Sheria: Ajira na mikopo

Mti wa Chuma

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2015
Posts
331
Reaction score
99
Habari msoma wa uzi huu,

Ni matumaini yangu u bukheri ya afya.

Kama kichwa cha uzi inavyosomeka, naomba kufahamu kama mtu anaweza kuacha kazi (ajira) akiwa anadaiwa mkopo kazini kwake.

Kwa kiufupi:
Iko hivi; Kuna rafiki yangu anataka kuacha kazi ya ajira ili afanye shughuli zake. Sasa tatizo aliwahi kuchukua mkopo wa mtu kazini kwake ambayo makato ni kwenye mshahara wake kwa kila mwezi, hadi sasa anapotaka kuacha kazi bado anadeni la sh340,000.

Mimi nimeshindwa kumpa ushauri wa kutosha kwa kuwa sina utaalamu wa sheria ya ajira na mikopo, japo nilimshauri asiache kazi hadi amalize deni.

Kwa wanaofahamu zaidi naombeni mchango wenu
 
Mkuu hii ni ngumu sana ila asiache kazi. Dah! wengine wanachezea kazi wakati kupata kazi ni vigumu
 
Mkuu hii ni ngumu sana ila asiache kazi. Dah! wengine wanachezea kazi wakati kupata kazi ni vigumu

Nafikiri amefanya " Cost - Benefit Analysis" ndo akafikia maamuzi hayo, kuna watu wengi sana wanachukua maamuzi ya hivyo maana unaweza ukakuta unapoteza badala ya kupata. Hivyo siyo ajabu.
 
Nashauri afanye yafuatayo;-
(a) Alipe deni lote ili aondoke salama vinginevyo anakaribisha mazingira ya utapeli/kujipatia pesa kwa udanayifu.
(b) Amjulishe Mwajiri wake juu ya dhamira yake ya kuacha kazi wakubaliane utaratibu wa malipo akiwa nje ya Ajira.
(c) Aombe kusamehewa Deni/Mkopo husika.
 



Ahsante mkuu ushauri mzuri sana huu.
 
Huyo jamaa alipe deni ndo aache kazi, sisi waswahili hua tunatatizo la kurokua waaminifu sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…