Pre GE2025 Shemsa Mohammed atoa Tsh. Milioni 8 kwenye ngoma ya asili ya Kisukuma

Pre GE2025 Shemsa Mohammed atoa Tsh. Milioni 8 kwenye ngoma ya asili ya Kisukuma

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
SHEMSA MOHAMMED AMBAYE NI MLEZI WA TAMADUNI NA WAGANGA WA TIBA ASILIA NA MLEZI SUNGUSUNGU KANDA YA ZIWA WAGAWA ZAWADI KIASI CHA PESA MILION NANE ( 8,000,000/=) MBINA YA THELATHINI

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Ndugu SHEMSA MOHAMMED ambaye ni Mlezi wa Utamaduni na Waganga wa Tiba asili Mkoa wa simiyu, Wakiambatana na Mlezi wa Sungusungu Kanda ya Ziwa walipopokelewa kwa shangwe kubwa katika Mbina ya Asili.

Shemsa Mohamed na Mlezi Sungusungu Walifika nakuanza kuimba na kucheza nao katika Mbina kwa pande zote Bhagika na Bhagalu kwa wakati tofauti.

Shamsa Mohammed aliwasihi Wajitokeze kwa Wingi katika kujiandikisha kwenye Daftari la kudumu la Wapiga kura ambalo litawafanywa wawe wapiga kura halali katika kuchangua viongozi makini Wa Chama Cha Mapinduzi.

Vilevile, Aliwaomba Waendelee kumuunga mkono DKT SAMIA SULUHU HASSAN Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maendeleo makubwa anayoyafanya katika nchi yetu ya Tanzania, nakuwaomba ifikapo Mwaka 2025 wampigie kura za kutosha Rais ili aendelee kulijenga taifa letu.

Aidha , aliwapatia zawadi ya kiasi cha milioni nne (4,000,000) Bhagika na kiasi cha milioni nne (4,000,000) Bhagalu, aliendelea kuwaomba kuendelea kuwaunga mkono Viongozi wote wa Chama cha Mapinduzi.

"Mimi ni Mlezi wa Tamaduni na Waganga Wa Tiba asili mkoa wa simiyu, hivyo tuendeleeni kudumisha mila na Tamaduni zetu kama Mababu zetu walivyotuachia"

Shamsa Mohammed, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu na Mlezi wa Tamaduni na Waganga Tiba Asili.
 
Back
Top Bottom