Sheria hii ya zimamoto si kwa manufaa ya taifa

Sheria hii ya zimamoto si kwa manufaa ya taifa

sangu mnene

Member
Joined
Sep 5, 2012
Posts
92
Reaction score
35
Kati ya mashirika ya umma hapa nchini yenye ufanisi wa chini na utendaji unaoshangaza ni idara ya ZIMAMOTO (FIRE BRIGADE).Ikitokea tukio la moto ndipo utakapowashangaa ZIMAMOTO,kwanza watachelewa kuja,pili watakuja ama na maji kidogo au bila maji kabisa,tatu wasipopata msaada wa Zimamoto zingine kama zile za Dandari,Airport au za watu binafsi si ajabu moto ukawashinda.Wananchi hawana imani tena na idara ya ZIMAMOTO,ukitokea moto huzima wenyewe au kuomba msaada wa zimamoto toka airport au bandari.Hakika zimamoto wanashangaza sana tena sana.

Wahenga walisema,'ukishangaa ya Musa hujaona ya Filauni'.Mala baada ya kumaliza kufundisha somo la kemia,mada ya uzimaji moto (Fire fighting),mwalimu mmoja wa shule kongwe ya serikali iliyopo jijini Mbeya,alishitushwa na uelewa mdogo walionao wanafunzi,walimu na wafanyakazi wasio walimu kuhusu masuala mazima yahusuyo kuzuia na uzimaji moto.Walikubaliana na uongozi wa shule kuwa wawaombe idara ya zima moto Mbeya waje watoe elimu ya kuzuia na kuzima moto.Waliamini kuwa watatakiwa kama shule ya serikali kununua vifaa (Fire extinguisher) na labda kuweka mafuta kwenye gari la zimamoto ili lifike shuleni umbali wa km 2 tu toka idarani.Alipofika Idara ya zimamoto na kuwaeleza ombi la kuwataka waje watoe elimu kwa wanafunzi wa Mbeyaday takribani 1670 na wafanyakazi kama 130 hivi juu ya uzuiaji na uzimaji wa moto,walitakiwa watoe malipo ya sh 20,000/- kwa kila mwanasemina,yaani jumla ya sh (1800 x 20,000) yaani watoe jumla Tsh 36,000,000/-.

Msemaji alimsisitizia mwalimu kuwa sheria iliyopitishwa na bunge inawataka kuchaji sh 20,000/-kwa kila mwanafunzi wa shule wanayoenda kutoa mafunzo ya uzimaji moto.Hivyo ili tuje kutoa mafunzo ambayo yanaweza kuchukua saa moja au masaa mawili inabidi shule yenu ya serikali ya mbeyaday itoe jumla ya milioni 36 tu,bila hivyo hatutakuja kuwaonyesha namna bora ya matumizi ya fire extinguisher.Ajabu alipowasiliana na kitengo cha zimamoto uwanja wa ndege wao walikubali kutoa elimu hiyo bure.Hakika inashangaza.

Sasa ndugu zangu wana JF;
  1. Kwa nini Bunge lilipitisha sheria ya hovyo namna hii?
  2. Kwa nini zimamoto wa airport,bandari hata watu binafsi watoe elimu bure lakini idara ya zimamoto itake malipo makubwa kiasi hicho?
  3. kama wanafunzi wasipopata elimu ya kujikinga na uzimaji bora wa moto,ujuzi huo utasambaa vipi?
  4. Je ni sawa idara ya zimamoto kuwalaumu wananchi kwa kutotoa ushirikiano wakati wa kuzima moto wakati wao wenyewe hawatoi elimu kwa wananchi bure?
  5. Kwa nini idara nyingine katika wizara ya mambo ya ndani hutoa elimu bure na hasa kwa wanafunzi (taifa la kesho) wao hawataki.Mfano?; Polisi hutoa elimu ya Polisi rafiki bure mashuleni.
  6. Je,ni sawa kwa idara moja ya serikali kudai malipo kwa idara nyingine ya serikali kila itoapo elimu?
  7. Ninini kifanyike ili kuondoa kabisa ubabaishaji wa idara ya ZIMAMOTO?

Haya maelezo nilipewa na mwalimu anayefundisha shule ya serikali kongwe kabisa ya Mbeyaday,inawezekana kukawa na udhaifu mwingine ambao hatuujui juu ya hii idara dhaifu kabisa ya ZIMAMOTO,kama upo udhaifu mwingine tuuwasilishe kwa nia ya kuiboresha idara hii nyeti ya ZIMAMOTO.Nawasilisha!
 
haaaaahaaaaah mbona ukitaka kumwona daktari unalipa elfu kumi hata kamq umetoka idara ya serikali?
 
Maelezo yako ni marefu sana,japo yana mantiki ya kuyajadili kwani mimi nikiwa kama mdau wa Zimamoto nimeona tayari wewe una mtazamo hasi na Zimamoto ebu angalia sentesi zako hizi "...Ikitokea tukio la moto ndipo utakapowashangaa ZIMAMOTO,kwanza watachelewa kuja,pili watakuja ama na maji kidogo au bila maji kabisa,tatu wasipopata msaada wa Zimamoto zingine kama zile za Dandari,Airport au za watu binafsi si ajabu moto ukawashinda..."
Naomba niambie utajuaje kuwa wamekuja na maji kidogo? uliwahi kuchungulia kwenye tenki la gari au unasimulia habari za kwenye vijiwe va kahawa? Je kama gari limekuja na maji ya kutosha yanaweza kuisha baada ya muda gani? Au maji hayatakiwi kuisha kwenye gari hadi moto uzimike?
Kuhusu kutoa elimu hapo kuna udhaifu kwani kuna training na kuna demonstration,inaonekana shule walitaka demostration ambayo hutolewa bure ila wenyewe waliomba training ambayo hulipiwa tena zaidi ya ulivyoainisha kwani kuna gharama nyingine zinaongezeka ukiacha hiyo ada ya kichwa.
 
Back
Top Bottom