Shadow, naona leo hauko direct.
Ni hivi:
Awali ya yote, hakukuwa na mjadala juu ya maana ya neno pornography katika mwamvuli wa sheria za Tanzania. Na hata kama ingekuwepo, nisingeshawishika na "authority" ya Black's Law Dictionary. Sio tu kwamba ni kamusi ya mfumo wa kigeni, bali hata huko ugenini kwenyewe hakimu wa Kimarekani anapokuwa na utata katika kutafsiri maana ya neno (kama maana ya kisheria au kitaalam haijulikani) kitu cha kwanza anafanya ni kutafuta "the ordinary meaning of the word," hivyo anavuta a Websters! Akitoka hapo mchezo wa dictionary umekwisha, anaenda kwenye step nyingine ya kutafsiri sheria, statutory construction, kama vile kutafuta nia ya wabunge, legislative intent. Kwa hiyo tafadhali tuweke pembeni uchambuzi wa kigeni hapa, hususan kutumia "authority" zisizo authority.
La pili, Waziri hawezi kupewa nguvu ya kuandika regulations zinazo kataza pornography kwa kigezo cha ku regulate ethics za uandishi kwa sababu ethics za profession huwa ni tenuous, debatable, principles even within the field itself, huwezi kumfungisha mtu jela kwazo. Bunge ndio linaandika, lina define vitendo au kutokutenda kunakotengeneza a criminal offense, linaweka mens rea, penalty, actus rea and all that good stuff. Vitu anavyoruhusiwa Waziri ku regulate sio pornography:
Section 53, Newspaper Act, 1976
The Minister may make regulations for the better carrying into effect the purposes and provisions of this Act, and without prejudice to the generality of the foregoing, may make regulations:
(a) prescribing the forms of registers, returns, applications notices and bonds, and other forms to be used under this Act;
(b) prescribing the particulars and other matters to be entered in the registers:
(c) prescribing the place and manner of keeping copies of newspapers delivered to the Registrar under this Act, or the manner in which and the purposes for which any such copies shall, consistently with the purposes and provisions of this Act, be dealt with or disposed of;
(d) prescribing the information to be furnished to the Registrar by way of periodical return or otherwise;
(e) prescribing the particulars and matters to be published by the Registrar and the manner of such publication;
(f) prescribing the fees which may be levied under this Act,
(g) Prescribing anything which under this Act is to be or may be prescribed.
Tatu, unasema "hakuna set ya sheria Tanzania ambayo inasimamia kusambaza, kununua au kumiliki pornographic materails" lakini hukuonyesha ni lini wamefuta prohibition ya "Traffic in Obscene Publication" under the Penal Code:
Traffic in Obscene Publication
Penal Code, Sect. 175 (1 )
Any person who:
(a) for the purpose of or by way of trade or for the purpose of distribution or public exhibition, makes, produces or has in his possession any one or more obscene writings, drawings, prints, paintings, printed matter, pictures» posters, emblems, photographs, cinematograph -films or any other objects or any other object tending to corrupt morals:
(b) for any of the purposes above mentioned... in any manner whatsoever puts any of them in circulation; or
(c) carries on or takes part in any business, whether public or private, concerned with any such matters or things... or distributes ...or exhibits...in public
(d) advertises or makes known by any means whatsoever with a view to assisting the circulation of, or traffic in, any such matters or things…
(e) publicly exhibits any indecent show or performance or any show or performance tending to corrupt morals,
is guilty of a misdemeanour, and is liable, to imprisonment for two years or to a fine of two thousand shillings.
La nne, section 138 A of SOSP Act inayosema "Any person who, in public or private commits, or procures any act of gross Indecency is guilty of an offence" haiongelei pornography kwa sababu kinachokuwa criminilized hapa ni "gross indecency." Ukurasa wa mbele, wa mwanzo kabisa katika sheria hii ume define
"gross indecency" means sexual act that is more than ordinary but falls short of actual intercourse and may include masturbation and indecent physical contact or indecent behaviour without any physical contact.
Kwa hiyo ukiuza gazeti la kikubwa, kwa mfano, hiyo provision haikuhusu, ila mkono wa sheria utakufikia kutumia Penal code, section 175 inayokataza biashara za usambazaji wa obscene material. Kwa upande wa child pornography ni SOSP Act sect. 138 B na sio "gross indecency" provisions za section 138 A. Hiyo 138 A inakataza kugusana, kujigusa, au kuwa na tabia freaky freaky!
Bm21, heshima mbele. Unasema mmoja aandike summary. Well, obviously hakuna makubaliano, lakini hata yangekuwepo nisingekubali falsafa yako ya kuwaachia "wanasheria...mnaojua zaidi" watoe hitimisho la wote. Isitoshe, mimi si mwanasheria wala mwana chochote. Lakini hata mahakamani kuna wazee wa baraza ambao wanachambua smokescreen na bullcrap za wanasheria. Tazama bullcrap za Andrew Chenge na smokescreen za Pinda, Masha, Sitta, Simba, na wanasheria wengine tuliowaamini kuendesha meli. Katika enzi hii ya mapinduzi ya habari atakaekuja akasema "mimi ndiye yule ajae kuwaletea habari njema na neno la kweli, kwa maana nalikufa mtini kwa ajili yenu" ataambiwa "onyesha mbavu."
I am done talking.