Shemeji yako aliyemuoa dada yako sio ndugu yako

Shemeji yako aliyemuoa dada yako sio ndugu yako

bulabo

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2015
Posts
628
Reaction score
780
Kwa mila na Desturi zetu za Kitanzania. Jamaa aliyeoa dada yako hata siku moja SIO NDUGU YAKO. Hii kitu inote kwa sababu kwanza kabisa dada yako akifariki jamaa anaenda kumzika kwao. Watoto wote anaandika majina yake. Mali zote anaandikisha either MAMA YAKE au Mdogo wake wa Kiume au watoto wake wa Kiume.

Nataka kusema nini?? Ukiwa na dada yako ameolewa na jamaa usitumie muda mwingi kujiweka karibu kwa sbb huyo sio ndugu yako hata siku MOJA. Mila na Desturi zetu hazimpi nafasi mtoto wa kike kumiliki chochote either kwa WAKRISTO au WAISLAMU. Hili ni janga kubwa.

Ndio maana ukizaa watoto wa kike ni kama vile huna chako. Ndio maana mtoto wa kike nashauri msomeshe vzr awe na mali zake asije kutegemea mwanaume. Mwanamke akiolewa na akategemea mwanaume huyo hana cha kurithi wala kumiliki.

Kwa hiyo Watanzania mjitahd kuhakikisha watoto wa kike wanakuwa na vitu vyao wenyewe ili wasinyanyasike kwenye NDOA Zao kama ni gari awe na uwezo wa kulinunua, Shamba Nyumba na n.k
 
Kuna walimwengu wengi watakuja kupinga huu ukweli sababu ya maslahi yao binafsi.

Kuna njemba zinaishi kwa shemeji na kila kitu kutegemea cha shemeji kiasi cha mpaka kuonea wivu ndugu wa shemeji.

Utakuta mwanaume ana uchungu na mume wa dada yake kuliko hata dada yake mwenye mume wake kiasi hata pakitokea ugomvi anakuwa upande wa shemeji yake na sio dada yake.
 
Kipindi hicho wote bado wadogo

Siku moja jama alimtorosha young sis(wakiwa wachumba), halafu asubuhi 12 akawa anamleta kiuficho nami ndio natoka kwenda kufanya mazoezi isitoshe mda huo sis alikuwa bado skuli ....salalee nilitandika sana wote wawili ile siku alikuwa kuamulia ugomvi mjumbe wa nyumba kumi😅😅😅

Jamaa alichukuaga jiko sahivi tukipiga stori akikunikumbushia huwa tunacheka sana.
Hata kama sio ndugu yangu jamaa yuko cool sana.
 
Back
Top Bottom