Sheria inaruhusu kudai zawadi ulizotoa kwa Mchumba wako pale Uchumba unapovunjika

Sheria inaruhusu kudai zawadi ulizotoa kwa Mchumba wako pale Uchumba unapovunjika

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2013
Posts
735
Reaction score
1,467
SHERIA IMERUHUSU KUDAI ZAWADI ULIZOTOA UCHUMBA UNAPOVUNJIKA.

Una mahusiano na mwanaume au mwanamke ambaye kimsingi mpo katika uchumba. Unampa zawadi nyingi naye anakupa zawadi. Mnayo ahadi ya kufunga ndoa na kuishi kama mme na mke . Na kwasababu hiyo unajitoa sana kimatumizi kwa mtu huyo.

Lakini katika mazingira usiyoyaelewa unaona sasa mambo hayaendi vizuri. Hayaendi vizuri katika kiwango ambacho sasa mahusiano yamevunjika kabisa. Hakuna tena mahusiano. Au bado yapo lakini kwa mambo unayofanyiwa unaona kabisa hutakiwi tena.

Kumbuka huko nyuma umegharamia sana. Umegharamia kwa fedha na mali. Swali ni je vitu hivi haviwezi kurudishwa ?. Vitu hivi haviwezi kufidiwa ?. Na je sheria imeongelea kuhusu jambo hili ?.

Majibu ya maswali haya yote ni ndiyo. Ni ndiyo, na gharama pamoja nazo zawadi zinaweza kurejeshwa. Unaweza kushangaa kuona sheria imeongelea hata mambo ya uchumba lakini ndio ukweli.

Wengi tunaijua sheria katika kuongelea wizi, dhamana, mikataba, mirathi, ndoa, na mengine. Lakini ni vyema tukajua kuwa sheria ni pana na imeongelea mambo mengi mno. Hili la uchumba nalo ni sehemu ya yaliyoongelewa.

1. KUVUNJA UCHUMBA

Kifungu cha 69( 1 ) cha Sheria ya Ndoa iliyofanyiwa marekebisho 2010 kinasema kuwa mtu anaweza kufungua shauri na kudai fidia baada ya uchumba kuvunjwa.

Kwa haraka utaona kuwa tafsiri ya kifungu hiki sio kufungua shauri ili kumlazimisha mtu akurudie, hapana. Mahakama haiwezi kutoa maamuzi kuwa fulani lazima amrudie fulani. Isipokuwa lengo lake ni kumtaka yule aliyeumizwa katika hili kudai fidia kutokana na maumivu aliyoyapata. Hapa hatujaongelea kurudisha zawadi.

Kudai fidia na kurudisha zawadi ni vitu viwili tofauti. Fidia inahusu kulipwa maumivu uliyoyapata kutokana na tukio hilo la kuachwa pamoja na muda uliopoteza na huyo mtu. Wakati zawadi ni kurejesha kile ulichotoa. Kwahiyo la zawadi tutaliona baadae.

Aidha masharti ya kufungua shauri la kudai fidia ni kuwa , moja anayefungua shauri awe ni yule aliyeumizwa, pili ahadi ya kuoana lazima iwe ilikuwa imefanyika Tanzania, tatu wakati mnaingia kwenye mahusiano iwe mlikuwa nyote mmetimiza miaka 18 .

2. KURUDISHA ZAWADI.

Kifungu cha 71 cha Sheria ya ndoa kinasema kuwa mtu anayo haki ya kufungua shauri kudai kurejeshewa zawadi ambazo alizitoa kwa mtu ambaye alikuwa ana ahadi ya kufunga naye ndoa lakini ndoa haikufungwa.

Zawadi ni pamoja na fedha, nyumba, magari, nguo na kila kitu chenye thamani(valuable). Haijalishi mali hiyo ipo kwenye jina la nani suala la msingi ni kuthibitisha kuwa wewe ndiye uliyetoa hiyo zawadi.

Shauri la namna hiyo unaweza kulifungua mahakama yoyote ya mwanzo, ya wilaya, ya hakimu mkazi au hata mahakama kuu. Itategemea na thamani ya kiwango cha mali unazodai.

Kama mali hizo zitakuwa zimekwishatumika au hazipo tena pengine zimeuzwa au kutolewa zawadi kwa mtu mwingine basi itatakiwa kulipwa fedha zinazolingana na mali hizo au mali hizo zikanunuliwe tena kwingine ili kumrudishia anayedai.

Ukishindwa kabisa kurudisha basi mali zako binafsi ambazo hazikuwa sehemu ya zawadi zitauzwa ili kupata kiwango kinachodaiwa na kama huna mali yoyote ya kuuza utatakiwa kwenda jela kama mfungwa wa madai.

Kwa hiyo watu wanatakiwa waelewe kuwa uchumba na ahadi za kuoana si jambo jepesi kama wanavyolitamka na kuliahidi.

Karibu kwa maoni
 
What's about wale wanaoingia kwenye promise of marriage kabla ya ku attain age of majority?

Bearing in mind that in accordance to our laws a person under the age of 18 years can contract a marriage vipi kuhusu hao?
 
71. Right to return of gifts
A suit may be brought for the return of any gift made in contemplation of a marriage which has not been contracted, where the court is satisfied that it was made with the intention on the part of the giver that it should be conditional on the marriage being contracted, but not otherwise.

69. Right to damages for breach of promise of marriage
(1) A suit may be brought for damages for the breach of a promise of marriage made in Tanzania whether the breach occurred in Tanzania Tanzania or elsewhere, by the aggrieved party or, where that party is below the age of eighteen years, by his or her parent or guardian:
Provided that–

(a) No suit shall be brought against a party who, at the time of the promise, was below the age of eighteen years;

(b) No damages shall be awarded in any such action in excess of loss actually suffered as a result of expenditure incurred as a direct result of the promise.

(2) A suit may similarly be brought in respect of the breach of a promise of marriage made in any other country but only if such an action would lie under the law of that country as well as under this Act.

(3) No suit shall be brought for specific performance of a promise of marriage.

Note Section 69 (1)b and Section 69 (2)

So gift zitakazorudishwa ni zile ambazo it was stated clearly ukiwa unampa kwamba you can keep this on condition that we get married, hizi za kupeana hovyo hovyo wanasema in consideration (exchange) of love and affection hazirudi.
 
Kuna mwanaume mmoja hapa kamuacha mkewe kamrudisha kwao lakini hataki kumpa vitu vyake (Yaani nguo pamoja na viatu na vipodozi n.k)

Je anaweza kumshtaki? Kama ndio ni wapi?
 
Je uchumba unaotambulika kisheria ni upi?

Maana wengine mfano wanavyuo wanadanganyana huku wanafanya ngono.

Kumbe mwanamke anatafuta unafuu wa kimaisha chuoni na kusaidiwa kuvuka kimasomo na mwanaume. Hata wazazi pande zote hawajui.

Je mwanaume atarudishiwa vipi nguvu zake kiakili kumfundisha mwanamke?

Tulipokuwa chuoni wanawake wengine walikuwa wanafanyiwa homework na wanaume.
 
Back
Top Bottom