Sheria inasemaje kuhusu kuacha kazi bila taarifa?

BATULUNGE

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2013
Posts
391
Reaction score
633
Naomba kuuliza je kisheria inakuwaje Kama mwajiriwa ambaye Hana mkataba akaamua kuacha kazi bila kutoa notisi ya mwezi mmoja kabla ya Siku ambayo ameacha laziness,

1. Je Mwajiriwa atawajibika kisheria kutimiza matakwa ya kisheria (km kulipa 1month salary as notice pay) sawa na Yule ambaye anamkataba halali na kampuni?

2. Kama alikuwa yupo kwenye payroll inawezekana case yake ikawa na uzito sawa na mwajiriwa mwenye mkataba na Mwajiri?

Wajuzi wa Sheria naombeni msaada wenu hapa
 


ushasema hana mkataba kwa hiyo ukiachakazi timua zako tuu. Na unafanyaje kazi bila mkataba? Kwanini wkt mkataba uko kwaajili ya kukulinda mfanyakazi na mwajiri , hasa mfanyakazi...

Kama unamkataba hapo ndipo najua kuna sheria zakufuata si kuachakazi kiholela holela..
 
j
jibu lako linatosha, naomba mjadala ufungwee
 
Kama huna mkataba usiache kazi hivihivi subiri uaminiwe kitu ndo usepe
 
Asante Sana mkuu maana wananipigia simu za vitisho eti kwann sikuwaambia mwezi mmoja kabla, wanatishia kuzuia mafao yangu ya nssf
 
Asante Sana mkuu maana wananipigia simu za vitisho eti kwann sikuwaambia mwezi mmoja kabla, wanatishia kuzuia mafao yangu ya nssf


Nenda ktk mamlaka zinazohusika na haki za binadamu/ ajira ueleze hayo yote...Hakuna aliye juu ya sheria...
Kwanza kukutumikisha zaidi ya miezi ikivuka 3 mfululizo bila mkataba ni kosa.
 
Nashangaa swali linalouliza "unafanyaje kazi bila mkataba" takribani asilimia 90 ya waajiri hawatoi mikataba wa maandishi kwa kuogopa kujifunga, ILA
kisheria kuna mikatataba ya aina 3
1. Mikataba ya maandishi (press)
2. mikataba ya maneno (words of mouth)
3. Contract by implication

Haiwezekani ukafanya kazi bila makubaliano yoyote, swala makubaliano yenu yako kwa mfumo upi?

Remember contract by press is more preferable.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…