Sherehe za kichawi huondoka na roho ya mtu

Daah!!! nimekumbuka mbali sana kipindi hicho tuko huko kiomoni(amboni-Tanga). Tulipokuwa tukienda kwenye maporomoko ya mto utofu, kuvua mchanga wa mtoni, kupalilia mpunga, nakumbuka marehemu babu aliwahi nisimulia kuhusiana na huyo mtu Osale Otango alikuwa kiumbe wa ajabu. Na tulikwenda hadi hapo mapangoni ni mita kama 500 kutoka kwenye nyumba ya babu, alitengeneza sehemu maalum kwa kujifichia, tulikuwa tunafaidi sana wakati watu wanapokuja kufanya matambiko, na wafanyabiashara wenye asili ya kiasia walikuwa wanatoa sadaka za kutosha tuuu!!! mbuzi, majogoo, pesa, vito. Nilikuwa na mjomba wangu alikuwa ni mlinzi hapo mapangoni alikuwa akitusimulia, vibweka, vituko, vimbwanga, ambavyo alivyokuwa anakutana navyo. Osale Otango mtu wa matukio sana!!!!
 
Asante mkuu kwa kufunua akili yangu sasa nimeanza kuelewa kafara ni nini,Lakini ningependa ulete makala hii pia.Black magic and White magic,kuanza na zilivyo tofauti na mengineyo
 
Asante mkuu kwa kufunua akili yangu sasa nimeanza kuelewa kafara ni nini,Lakini ningependa ulete makala hii pia.Black magic and White magic,kuanza na zilivyo, tofauti na mengineyo
 
We mshana jr kwa hizi stori za kichawi nimekuvulia kofia
 
Mkuu@mshana jr! miongoni mwa mambo aliyowahi kunisimulia mjomba angu!! ambayo sitokuja yasahau ni:- siku moja wakati akiwa lindoni hapo mapangoni lindo la usiku!! alisikia mlio wa ngoma ukiambatana nyimbo ukitokea karibu na shamba(hilo shamba ni la familia fulani maarufu sana hapa kwetu Tz). Huku ile sauti ya ngoma ikikaribia maeneo ya pangoni, mara akawa ameona kikundi cha watu wakiwa uch!!, huku wamebeba mioto, na mili ya wanawake wawili, na vyungu vikubwa!! basi anasema wale watu wakaendelea kuimba!! halafu wakakoka moto na kuinjika vile vyungu viwili katika moto vilivyopata moto sana, vikaanza kuchemka!!! Mwisho wa yote wakatoa mawe katika vyungu viwili vile na kuwalisha wale wanawake wawili, ambao yeye mjomba alituambia kuwa anawafahamu wanawake hao tena walikuwa wajawazito!! waliwalisha mawe hayo huku yakiwa ni ya moto, kuwanyusa na kuwasotea sotea. Mwisho wa yote wale wanawake wakati wa kujifungua mmoja alifariki, mwengine alikufa mtoto akabaki yeye.
Je mshana jr kuna mahusiano yoyote yakulisha mawe na vifo hivyo.
Halafu mjomba tulimuuliza yeye amewezaje kuwaona wachawi alituambia kuwa amezindikwa(zindiko) je kwani dawa za waganga wa kienyeji zina nguvu kuliko za kichawi?
 
Na ole wao wanaoalikwa kwenye sherehe wanajipeleka na kubugia vyakula na vinywaji kwa matajiri wakafikiri wamependelewa!
 
[emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…