Bashir Yakub
Member
- May 27, 2013
- 96
- 1,745
SHERIA INAKATAZA KUOA AU KUOLEWA NA X WA BABA AU MAMA YAKO.
Bashir Yakub,WAKILI
+255714047241.
Kifungu cha 14 Sheria ya Ndoa kinakataza kumuoa au kuolewa na mtu yeyote aliyewahi kuwa mke au mme wa baba yako au mama yako. Na hii ni hata kama walishaachana miaka mingi sana.
Jambo hili ni kosa kama makosa mengine ambalo linastahili adhabu kwa mujibu wa kifungu hicho.
Aidha, ni makosa pia kumuoa au kuolewa na Mpwa wako, kuoa au kuolewa na babu au bibi yako wa upande wowote. Kuoa au kuolewa na mjomba au shangazi.
Hapo kwa bibi na babu pia hata mtu yeyote aliyewahi kuoa au kuolewa na bibi au babu yako, yaani X wa bibi au babu yako huruhusiwi kumuoa au kuolewa naye.
Pia mtoto uliyemuasili(adopt) ni makosa kumuoa au kuolewa naye.
Nyongeza ya makatazo ni wale ambao kawaida tunawafahamu kwamba inakatazwa kwa baba, mama, kaka, dada.
Isipokuwa sheria imesisitiza kuwa hata awe dada au kaka wa nje ya ndoa ni kosa pia.
Haya yote juu kifungu hiki kimeyaita MAHUSIANO YALIYOKATAZWA(Prohibited Relationships).
Ni muhimu kuyajua haya hasa sasa ambapo mtu na shangazi au mjomba au mpwa wote ni vijana wadogo ambao wanalingana umri na pia unakuta wana mazoea kupita kiasi.
Tofauti na zamani ambapo ukiambiwa mjomba au shangazi ni shangazi kweli. Ni mtu mzima haswa.
Siku hizi hata mtu na mkwe au mjukuu unakuta wote ni vijana au wamepishana kidogo.