Sheri hapa inasemaje? Karibu uwanjani

Sheri hapa inasemaje? Karibu uwanjani

Shujaa Nduna

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2022
Posts
599
Reaction score
487
Ikiwa mtu kaja kwangu kutaka nimkopeshe hela kama laki nayeye kakubali kuleta kitu cha thamani ya hela au zaidi na tukaandikishana ili kama hatalipa kwa wakati vitu vinakuwa wangu.

Sasa ikapita muda wa makubaliano anakuja kudai nimpe vitu anipe hela wakati muda umepita je hapo kisheria ipoje?
 
Ikiwa mtu kaja kwangu kutaka nimkopeshe hela kama laki nayeye kakubali kuleta kitu cha thamani ya hela au zaidi na tukaandikishana ili kama hatalipa kwa wakati vitu vinakuwa wangu.Sasa ikapita muda wa makubaliano anakuja kudai nimpe vitu anipe hela wakati muda umepita je hapo kisheria ipoje?
Kisheria huna nguvu,mrudishie tu ila inatakiwa akufikilie tu

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Hapo umebugi, mpe vitu akupe hela Yako yaishe. Kisheria huna nguvu ya kukopesha bila kusajiliwa, hivyo wewe ulimuazima mtu hela bila riba. Na kwasababu hutozi riba unamaanisha kuwa hivyo vitu hata vingekaa mwaka mzima makubaliano yangebaki pale pale. Ungekua na taasisi ya kukopesha basi ulikua na nguvu hata ya kudai Mara tatu ya Hela Yako kadili ya vigezo vyako.
 
Kama kwenye mkataba mliandikishana unamuazima kiasi cha fedha kwa dhamana ya hivyo vitu basi kisheria una nguvu!

Na kama mmeandikishana kwamba unamkopesha na riba basi sheria itakubana kwakuwa haujasajiliwa kisheria kukopesha watu...Haya maneno mawili kama yanafanana hivi lakini mimi nimeshuhudia kwamba yanaweza kutumika tofauti kisheria na yakaleta maana tofauti
Ushauri wangu fanyianeni fair tu mrudishie vitu vyake chukua hela yako kama hamkugombana
 
Ikiwa mtu kaja kwangu kutaka nimkopeshe hela kama laki nayeye kakubali kuleta kitu cha thamani ya hela au zaidi na tukaandikishana ili kama hatalipa kwa wakati vitu vinakuwa wangu.

Sasa ikapita muda wa makubaliano anakuja kudai nimpe vitu anipe hela wakati muda umepita je hapo kisheria ipoje?

Kama kwenye mkataba mliandikishana unamuazima kiasi cha fedha kwa dhamana ya hivyo vitu basi kisheria una nguvu!

Na kama mmeandikishana kwamba unamkopesha na riba basi sheria itakubana kwakuwa haujasajiliwa kisheria kukopesha watu...Haya maneno mawili kama yanafanana hivi lakini mimi nimeshuhudia kwamba yanaweza kutumika tofauti kisheria na yakaleta maana tofauti
Ushauri wangu fanyianeni fair tu mrudishie vitu vyake chukua hela yako kama hamkugombana
Inategemeana na Namna mtakavyozungumza ,lakini kama makubaliano yalifanyika Kwa kufuata taratibu za kisheria utakuwa na haki ya kuendelea kushikilia msimamo WA makubaliano isipokuwa itaonekana batili indepo TU thamani ya Mali iliyowekwa dhamana ikiwa inathamani maradufu kuzidi Deni na muda nao utaangaliwa.
 
Back
Top Bottom