vyombo, Fresh!
Unipikishe, Sawa.
Unidekishe, hewala
Mimi ilimradi nipate sehemu ya kujihifadhi nikiwa napanga Formation ya kutoboa kimaisha.

Ulinifanyia visa na mikasa Kama kasa wa Nungwi ili nikereke niondoke hapa kwenu lakini Mimi nilijikaza. Ukaona haitoshi,

Ukaanza mpango mkakati wa kunitega na hapo Kati patamu lakini ili nijinome Kwa utamu utakaonipeleka kuzimu siku Kaka akitukuta.

Kunivalia Taulo ulilobana kwapani tadhani Juma Kaseja aubanavyo mpira kwapani ukadhani nitacheza Faulu zako za kipuuzi.
Nikweli Shemeji unamatako makubwa na mapaja yaliyonona, hili sikupenda kulisema lakini maji yameshavuka shingoni na sasa yapo kidevuni.
Kunivalia kanga moko na ukiona haitoshi unajipitisha na Dera lako ambalo ndani hujavaa nguo ya ndani. Hayo yote niliyakwepa kuepusha ushetani wako na hila yako ya kunifukuza.

Labda nikuambie, nilipokuwa nasoma Chuoni nikichukua Shahada yangu ya juu kabisa katika Chuo kikuu Bora kuliko hapa nchini, walikuwepo Wadada machozi zaidi yako, wazuri zaidi yako, waliovurugwa kitabia ingawaje kiakili zilikuwa zinachaji.
Nikuambie hao wanafunzi walivyokuwa wanavaa!
Huyo Sakina ungewezaje kuvumilia akivaa kikaputra tadhani yuko beach. Mtoto tako lilikuwa limemwagika utadhani maziwa yanayochemka.

Huyo Ashura je? Alikuwa akija amevaa suruali nyepesi pasipo nguo ya ndani, Hali iliyofanya matako yake kutetemeka. Unafikiri hiyo mitego sikuipitia.

Labda sijakuambia habari za hosteli, huko ndiko mitego ilikuwepo sio wewe mitego yako ya kanga isiyoweza kumnasa hata Digidigi. Wenzako walibobea katika mitego mikubwa nasikia mpaka Tembo wakubwa walinasa. Husikilizagi habari magazetini au pengine hujui kusoma, je Taarifa ya habari Redioni au luningani husikiagi jinsi wahadhiri na wakufunzi wa Chuoni wanavyonaswa na watoto wabichi wa Chuoni.
Sisemi ni tamaa zao kuwalaumu, wala siwatetei Kwa kushindwa kujizuia, Ila wakati mwingine mitego ya Tembo iliyotegwa na watoto wa Chuo waliovurugwa sio lelemama.

Hivyo nikusema, nimesoma Bibi wewe! Mitego yako niliipata kozi nikiwa mwaka wa pili kwenda watatu nikiwa bado kijana mtanashati niliyekonga nyoyo za walimbwende waliowengi.

Maneno yako yalikuwa yamenifikia, lakini leo nimekukamata Red-handed macho yakiwa yamekutoka.

Ati najaza Choo!!!
Kwamba Mimi nakunya nusu ndoo kila siku ama! Usijesema sina lugha nzuri Kueleza haya Acha niseme makavu makavu pasipo kutumia tafsida wala tahasida.
Kwanza Mimi ni msomi WA elimu ya juu kabisa katika Lugha adhimu ya kiswahili, usinifundishe wapi na nini chakusema.

Kama ni kujaza Choo ingenichukua miaka hamsaini kwani kwa siku nakunya mara moja na kiasi kisichozidi gramu Mia tano yaani hata kilo moja sifikishi.

Hilo halijaniuma, lakini kuniambia Mimi ni joka la kibisa ambalo jogoo haoandi mtumbwi wangu limeniuma sana.

Wakati unasema maneno hayo Kwa Shostito wako akiwa anakusuka hapa sebuleni Mimi ndio nilikuwa narudi nyumbani, nikayasikia maneno haya nikiwa hapo mlangoni.
Tena umepanga njama ya kunishambulia Kwa sumu ukidhamiria kuondoa Uhai wangu, licha ya shostito wako kukuonya na kukutaka uwe na huruma lakini wewe umekaza fuvu Kwa roho mbaya Kama Shwetani.

Elimu yangu ingeisaidia jamii hilo hata wewe unalitambua, lakini kukaa kwangu nyumbani Kwa kukosa Ajira ndio kunaleta haya yote.
Umeona nimezubaa Kama Maziwa mtindi lakini juhudi zangu za kusaka kazi unaziona.

Nimeomba kazi kila Kona kwenye jiji hili, kila Mkoa WA nchi hii, wapi sijafika kutuma maombi ya kazi.
Nikasema niombe kujitolea Kwa bure kabisa kwenye mashirika yasiyo ya kiserikali, huko nimefanya mpaka unajua nimechoka sasa, hela hakuna nitajitolea mpaka lini ikiwa nimejitolea miaka minne, unataka nijitolee ujana wangu wote mpaka nguvu ziniishe ili niajiriwe uzeeni, Nani atakubali hayo?

Kama sikufanya ujitoamhangamali kwenye Machinga ungenilaumu, Nani asiyejua nimekuwa Machinga mpaka nikachizika, kutwa kuchwa kupigishana kelele Kama mwendawazimu tadhani sikusoma Mimi, tena kusoma Ile kusoma yenyewe kwa viwango vya juu kabisa.
Kuvuta vuta wateja kule Kariakoo na Karume ili wanunue bidhaa zangu yote hayo nimefanya, matusi yalikuwa fungu langu hasa hawa ninyi msioyajua maisha ya wasakatonge AKA Walia na Mungu.

Udalali nao nikafanya hiyo ndio kabisa pasua kichwa. Unafikiri napenda kukaa hapa Mimi.

Maneno yako ya dhihaka na kejeli yamevuka ukomo na sasa yananipa somo kuwa uvumilivu pia Una mipaka, na Kama uvumilivu umenishinda unafikiri nisingeweza kulala na wewe na kumkosea Kaka yangu.
Kama nisingekuwa mvumilivu Leo hii si ningekuwa nimeshaondoka nikiwa nimegombana na Kaka yangu.

Juzi nilisema tukiwa wote na Kaka nawe ukisikia kuwa naenda kuongeza Elimu ya juu kabisa ya uzamivu ukanicheka Kwa Dharau na kuniambia hiyo sio elimu ya uzamivu labda elimu ya juu ya maumivu.
Wote tulicheka lakini maneno yako Kwa kweli yaliniuma Sana.

Kaka akija nitamuaga niwaache na maisha yenu, nisikufanya utende Uovu mkubwa ulioufikiria.

Nakumbuka ulivyoenda Kwa walozi na waganga kuniloga ati ili nice lakini uwezo wa maulana ukanikinga, hayo yote ningeyajuaje Kama sio huyu rafiki yako kuniambia.

Kwa taarifa yako kutoka kwangu msomi WA elimu ya juu kabisa kutoka Chuo kikuu kikubwa kuliko, huyu rafiki yako ndiye anayenituliza Moyo wangu, yeye ndiye ananipa tende namung'unya , yeye ndiye msaada mkubwa kwangu.
Kila usemacho ananiambia hata siku Ile ulivyotaka kuniwekea sumu alinambia ndio maana nikakataa Kula licha ya kunilazimisha Kwa mapenzi yako ya kinafiki ati unanipenda Kama Shemeji yako kumbe ni ili Nile nife.

Sitajali utakavyosema Kama Nalelewa na Rafiki yako, ndio maisha ya sasa yalivyo, ukiniita Mario shauri yako maana hata Mimi nakuona changudoa unayeishi ndoani.

Kama ni kazi nimehangaika Sana kuzifanya,
Kama ni kujitolea nimejitolea mpaka nimechoka sasa, kipi sijafanya?
Nimesoma na Kuhitimu,
Nimetafuta kazi na nikakosa mpaka vibarua,
Nimejitolea mpaka wakanitoa,
Sasa siwezi Acha kuwa na rafiki yako Kwa maneno yako yasio na msaada.

Tena tayari tumeshafungua biashara hapo mjini ya nguo na inaenda vizuri.

Kwa heri Shemeji, Kaka akija mwambie nimekimbia maneno yako ya shombo.

(Ninatoka nikiwa nimemshika Mchumba wangu"rafikiake shemejiangu" nabamiza mlango. Kunakuwa kimya)

Niite Taikon wa Fasihi.

Robert Heriel
Kwa sasa Morogoro
Weka namba ya simu unaweza kulamba teuzi,licha ya Jana CCM kutangaza teuzi za makatibu wa chama.
 
Back
Top Bottom