MwanaHaki
R I P
- Oct 17, 2006
- 2,401
- 707
Habari zilizopatikana jioni hii (Jumatano, Mei 27, 2009) zinasema kwamba shemeji yake Dk. Shukuru Kawambwa, ambaye ndiye aliyekuwa msimamizi wa shamba la Dk. Kawambwa (Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu na Mbunge wa Bagamoyo - CCM), ameuwawa jana, Jumanne, Mei 26, 2008, takriban saa 2 usiku, baada ya tukio la uhalifu ambalo watu kadhaa walivamia kwenye shamba hilo wakiwa na nia ya kufanya uporaji.
Chanzo cha habari hizi kinasema kwamba katika purukushani hizo, shemejiye Dk. Kawambwa, ambaye alikuwa akisimamia shamba hilo lenye idadi kubwa ya mifugo na mazao kadhaa, akishirikiana na mkewe (dada wa Dk. Kawambwa), alipigwa risasi kwenye miguu yote miwili na kuanguka chini. Akipambana na maharamia hao, alifanikiwa kumvua soksi ambayo ilikuwa imeuficha uso wa mmoja wa wahalifu hao, akamtambua. Alihamaki na kuonesha kwamba amemtambua, jambo ambalo linasadikiwa kuchangia kifo chake, kwani majambazi hao waliokuwa na silaha za moto pamoja na mapanga waliamua kummaliza kwa kumkata mapanga shingoni.
Chanzo kimeeleza zaidi kwamba katika siku za karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la uhalifu kwenye Wilaya ya Bagamoyo, jambo ambalo limewafanya wakazi wa mji huu wenye historia kongwe kuishi maisha ya hofu na wasiwasi mkubwa.
"Tumekuwa tukivamiwa, wakiingia wanachukua chochote kile chenye thamani kwao, TV, redio, kompyuta, chochote kile... ukiwabishia utaumizwa..." kilisema chanzo hiki.
Inasadikiwa kwamba baada ya uvamizi kwenye shamba hilo la Dk. Kawambwa iliwachukua takriban muda wa saa moja askari polisi wa Kituo cha Bagamoyo kufika hapo, eneo la Sanzale, wakati huo wahalifu wakiwa wameshafika mbali na kutoweka kabisa.
Kwa maoni ya chanzo cha habari hizi, inashangaza ni kwa sababu gani mpaka sasa habari za tukio hilo la uhalifu lililotokea kwenye shamba kubwa la mmojawapo wa viongozi waandamizi wa Serikali ya Awamu ya Nne inayoongozwa na CCM halijatangazwa kwenye vyombo vya habari. Maoni ya wadau kadhaa yameelezea kuwapo kwa jitihada za kuficha habari hizi ili kuficha ukweli kwamba Waziri huyo mwandamizi ni mkulima na mfugaji hodari, jambo ambalo linashangaza, kwa kuwa kilimo na ufugaji ni uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania. Hata hivyo, wadau wamesema, pengine ni ukubwa wa shamba hilo ndio unaoweza kuwa sababu ya Waziri huyo kutotaka habari hizo kutangazwa, kwani zinaweza kumwaibisha na kumharibia nafasi yake kwa namna fulani.
Wachunguzi wa habari zaidi watazidi kutuletea habari na maoni zaidi kuhusu tukio hili la kusikitisha.