Sheria inasemaje fundi anapokamatwa na vitu vya wizi katika karakana yake?

yutu

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2013
Posts
1,668
Reaction score
1,017
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu hivi majuzi nilipata nafasi ya kuudhuria kesi ya jiran yangu ambaye ni fundi radio aliyekamatwa na vitu vya wizi katika ofisi yake ya kazi, wiki moja kabla hajaletewa radio hiyo ya mtumba aina ya kenwood yalivunjwa maduka matatuna wezi kuiba vitu mbalimbali ikiwemo hiyo radio. baada ya siku chache kupita ndipo alipoletewa radio hiyo kwa matengenezo ya jicho la cd kutokusoma na kumuahidi mteja wake huyo aje kesho yake itakuwa tayari lakini ilipofika kesho akashangaa jamaa mmoja amekuja na maaskari na kuwaonyesha wale maskari radio bila ajizi wale maaskari wamlim'bebesha ile radio na kumpeleka kituoni na wakagoma kumpa dhamana siku iliyofuata walimpandisha kizimbani na kusomewa shtaka la kuvunja na kuiba kinyume cha sheria. naomba kujua kutoka kwa wataalam sheria inasemaje kuhusu hilo, je ni sahihi mafundi kuandikishiana na wateja wao pale wanapopeleka radio, simu, tv nk. kwa matengezo ikitokea mteja ajaonekana na mali ya wizi imepatikana kwa fundi huyo si atakuwa mtuhumiwa wa kwanza na kwasababu amekamatwa na kizibiti hukumu yake itakuaje?
nitashukuru kwa majibu mazuri
 
Kwanza tambua kuwa swala la wiz linamshiliki wake fundi anaweza kuwashiliki kwa maana ya kwamba ndo aliekamatwa na mzigo husika kwake kitakachohitajika ni kutoa maelezo ya kutosha kuwa redio hiyo ilikuwa ya nan na anapatikana wapi hivyo yeye awe mwenye kusaidia ukamataji na ikitokea mhalifu akakana mkamatwa na ngoz ndie mla nyama na atashitakiwa kama wengine
 
Ni hivi ukae ukijua hata gari achana na tv mwenye office ya lutengeneza chochote kile anatakiwa kuwa na hivi vitu; register, job card, delivery note baada ya hapo ukiwa navyo hivi hata aje nani wewe huwezi kuingia hatiani kwani umekamilisha taratibu zote kisheria! Kama huna na wewe ni mwizi tu.
 
read the sale of goods act
24. Market overt
Where goods are openly sold in a market established by law in Tanzania in the ordinary course of the business of such market, the buyer acquires a good title to the goods provided he buys them in good faith and without notice of any defect or want of title on the part of the seller.

26. Revesting of property in stolen goods on conviction of offender
(1) Where goods have been stolen and the offender is prosecuted to conviction, the property in the goods so stolen revests in the person who was the owner of the goods, or his personal representative, notwithstanding any intermediate dealing with them, whether by sale in accordance with the provisions of section 24 or otherwise.
(2) Notwithstanding any written law to the contrary, where goods have been obtained by fraud or other wrongful means not amounting to theft, the property in such goods shall not revest in the person who was the owner of the goods or his personal representative, by reason only of the conviction of the offender.

27. Resale by seller or buyer or the agent of either party in possession after sale
(1) Where a person having sold goods continues or is in possession of the goods, or of the documents of title to goods, then the delivery or transfer, by that person, or by mercantile agent acting for him, of the goods or documents of title, under any sale, pledge or other disposition thereof to any person receiving the same in good faith and without notice of the previous sale, shall have the same effect as if the person making the delivery or transfer were expressly authorised by the owner of the goods to make the same.
(2) Where a person having bought or agreed to buy goods obtains, with the consent of the seller, possession of the goods or the documents of title to the goods, the delivery or transfer, by that person or by a mercantile agent acting for him, of the goods or documents of title, under any sale, pledge or other disposition thereof, to any person receiving the same in good faith and without notice of any lien or other right of the original seller in respect of the goods, shall have the same effect as if the person making the delivery or transfer were a mercantile agent in possession of the goods or documents of title with the consent of the owner.
(3) In this section, the term "mercantile agent" means a mercantile agent having, in the customary course of his business as such agent, authority either to sell goods, or to consign goods for the purposes of sale, or to buy goods, or to raise money on the security of goods.
 
Sheria iko wazi kabisa kwamba kama ukikamatwa na kitu cha wizi kitakachokutoa ni kujiekeza kwako,lakini ninavyojua hapa kwetu hawafundishi biashara na sheria zake kwani mtu hajui haki ikoje na inasema nini, kwa mfano huyu Fundi ni lazima awe na kitabu cha kuandika kila anaeleta chombo chochote kwake pia achukue maelezo yote ya mteja kama anuani yake,jina halisi na namba ya simu,ili kama tatizo litajitokeza kama hili ana maelezo ya kujibu na pia kumbukumbu, hapo ndipo tunapokosea huna details eti alieileta alikuwa mfupi kidogo kachomekea halafu kavaa miwani. Hivi hayo maelezo ukiwa wewe hakimu utamuelewa? Mfano mwingine ni kukopeshana kiswahili unamkopa mtu hela halafu harudishi lakini kama ungemsainisha ushahidi tosha jamani tuwaelimishe watu mbona bank unasaini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…