Sherehe za CCM Kutimiza Miaka 33 Zafana - Reading, Uingereza


Mkuu taratibu sio wote walio UK wako kwenye huo upuuzi.
 
Hivi wanaweza kutueleza Fweza za walipa kodi zilizotumika hapo ni ngapi? Je, nani aliridhia fweza hizo kutumika. Huu ni wizi wa mchana kweupe na watu wapo wanashududia wakati ni hii hii serikali iliyoshindwa kuwasaidia waliokumbwa na maafa kule Kilosa nk.
 

Mlalahoi,

Hebu punguza jazba kidogo, kisha utaona mimi na wewe tuko kwenye mstari mmoja, tunakubali Wana CCM wajiunge na CCM yao popote pale walipo.

Unapokuja kwenye nini Wana CCM wa UK wanatakiwa kufanya ndani ya Chama Chao kama wewe sio Mwanachama mwenzao unakosa haki ya kuwaamulia. Huo ndio ukweli halisi, kutegemea kuwa Wana CCM watafanya anavyotegemea Mlalahoi ni yale ya yale ya kusubiri kuwa disapointed.
 

Labda nikufahamishe kuwa Wana CCM waliopo States nao vile vile wanatumia haki yao kujishughulisha na chama chao.
 

Attachments

  • CCM MArekani.JPG
    161.9 KB · Views: 69
Mkuu taratibu sio wote walio UK wako kwenye huo upuuzi.


I agree with you,but kama unaona kila siku wanajipromote kwenye vyombo vya habari inakuwa too much.I know wapo waTz wengi they dont give a damn about this stupidity of high calibre.Mwananchi iliandika habari hizi,hivyo watu wengi walisoma hii information
 

Labda nikufahamishe kuwa Wana CCM waliopo States nao vile vile wanatumia haki yao kujishughulisha na chama chao.
 
Samahani S.S Phares

Swali la kijinga and it is personal lakini huenda linaweza jibu mambo yote.

Ulifikaje huko? kuwa mkweli.
 
Samahani S.S Phares

Swali la kijinga and it is personal lakini huenda linaweza jibu mambo yote.

Ulifikaje huko? kuwa mkweli.

Hii ni topic ya Siasa mimi binafsi nilifikaje hapa inakuhusu wewe.

Ina maana kwa sababu tu, tumetofautiana kwenye hii hoja ndio unataka kunijua??!!
 
s s phares naona umeshindwa kuiweka mada yako vizuri hizo picha hazielezi chochote zaidi ya kutaka hayo uliyoyataka na kama wewe ni msemaji wa ccm huko london naona umeumia hii sio move nzuri hata kidogo kisiasa hata kijamii

wakati mwingine kabla ya kuweka mambo haya ongeeni na wakubwa zetu au wasemaji wa chama sio kuja kujiwekea mapicha hata bila idhini ya waliopigwa
 

Hembu nianze kuipasua hii hoja yako bwana phares. Kuwa mwanaCCM nje ya nchi ni haki yako ya kikatiba ambayo kila mtanzania anaweza kujishughulisha na na kijiunga na chama chochote popote duniani. Swali la kuanzia ni hivi kwanini wewe unajiunga na CCM wakati wewe huhudhurii hata kikao kimoja cha CCM? Wengi hamjui hata CCM imeanzaje badala yake huwa mnafata mkumbo wa kutaka kuwa wanaCCM je hebu tueleze bwana Phares wewe CCM umeipendea nini?

Pili tuje kwa wanandugu zetu na hizi movement zao. Wengi wao wameenda UK na kujibadilisha uraia wao, wengine wamesomeshwa na serikali wakaitosa walipopata kazi nzuri na wengine wameenda wakaoverstay UK wanatafutwa na Home office wanaishi kwa kubadilisha majina yao. Ukiangalia hawa watu wengi wao hawana uzalendo halisi na nchi yao kwasababu kama walikuwa na uzalendo halisi uzalendo wa kwanza ni kuipenda nchi yako hata kama ni jangwa!!!! Je swali nyie ni wazalendo kweli????

Tatu tukija katika historia nani asiyemjua Masha hapa jamvini na movement zake kule States? Nani asiyemjua Kevin Twisa na wengineo wengi. Kihistoria hawa watu walikuwa wanajifanya ni proactive ili nao wapate access ya kuingia katika system wakiingizwa wanaingia na tamaa ya kutajirika kiurahisi je swali nakuuliza bwana au sijui bibi phares je tuelezeni ajenda yenu ya kuingia katika siasa ipi???

Ndio maana ndugu yangu nimekushauri achana na siasa wewe piga mzigo wako katika mambo ya Information Technology upate hela nzuri but ukiingia katika politics utaumia.

Nilikuwapo!!!!
 
Hii ni topic ya Siasa mimi binafsi nilifikaje hapa inakuhusu wewe.

Ina maana kwa sababu tu, tumetofautiana kwenye hii hoja ndio unataka kunijua??!!

hii sio siasa sio mada ya kisiasa hii ndio maana ilitakiwa kwenye picha sasa unataka kijadiliwe nini kama umeficha hata jina lako kudefend ulichoandika kwamba mkutano umefana kwa yepi
 

Yaleyale ya CCM "yenyewe" huko nyumbani.UBISHI na kuona kila anayewakosoa ni adui wa "umoja na mshikamano wa kitaifa (kifisadi)".

Sawa,mie sio mwanachama mwenzenu lakini ni Mtanzania mwenzenu.Na ni kwa minajili hiyo ndio maana nawaeleza matarajio yetu kwenu wana-chama tawala mlio nje ya nchi.Hivi kweli kabisa mnajifanya hamuelewi,kwa mfano,kuwa ishu za rada,richmond,epa,kiwira,nk ni matokeo ya siasa za kulindana ndani ya tanzania?Hivi mnajifanya vipofu wa kufahamu kuwa Tanzania yetu haistahili kuwa hapo ilipo (masikini wa kupindukia) licha ya neema lukuki tulizojaliwa ikiwa pamoja na "upole wa walalahoi wanaoibia raslimali zao mchana kweupe kwa kisingizio cha uwekezaji"?

Uhuru bila wajibu ni upuuzi.Na japo mna uhuru wa kuwa wanachama wa chama chochote kile,hata ingekuwa BNP,lakini mishipa yenu ya aibu (kama ipo na inafanya kazi) inapaswa kuwajibika as well as brains zenu.Kinachowafanya muonekane vituko ni umahiri wenu wa kutuwekea mipicha yenu ya kila kikao badala ya ku-address nini chama chenu kilifanyie taifa.Nyie ni wasaliti wa Watanzania wenzenu.Na msijilinganishe na wana-CCM walioko nyumbani kwa vile wao bado wako kizani.Ninyi mmebahatika kuwa nje ya kiza hicho,lakini unfortunatelymmebakia kuwa so much obsessed na kuonekana kwenye picha mkipeana mikono na viongozi kuliko kusaidia uboreshaji wa CCM from makucha ya mafisadi into chama cha kuwatumikia Watanzania.

Vox populi vox dei,ndugu yangu.Hamjiulizi kwanini wengi wetu tunawashangaa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…