Sheria inasemaje kuhusu baba kumchukua mtoto kutoka kwa mama yake?

dimatteo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2018
Posts
868
Reaction score
932
Habari Wana jf.

Naomba kujua sheria inazungumziaje katika hili,
Yani umezaa na mwanamke ila huishi nae na umelea mimba na mtoto kazaliwa,ukalea mtoto Kwa kila kitu Akiwa na mama yake

Akafikisha umri kama miaka 7 Wa kuanza Darasa la kwanza.

Nataka kujua sheria inasemaje hapa mama akigoma kukupa Kwa kisingizio yeye anaweza kulea hata usipo toa pesa,wakati na wewe unataka katika umri huo apate malezi yako kama Baba,

Je? Baba hatakiwa kumkuza mtoto katika Misingi yake isipo kuwa mana tuu au Baba Kazi yake ni kutoa ela tuu na kumchunguli kwa mbali mpaka pale mtoto atakapo amua yeye..???

Karibuni
 
Katika sheria kinachotazamwa sio issue ya umri tu bali pia swala la ustawi wa mtoto kimakuzi. Unaweza kumchukua mtoto ikiwa sehemu/mzazi mwenza anaishi na mtoto kwamazingira ambayo yanauwezekano mkubwa wakuathiri ustawi wa mtoto.

Nihaki ya mtoto kisheria kupata malezi ya baba na mama, ingawa zipo sababu zinazoweza kupelekea mtoto kukosa malezi ya moja kwa moja ya mama au baba.

Kwa hali inayokukumba unapaswa kukubaliana na mzazi mwenza juu ya namna bora yakumlea mtoto wenu kwa ushirikiano wa moja kwa moja. Mfano mtoto anaweza kusoma akuwa kwa mama lakini kipindi cha likizo akaja kupumzikia kwako.

NB: Mtoto anahaki yakupa malezi ya pandezote mbili.
 
Maelewano, ila ni kheri mtoto abaki kwa mama yake mzazi, maana kama una mwanamke mwingine, mama wa kambo siyo mama...
 
Yaaa, binafsi napendelea mtoto alelewe na mama, isipokuwa kama kutakuwa na changamoto zingine zinazoweza kupelekea mama ashindwe kumlea mwanae.

Ukiwa umeoa mwanamke mwingine halafu ukataka kuishi na mtoto ambae si wamwanamke unaeishinae nikumtafutai majanga mtoto.
 
Tupate wanasheria wenye upeo wa ufahamu huu ,wengi hawajajibu kisheria
 
Kujibu kisheria kupoje labda?
Je kuna acts za kisheria zinazoelezea jinsi ya kudeal na issue kama hizi, mfano wenzetu wana birth certificates za aina mbili kwa mtoto, ya kwanza wanaita unbridged birth certificate hii ina informations za baba mzazi na mama mzazi, issue zote zinazomhusu mtoto lazima zipate ridhaa ya wazazi wote, kusafiri nje ya nchi kwa mtoto wa aina hii inasumbua kama ni mzazi mmoja tu ndio anasafiri naye na wazazi wote wana haki sawa, na pili ni normal birth certificate na hii ina informations za mzazi mmoja hasa mama, mtoto wa aina hii kisheria mama she have a final decision kuhusu mtoto, kwetu hapa Tanzania sijui sheria zinasemaje
 
Mtoa mada amezungumzia swala la kutaka kumchukua mtoto ili kuishinae na kumlea, ndomana nimejibu kulingana na sheria za Tanzania kuhusu swala la malezi ya mtoto na mamlaka ya wazazi juu ya mtoto.

Kwatanzania kila mzazi anayohaki/mamlaka sawa juu ya mtoto. Kinachoangaliwa zaidi katika swala hili niupande upi ambao mtoto akikaa nakulelewa atakuwa na ustawi mzuri.

Kuhusu swala la birth certificate na issue za passport Tanzania kunaaina moja ya birth certificate, maswala ya passport na informations za mzazi kwa watoto waliochini ya umri wa miaka 18 sijajua ni utaratibu upi unatumiwa kufanya approval ya usalama wa mtoto katika kumuwezesha safarizake za njee.
 
Sheria zinazohusika na maswala ya watoto.

1) The Law of Marriage Act. S.125(2), Welfare of the child, wishes of the child, and custom of society. Vitaamua nani aishi na mtoto

2) The Law of Child Act.
 
Mtoa mada amezungumzia swala la kutaka kumchukua mtoto ili kuishinae na kumlea, ndomana nimejibu kulingana na sheria za Tanzania kuhusu swala la malezi ya mtoto na mamlaka ya wazazi juu ya mtoto.

Kwatanzania kila mzazi anayohaki/mamlaka sawa juu ya mtoto. Kinachoangaliwa zaidi katika swala hili niupande upi ambao mtoto akikaa nakulelewa atakuwa na ustawi mzuri.

Kuhusu swala la birth certificate na issue za passport Tanzania kunaaina moja ya birth certificate, maswala ya passport na informations za mzazi kwa watoto waliochini ya umri wa miaka 18 sijajua ni utaratibu upi unatumiwa kufanya approval ya usalama wa mtoto katika kumuwezesha safarizake za njee.
1. Kuhusu baba kumchukua mtoto: Imejibiwa vizuri na wachangia mada hapo juu. Nikazie, Sheria imeweka angalau miaka 7 ya mtoto, Lakini Mahakama kwa kupitia ushahidi na taarifa ya Ustawi wa Jamii huamua ni mzazi yupi atasimamia kwa usahihi malezi na maslahi bora ya mtoto. Kwa hiyo Mzazi mwenye kukidhi atapewa mtoro.

2. Kuhusu mzazi mmoja kuwa na mtoto, akatakiwa asafiri naye. Kuna mamlaka zinasimamia hilo na wanatoa taratibu za kufuata(Uhamiaji na Ustawi wa Jamiii wanataratibu zao.

Kwa uzoefu wangu, Wazazi husika huwa wanajaza fomu. Yule ambaye hakai na mtoto huwa anatoa ridhaa ya kukubali mzaze mwenzake kusafiri na mtoto n.k

Ikiwa mmoja ni Marehemu basi taratibu za Kimahakama, na/au uthibitisho wa jambo hilo huambatanishwa kusaidia taratibu za kusafiri n.k
 
Back
Top Bottom