Nenda Kilimanjaro kwenda kulia wanaita kupandisha na kwenda kushoto wanaita kushuka. Unaambiwa shuka na hii barabara wakati barabara yenyewe huoni ikiwa na mteremko.
Ukienda vijiji vya mikoa wanayochota maji umbali mrefu au wanaopata huduma mbali ukaulizia sehemu fulani unaambiwa ni hapo tu karibu kama nusu saa unafika. Hapo utatembea lisaa na nusu hujafika.
Kuna maeneo wanakadiria kwa mfanano, fulani kaondoka muda gani it's likely uambiwe kama dakika tano au kama dakika kumi na watu wa eneo hilo. Wakati kiuhalisia ana zaidi ya dakika 50 ameondoka. Dakika tano nakuja, tulitumia kama dakika kumi, alikaa kama dakika tano.