Shujaa Nduna
JF-Expert Member
- Sep 8, 2022
- 599
- 487
Kisheria huna nguvu,mrudishie tu ila inatakiwa akufikilie tuIkiwa mtu kaja kwangu kutaka nimkopeshe hela kama laki nayeye kakubali kuleta kitu cha thamani ya hela au zaidi na tukaandikishana ili kama hatalipa kwa wakati vitu vinakuwa wangu.Sasa ikapita muda wa makubaliano anakuja kudai nimpe vitu anipe hela wakati muda umepita je hapo kisheria ipoje?
Ikiwa mtu kaja kwangu kutaka nimkopeshe hela kama laki nayeye kakubali kuleta kitu cha thamani ya hela au zaidi na tukaandikishana ili kama hatalipa kwa wakati vitu vinakuwa wangu.
Sasa ikapita muda wa makubaliano anakuja kudai nimpe vitu anipe hela wakati muda umepita je hapo kisheria ipoje?
Inategemeana na Namna mtakavyozungumza ,lakini kama makubaliano yalifanyika Kwa kufuata taratibu za kisheria utakuwa na haki ya kuendelea kushikilia msimamo WA makubaliano isipokuwa itaonekana batili indepo TU thamani ya Mali iliyowekwa dhamana ikiwa inathamani maradufu kuzidi Deni na muda nao utaangaliwa.Kama kwenye mkataba mliandikishana unamuazima kiasi cha fedha kwa dhamana ya hivyo vitu basi kisheria una nguvu!
Na kama mmeandikishana kwamba unamkopesha na riba basi sheria itakubana kwakuwa haujasajiliwa kisheria kukopesha watu...Haya maneno mawili kama yanafanana hivi lakini mimi nimeshuhudia kwamba yanaweza kutumika tofauti kisheria na yakaleta maana tofauti
Ushauri wangu fanyianeni fair tu mrudishie vitu vyake chukua hela yako kama hamkugombana