Wanajanvi jana asubuhi nilikuwa nikifuatilia matangazo ya Channel 10, nikamuona bwana mkubwa wa nchi akiwapa pole wakiristu ambao makanisa yao yamechomwa moto na kuporwa, Moja ya vitu alivyosema ni kwamba kukojolea kitabu cha dini ni kosa. Ingawa nakubaliana naye kuwa kwa utamaduni tulioujenga wa kuheshimiana na kosa lakini nikajiuliza sheria inasemaje kuhusu hili au iko kimya? Ndo maana nikalitupa hapa janvini waliobobea katika sheria watupe ushauri.
Nawakilisha.
Nawakilisha.