Sherehe za kichawi huondoka na roho ya mtu

Ile ilikuwa ni sherehe ya kafara ya kuwachukua wazazi ama watoto jambo ambalo lilifanikiwa
Pili ukifanyiwa zindiko hujumuisha pia uchawi na ushirikina kwahiyo huweza kuyaona mengi ya kichawi
 
Ningekupa kitabu cha kusoma lkn bahati mbaya ww sio mkristu
 
Mkuu mshana jr naomba unijuze ni sehemu gani katika mwili wa binadamu hupendelea kuweka vitu vyao kama kumtupia mtu nuksi n.k
 
Mkuu mshana jr naomba unijuze ni sehemu gani katika mwili wa binadamu hupendelea kuweka vitu vyao kama kumtupia mtu nuksi n.k
Nywele hutumika hasa kwenye uchizi lakini mara nyingi ni vya kumeza kwa maana ya tumboni
 
Mkuu mshana jr nafuatilia Uzi kwa makini sana.

Kitambo huko nyuma, enzi hizo mchezo wa netball uko juu sana, dada yng alikuwa star ktk timu yao.

Ghafla alipata maradhi ya mguu, ambao ulimuuma sana. Wazee walihangaika sana na matibabu bila mafanikio. Mara zote hospital walisema hawaoni tatizo.

Sijui ilikuwaje lakini nakumbuka alifanyiwa upasuaji wa mguu maeneo ya kifundo cha mguu, akatolewa battery la radio au tochi likiwa limejaa mafuta km ya nyama ya Ng'ombe!

Maswali:

Naomba kujua, uchawi gn au mbinu ipi ilitumiwa na wachawi kupandikiza lile battery?

Kwa nini waganga wengi walishindwa kuona lile battery?

Waliompasua mguu na kumtoa lile battery wanaweza kuwa ndio wao wao waliompandikiza?

Dada yu hao lkn mpk leo akivaa viatu, kimoja hakimtoshi kutokana na upasuaji na kutolewa battery lile!

Shukrani kwa elimu hii
 
Hiyo battery ilipandikizwa kichawi akiwa usingizini kwa sehemu kubwa, ilikuja kuonekana baada ya zile dawa kuisha nguvu la sivyo ingekuwa ngumu sana kutibika
 
Maana nina jamaa yangu mambo yake yalikuwa hayaendi kabisa ikabd akachungulie upande wa pili,baada ya kufanyiwa shughuli zote alitolewa kipande cha ngozi kwenye maeneno ya kifua na kinailoni ambacho kimefungwa vizuri na waya ndani yake kukiwepo kimfupa,nywele za sehemu za siri kulingana na maelezo ya mtaalam pamoja na vile vikobe vya bahari
Kikubwa mtaalamu alimwambia walimtia nuksi tu katika mambo yake na kuififisha nyota yake..! mshana jr vinawezekana hvyo?!
 
Kwenye ulimwengu wa kishirikina na kichawi hakuna linaloshindikana
 
Mkuu mshana jr, naomba uwe unanitag kwenye hizi mada zako ili tuweze kujifunza mawili matatu, na sisi tunaweza changia chochote tunachokifahamu
 
Mkuu mshana jr, naomba uwe unanitag kwenye hizi mada zako ili tuweze kujifunza mawili matatu, na sisi tunaweza changia chochote tunachokifahamu
Haina shida ila nikipitiwa uniwie radhi
 
Thubutu, hagusi hapo anaujuwa mziki wangu na anajuwa huo ndiyo ukweli.
....ogopa sana mtu anaepita kimya,huwezi jua kwenye akili yake amekuchukuliaje,ningekuwa wewe ningesikitika sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…