Sheria inasemaje kuhusu kumpiga mtu picha bila ridhaa yake?

Rato

Member
Joined
Jul 10, 2012
Posts
92
Reaction score
7
Naomba kujua sheria zinasemaje kuhusu mambo mawili yafuatayo(1)Ikiwa mtu atakupiga picha bila ridhaa yako?(2)Ikiwa mtu atakutwa akifanya mapenzi kwenye gari lake.Naomba kuelekezwa vifungu vinavyomshitaki mtu atakayefanya makosa yaliyotajwa hapo juu na pia adhabu zake
 
Naona defamation can stand but uweze kuprove imekuathiri vip
 

...Kuhusu namba 2:
kama hivi hapo chini;












1 Corinthians 7 Swahili NT 1Yahusu sasa mambo yale mliyoandika: naam, ni vizuri kama mtu haoi; 2lakini kwa sababu ya hatari ya uzinzi, basi, kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe. 3Mume atimize wajibu alio nao kwa mkewe, naye mke atimize wajibu alio nao kwa mumewe. 4Mke hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mumewe anayo; hali kadhalika naye mume, hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mkewe anayo. 5Msinyimane haki zenu, isipokuwa kama mnaafikiana kufanya hivyo kwa kitambo tu, ili mpate nafasi nzuri ya kusali. Kisha rudianeni tena mara, ili Shetani asije akawajaribu kwa sababu ya udhaifu wenu. 6Ninayowaambieni sasa ni mawaidha, si amri. 7Ningependa watu wote wawe kama mimi nilivyo; lakini kila mmoja anacho kipaji chake kutoka kwa Mungu; mmoja kipaji hiki na mwingine kile.
8Basi, wale ambao hawajaoana na wale walio wajane nawaambia kwamba ni vema kuendelea kuwa kama mimi nilivyo. 9Hata hivyo, kama mtu hawezi kujizuia basi, na aoe; maana ni afadhali zaidi kuoa kuliko kuwaka tamaa.
10Kwa wale waliooa ninayo amri, tena si yangu, ila ni ya Bwana: mke asiachane na mumewe; 11lakini kama akiachana naye, basi abaki bila kuolewa; ama la, apatanishwe na mume wake. Mume naye asimpe talaka mkewe.
12Kwa wale wengine, (mimi binafsi,si Bwana) nasema hivi: Ikiwa mwanamume Mkristo anaye mke asiyeamini, na huyo mwanamke akakubali kuendelea kuishi naye, asimpe talaka. 13Na, kama mwanamke Mkristo anaye mume asiyeamini, na huyo mwanamume akakubali kuendelea kuishi naye, basi, asimpe talaka mumewe. 14Kwa maana huyo mume asiyeamini hupokelewa kwa Mungu kwa kuungana na mkewe; na huyo mke asiyeamini hupokelewa kwa Mungu kwa kuungana na mumewe. Vinginevyo watoto wao wangekuwasi wa Mungu; kumbe sasa ni watoto wake Mungu. 15Hata hivyo, ikiwa yule asiyeamini anataka kumwacha mwenzake aliye Mkristo, basi, na amwache tu. Hapo huyo Mkristo, mume au mke, atakuwa huru. Maana Mungu amewaiteni ninyi muishi kwa amani. 16Wewe mama Mkristo, unawezaje kuwa na hakika kwamba hutaweza kumwokoa mume wako? Au wewe mume Mkristo, unawezaje kuwa na hakika kwamba hutaweza kumwokoa mkeo?
 


Rebecca akitoka kwenye jengo alimokuwa akifanyia kazi huku akiwa kabeba boksi lenye vitu vyake baada ya kutimuliwa kazi.Mfanyabiashara wa Uingereza anayetuhumiwa kufanya ngono kwenye teksi huku akiwa amelewa chakari mjini Dubai, amefukuzwa kazi.
Rebecca Blake mwenye miaka 29 ametimuliwa baada ya kuamriwa na bosi wake aliyechukizwa na kashfa hiyo kupakia kila kilicho chake kutoka ofisi hizo za kampuni inajojihusisha na masuala ya ajira ya Manpower Professional.
Aliongea huku akibubujikwa machozi katika simu yake ya mkononi wakati akitoka makaomakuu ya kampuni hiyo akiwa amebeba ubavuni boksi lililokuwa na vitu vyake.
Rebecca anayetokea Croydon, kusini mwa London na fundi uchomeaji vyuma kutoka Ireland, Conor McRedmond walikamatwa mapema mwezi huu baada ya kutumia siku nzima kunywa pombe.
Wawili hao walishikiliwa kwa siku tano na kushitakiwa kwa kutembea nje ya ndoa na kunywa pombe hadharani ambapo yote hayo ni makosa yajinai katika mamlaka hiyo inayoongozwa kwa sheria kali za Kiislamu.
Rebecca, aliyeajiriwa kwa mudana Max Clifford, atakabiliwa na kifungo cha hadi miaka mitatu jela kama atapatikana na hatia. Alikana mashitaka yote.
Ofisi ya Clifford imethibitisha kwamba ametimuliwa kazi.
Rebecca, mshauri wa mambo yaajira, alikutana na McRedmond kwenye Hoteli ya Kijiji cha Ireland ambapo wateja hulipia Pauni za Kiingereza 10 kwa ajili ya promosheni ya kunywa uwezavyo siku nzima.
Baada ya kunywa kwa masaa 12, wawili hao walichukua teksikuelekea Dubai Marina.
Dakika baadaye walinaswa na dereva wa teksi kupitia vioo vya gari wakiwa katika hali ya kufanya mapenzi, kwa mujibu wa ripoti za polisi.
Kufuatia kukerwa na tabia hiyo,dereva huyo akasimamisha gari na kwenda kuwaripoti kwa polisi wa doria aliyekuwa kwenye gari lililoegeshwa jirani.
Aliporejea akiongozana na polisi, wakawaona Rebecca na McRedmond wakifanya ngono kwenye kiti cha nyuma cha teksi hiyo, imedaiwa.
Vyanzo vya habari zimesema: "Walikuwa wamelewa chakari, wakaanza kubusiana na kukumbatiana. Kisha wakaanza kufanya ngono.
"Polisia aliwafuata kwenye gari,alikuta mwanamke akiwa mtupu na walikuwa wakifanya ngono kwenye kiti cha nyuma."
Baada ya kukamatwa kwao, wawili hao walipelekwa kwenye kituo cha polisi cha jirani cha Jebel ali na kuwekwa rumande kutoka Mei 4 hadi Mei 9, mwaka huu.
Polisi waliwachukua kipimo chaDNA kama ushahidi kwamba walikuwa wakifanya ngono na kwamba walikuwa wamelewa.
Polisi wanangojea majibu ya kipimo hicho kutoka maabara ya mkemia mkuu kabla ya kuwafikisha wawili hao mahakamani.
 
Kwahiyo ni sawa na kufanya mapenzi hadharani, pia kwenye gari ni uchafu...

Pia hauna staha, Na huyo mwanamke hajiheshimu. Kwa lugha rahisi unafanya uzinzi hadharani...
 
Sijaona msaada wenu wa kisheria hapa just a - bla - bla - so how can we help that guy
 
sijaona vifungu hasa lakn nikitolea mfani hawa wanappiga picha kwenye harusi au mikutano kisha wanakuuzia, mm huwa nazichana tu, maana kuna rationale mbili hivi, kwanza hakukua na ridhaa yako, pili huwezi jua unapumuachia atakwenda kuzifanyia nn .....................your image is your property hence you can claim your property right to be respected, protected and fulfilled
 
kwa hiyo ina fall under Tortous liability kama ungependa kuipeleka hivyo na kama ataitumia kwa crime, the same......
 
Kumbe hakuna loyer humu nasikitika cjapata jibu nafikiri hapa ndio mwisho wa mawazo yetu
 
Rato kwenye sheria ya madhara "Law of Torts" kuna kitu tunakiita trespass kwa wenzetu mfano uk inaenda mbali sana mpka "intrusion of privacy" kama moja ya trespass. Kwa tz sina material case per se ila nina mfano mzur recently wa prince William na mke wake walipigwa picha bila ridhaa yao na gazet moja la ufaransa na wakachapisha hzo picha. Gazeti lilishtakiwa na kuamriwa kulipa fine ikiwa na ku issue apology kwa familia ya kifalme. Hizi material case unaweza zitumia hapa kuenforce claim yako. Intrusion of privacy ni kosa kisheria na lina treatment ya mahakama.
2. Kufanya mapenz kweny gar inategemea na location. Mfano kama gar lipo location ambayo kiraman ni public place hilo ni kosa cz kwa sheria za nchi yetu ni kosa kufanya mapenz hadharan au katika sehem za umma (public place) ndo mana unaona watu wakikamatwa maeneo km coco beach wakifanya mapenz.
Lakin km gar ipo ndani ya uzio wa nyumba yako na mnafanya mapenz na mtu wako haina makosa cz mpo within boundaries of your privacy.
 
Nashukuru nimepata mwanga kdg kuhusu mada hii hasa nikipitia post za Mossad007 na Amavubi thanx
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…