Shemeji zangu Wagogo wako vizuri kwa Jiografia!

Kimwakaleli

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2018
Posts
7,755
Reaction score
11,737
Habari wanajf,Nipo hapa Dodoma ingawa mwenyewe ni mwenyeji wa Mbeya.Nimeishi hapa Dodoma kwa zaidi ya miaka kumi(10)na kubahatika kuoa mgogo,nimegundua kwamba wapo vizuri kwa jografia!Ukiwa mgeni hapa na unaulizia mahali pa kwenda wao hawana kuelekeza pita kushoto au kulia ,au mbele wao husema nenda magharibi au elekea mashariki nk.Wako vizuri nawapa maua yao.
 
alafu hiyo kweli kabisa mwanzo nafika hapa Dodoma mwaka 2017 nilikuwa nashangaa sana jinsi wanavyoelekeza mtu utaskia "...Nenda na hii barabara mbele kidogo angalia upande wa Mashariki utaiona hiyo ofisi..."
 
Aisee kwa kweli!
 
Nenda Kilimanjaro kwenda kulia wanaita kupandisha na kwenda kushoto wanaita kushuka. Unaambiwa shuka na hii barabara wakati barabara yenyewe huoni ikiwa na mteremko.

Ukienda vijiji vya mikoa wanayochota maji umbali mrefu au wanaopata huduma mbali ukaulizia sehemu fulani unaambiwa ni hapo tu karibu kama nusu saa unafika. Hapo utatembea lisaa na nusu hujafika.

Kuna maeneo wanakadiria kwa mfanano, fulani kaondoka muda gani it's likely uambiwe kama dakika tano au kama dakika kumi na watu wa eneo hilo. Wakati kiuhalisia ana zaidi ya dakika 50 ameondoka. Dakika tano nakuja, tulitumia kama dakika kumi, alikaa kama dakika tano.
 
Watani wangu, pamoja nakujua Jiografia nimegundua ni miongoni mwa makabila yenye furaha siyo kama kabila langu utamkuta mtu anamiliki magunia Mia ya mpunga na mahindi nyumba na mali nyingine lakini hatuna raha sijui kwa nn?
 
Nao hao wa kilimanjaro wanachanganya pandisha,shuka!
 
Watani wangu, pamoja nakujua Jiografia nimegundua ni miongoni mwa makabila yenye furaha siyo kama kabila langu utamkuta mtu anamiliki magunia Mia ya mpunga na mahindi nyumba na mali nyingine lakini hatuna raha sijui kwa nn?
Kweli wana furaha!
 
Back
Top Bottom