Sheria inasemaje katika hili

Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2009
Posts
13,403
Reaction score
12,775
Nimekua msomaji mzuri sana wa vitabu hadithi za kubuni hususan vya mtiririko wa kina Marehemu Eddie Ganzel...baada ya wale wakongwe kupita kuna vijana wamekuja kuibuka hapa miaka ya karibuni ambao ni matunda ya kina Ganzel na Musiba!

Nimetatizika kidogo siku za hivi karibuni baada ya kusoma kitabu kimoja "Mkakati wa Kuelekea Ikulu" kilichoandikwa na Hussein Wamanywa (niombe radhi km nimekiuka kanuni kutaja) Kilichonitatiza ni kwamba; japo kuna ubunifu kiasi kwa mwandishi kuhitimisha vizuri.. ila sehemu kubwa imekua inawataja watu wanaojulikana wazi wazi km Jakaya Kikwete,Salim Ahmed Salim na timu nzima iliyokua inawania nafasi ya kugombea urais 2005 na taasisi nyingine km CCM,CUF,TLP na nyingine....

Mtiririko huu ungekua mzuri endapo mwandishi angekua ameajiriwa na chama ama akawa ni katibu mwenezi wa chama,kwa kuwatumia watu na taasisi bila kuomba idhini kimaandishi km waandishi wengine wanaoomba radhi itokeapo wanatumia vifungu vyenye kuweza kuibua utata sheria inasemaje katika hili!
 
Kusema kwamba Kikwete ni Raisi au nwanachama wa CCM au Pinda ni waziri mkuu kisheria si kosa kulitaamka wala kuliandika maana ni kweli... Kosa ni kuwachafua majina kama kuwaita mafisadi na ukashindwa thibitisha. Waandishi wanatumia haki yao kikatiba ya uhuru wa kuongea/kujieleza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…