Sheria 17 za soka na ufafanuzi wake

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
Sheria 17 za Soka na Ujio wa Teknolojia Viwanjani.........

Katika soka kuna sheria mama 17 zinazounda mpira wa miguu (soka) na kanuni zake nyingi zinazozitafsiri.

1. Uwanja 2. Mpira 3. Idadi ya wachezaji 4. Mavazi na vifaa vya michezo 5. Referee 6.Wasaidizi wa referee . 7. Muda wa Mchezo 8.Kuanzisha na kusimamisha mchezo 9. Mpira ulio na usio mchezoni 10. Goli 11. Kuotea( offside) 12.Faulu 13.Mapigo Huru( freekikcks) 14. Penati 15.Mipira ya kurushwa 16. Golikiki 17. Kona.

Kati ya sheria hizi kuna sheria mbili ambazo zinawasumbua na kuwatesa sana watu wa soka kwa miaka mingi.

1. Sheria Namba 10 inayofafanua nini maana ya Goli( wakati gani litahesabika ni goli na wakati gani sio goli)

2. Sheria namba 11 ya kuotea ( offside)..

Sheria hizi zimeleta shida sana katika historia ya soka....Watu wengi (hasa marefa) wamepoteza maisha na kupata ulemavu sababu ya kutafsiri hizi sheria mbili.

Nchi zilizoendelea waliamua kutafuta solutions za haya matatizo ya msingi na kuokoa maisha na heshima za watu...Ndo maana walileta GOAL LINE TECHNOLOGY( GLT) NA VIDEO ASSISTANT REFEREE( VAR.).

Tatizo limebaki kwa nchi masikini ......Bado Waamuzi wanapoteza heshima,wanakuwa walemavu na wengine wanapoteza maisha kabisa.

Hakuna sheria ngumu kuitafsiri kama ya Kuotea( Offside) hasa kama waamuzi hawatumii Video kureverse matukio....Hata mshabiki wa soka asipoona replay ni ngumu sana kuitafsiri hii.

Japo Ujio wa Teknolojia unaleta ubaguzi kwenye soka maana Kabla ya teknolojia mpira uliokuwa unachezwa sumbawanga ulikuwa sawa tu na mpira unaochezwa pale London Uingereza....Goli tata likifungwa Misungwi ilikuwa sawa tu na goli tata lililofungwa na maradona pale Mexico wc 86. Kwa sasa soka limetutenga masikini na tajiri..Nani ataweka VAR pale Kinesi?....Nani ataweka VAR pale Tandika kwenye ndondo?

Tusilaumu mareferee na tuondoe dhana ya kupendeleana. Tutafute solution ya haya matatizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naweza kupata pdf ya hiz sheria ?
 
Title na contents haviendani kabisa mleta mada
 
Umekua kama vichanel vya waandishi uchwara wa youtube.
Utakuta heading inasema "Diamond amuoa Kajala" af ukija kwenye content ni wimbo wa msanii gani sijui wa huko Nanjilinji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…