Mr Ntinginya
Member
- Apr 26, 2024
- 24
- 29
Nianze makala hii kwa kutoa mfano halisi ambao nilikutana nao mimi mwenyewe. Siku moja nilikutana na tafrani kati ya dereva bajaji na askari barabara. Kile kilichotukia ni dereva kukamatwa akiwarekodi video askari barabarani wakipokea hongo kutoka kwa dereva wa bajaji aliyekuwa mbele yake.
Simu alipokonywa na kupigwa na askari, watu walikusanyika na hakuna aliyeweza kuwazuia wale askari kufanya walichokuwa wakifanya maana kwa jinsi askari walivyokuwa ni kama wameibiwa silaha yao na wengi miongoni mwa watu walishindwa kuelewa nani wamtetee nani wamwache. Askari walisimamia kuwa ni kosa kisheria kuchukua video.
Mtu mmoja ambaye alionekana ni kama mwanasheria akawaambia askari kufuata sheria, akawaelekeza askari kuwa hawana ruhusa kumpiga yule dereva bali wampeleke kituo cha polisi. Baada ya mda wale askari wakamchukua yule kijana kwenye bajaji yake kwenda kituo cha polisi. Wazo la kwenda kituo cha polisi halikuwa zuri kwa dereva pamoja na kwamba amepigwa, hivyo alijaribu pia kukataa kabla hajakubali kwa shuruti.
Wale askari walikuwa hawashikiki, na nilichokiona kwa watu waliokuwa pale, walianza kuwa upande wa dereva lakini baadae wengi wakawa upande wa askari wakiona kosa la dereva ni kubwa kuliko kupigwa, bora angeelewana nao kuliko kwenda kituoni.
Kwa upande wangu nilimwonea huruma yule dereva huko anakopelekwa, maana ni heri nusu shari kuliko shari kamili. Shari ile ilikuwa inaenda kuwa kamili, kati ya yeye na kituo kizima!
Maswali mengi yalinijia, amekwenda yeye na askari peke yake, nani ataenda kumtetea? Kama wamempiga mbele za watu itakuwaje nje ya umati?
Kwa mhutasari huo niende moja kwa moja kuleta hoja yangu. Nimeona jumla ya sheria zote kuwa ni mbili, sheria ya kuzuia uovu na sheria ya kulinda uovu. Tofauti ya hizi mbili ni kama ifuatavyo.
Sheria za kuzuia uovu; hizi ni sheria zinazuia mtu kutenda uhalifu. Sheria ya kuzuia rushwa, ungang’anyi, kupiga n.k.
Sheria za kulinda uovu; hizi ni sheria juu ya sheria za kuzuia uovu. Ni sheria za kulinda wanaotenda uovu. Sheria hizi zinakinzana kiutendaji na sheria za kuzuia uovu na kwa namna moja ama nyingine, zinalinda uovu. Mimi nikiwa nashudia lile tukio nilibaki na maswali tu, nikisema dereva ana haki sheria inasema haruhusiwi kuchukua video bila ridhaa ya yule mtu. Nikisema askari ana haki sheria; ana haki kwa sababu karekodiwa bila ridhaa yake?
Ukiangalia hayo maswali mawili ndio yanakuwa kiini cha mjadala, na like la askari kula rushwa linakuwa kama limekufa. Hii ni kwa sababu ya ukinzani wa sheria zenyewe. Zinatoa nafasi ya kuzuia uovu kwa 10% huku zikizuia kufunua uovu au kulinda uovu kwa 90%.
Zinalinda wenye mamlaka wasije wakashikwa na hatia. Hata ikiwa mwenye mamlaka anafanya uhalifu mbele yake, huwezi kufanya kitu chochote.
Hairuhusiwi kumrekodi mtu bila ridhaa yake, kuna sheria inayokataza kumhalilisha mtu mtandaoni kwa namna yoyote. Nitaenda kumripoti bila uthibitsho? Nikichukua uthibitisho nitachukuliwa hatua ya kukiuka sheria na nitakuwa hatiani tena nitakuwa mfano kwa wengine. Wenye mamlaka kiufupi wako juu ya sheria mpaka watakaposhindwa kufanya hivyo. Namdhalilisha kwa lipi? Bora ni lipi, nimdhalilishe au nimwache aendelee kula rushwa hazarani?
Chukua mfano dereva huyu wa bajaji amemwona huyu askari anaomba hongo akamrekodi na askari alipoona, akamtia hatiani dereva. Dereva huyu hakuna kituo cha polisi atapelekwa na akaonekana ana haki. Atakuwa kitoweo kwa namna yoyote. Sheria ya kumlinda anayetenda uovu hapa inakuja juu zaidi kulingana na mamlaka ya aliyetenda uovu.
Mimi nikivunja sheria, atatumwa askari mara kunikamata lakini mimi nikimwona askari anavunja sheria nitamtuma nani kumkamata? Nilipoti takukuru kwa uthibitisho upi?
Siku zote itabaki kuwa wanaotenda uovu ni watu wa kawaida, wa hali ya chini. Hao ndio sheria imetungwa kwa ajili yao. Maana sheria inawahukumu wakitenda kinyume na sheria aidha kwa kutenda uovu ama kunyooka mikono yao juu ya wenye mamlaka wanaotenda uovu. Na mamlaka zitakuwa mlagoni kuwaburuza haraka sana kwa sababu wanayo nguvu kisheria na kimamlaka.
Sheria ya kulinda uovu imepewa nguvu kuliko sheria ya kuzuia uovu. Nirude kwa yule dereva na wale askari, kuna sheria inayomlinda askari au kiongozi kuchafuliwa na sheria inayomzuia askari kula rushwa ambayo dereva kwa kuijua aliamua kuchukua uthibitisho huo.
Hiki ndicho nilichokiona siku ile na ndicho naendelea kukiona kila mahali. Na ndipo kilipo kiini cha uovu ambao hautakaa uishe.
Dereva alichukua video kwa lengo zuri kama ambavyo askari alivyokuja kusimama barabarani. Lakini sheria ya kumlinda askari muovu ina nguvu kuliko sheria ya kuzuia uovu anaoufanya. Nakumbuka pia tafrani kama hii ilitokea zanzibar ambapo mtalii alichukua video ya askari akiomba rushwa na askari yule aliadhibiwa, askari aliadhibiwa nadhani ni kwa sababu ya ile video lakini baadae mtalii akachukuliwa hatua. Ni sheria ambazo hazina maana yoyote. Yule mtu kama si kurekodi ile video hana namna nyingine ya kufikisha hilo tukio. Hawezi kwenda kituo cha polisi kuripoti hilo tukia, angejitafutia matatizo yeye mwenyewe.
Karipio kwa mtu aliyefunua uovu kwa njia isiyo sahihi linapewa nguvu na kipao mbele cha aina yake kuliko yule mwovu. Somo tunalokuwa tunajifunza huku chini ni kuwa kufunua uovu ni kujitoa mhanga. Na mamlaka ndicho wanachokitaka kwetu, tuogope na tusithubutu kufanya hivyo. Lakini kwa sura ya nje wanaonekana kuhimiza tusifiche uhalifu. Kwa hiyo uhalisia unabaki kuwa kuna ganda na mbegu yenyewe. Lakini mamlaka zinatuaminisha ganda la mbegu ndio mbegu.
Mapendekezo yangu ndani ya miaka mitano ijayo juu ya nini kifanyike,
Sheria iruhusu kurekodi na kuisambaza hiyo video ikiwa inahusu rushwa.
Kutokana na nguvu ya ukinzani kutoka kwa wenye mamlaka, kuwe ruhusa kuwarekodi na kuituma video mitandaoni kama sehemu ya kufikisha ujumbe wenye uthinitisho kwa mamlaka husika.
Hii itapunguza hatari ya kudhulika yule anayefunua uovu.
Tukumbuke haki na uovu zipo katika mzani mmoja, kutaka kuzibalansi zote ziwe sawa ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu. Sharti kama tunataka haki basi anaekula rushwa amejidhalilisha yeye mwenyewe. Sijamdhalilisha kwa kufunua uovu wake mbele ya watu. Haiitaji mbeleko hata akae mgongoni kufarijiwa kwa kudhalilishwa.
Itapaswa kuwepo marekebisho ya sheria zinazofungamana na uovu. Ili kuepuka kuzunguka mbuyu, ni lazima kuchunguza na kuondoa sheria zinazotetea au kulinda na kuwapa haki wahalifu. Hapa nimetolea mfano wa askari tu, lakini zipo mamlaka hata ukizitaja hapa tayari unakuwa unataftwa.
Uovu umezungukwa na kulindwa na sheria, waovu wanataka haki itendeke; kwa maana ya kufuata sheria ili kulinda uovu.

Upvote
2