Kama mke wako hana ajira, nakusikitikia sana, pole yako. Mzigo wa matunzo yote ya watoto yatakua juu ya mabega yako kila mwezi (Matumizi, Ada, Bima Ya Afya, Chakula N.K).
Ila kama mke ana ajira, ondoa shaka maana nusu kwa nusu mtachangia juu ya matumizi ya watoto. Ila atakae ishi na watoto atapunguziwa mzigo kidogo ya mchango.
Na kama mkeo hana ajira na ana watu wanaomshawishi au ana nia ya kukuburuza polisi (Deski la jinsia na watoto) au mahakamani kudai matunzo ya watoto, nakushauri wahi mapema kumfungulia hata genge la kuuza nyanya au kabeji au bamia au vitumbua. Hii itakuweka salama kwenye kujitetea huko mbeleni mwa safari (Utanielewa na kunishukuru baadae sekeseke likianza).
Ahsanteni kwako pia. Mungu akubariki na zahama linaloku nyemelea.