Sheria inasemaje mfungwa anapofia jela?

Sheria inasemaje mfungwa anapofia jela?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Wafungwa nao ni binadamu kama sisi tuu. Wanaugua na wanaweza kupoteza maisha wakiwa kifungoni.. Je sheria inasemaje?

Zamani tuliambiwa mfungwa aliye kifungoni akipata madhila ya kupoteza maisha huzikwa na serikali kupitia magereza na ndugu zake huja kupewa taarifa baada ya kifungo kwisha.. Je hii ni kweli?
Na kama ni kweli je sheria ni haki? Sijawahi kushuhudia mazishi ya mfungwa anayetumikia kifungo.. Sitaki kuamini kwamba hawafi..!

Wanasheria tunaomba ufafanuzi kwenye hili..
Natangulisha shukrani🙏🏿🙏🏿🙏🏿
 
Labda wanaogopa itakuwa escape plan,ndo mana wanaamua kuzika wenyewe.
Ama bado Yuko chini ya magereza sio huru.ndio maana wanaratibu Kila kitu chini Yao.au labda ndugu hawapatikani,mawasiliano hayafikiki tena.ukute ana miaka kumi hakuna anaemtembelea
 
atapelekwa mortuary ndugu watapewa taarifa wasipofika within 14 days anazikwa na magereza. Wengi wakiumwa wanawahishwa hospital ni kosa kubwa sana mfungwa kufia jela wengi wanafia hospital, kuhusu gharama magereza watalipa kila kitu kupitia kwa afisa ustawi wa jamii wa hosp husika
 
Akifariki tu ndugu hupewa taarifa kwenda kuuchukua mwili. Wasipoenda anazikwa na magereza.
hiyo ndugu kupewa mwili ni kwa mahabusu tu lakini kwa mfungwa hampewi mwili ila ndugu wawili wa mfungwa watakuwepo kushuhudia mwili wake na kuhudhuria mazishi kama ushahidi pia kuwakilisha familia..lakini kisheria anazikwa na magereza wakitumia wafungwa ambao ni waislam au wakristo kwani masheikh na walokole wapo wengi magerezani watazika chini ya usimamizi wa askari
 
atapelekwa mortuary ndugu watapewa taarifa wasipofika within 14 days anazikwa na magereza. Wengi wakiumwa wanawahishwa hospital ni kosa kubwa sana mfungwa kufia jela wengi wanafia hospital, kuhusu gharama magereza watalipa kila kitu kupitia kwa afisa ustawi wa jamii wa hosp husika
Kama akifia gerezani hawawezi kughushi kwamba kafia hospital?
 
Hali hiyo inawakuta sana Wafungwa waliofungwa vifungo vya muda mrefu maana huwa hawakai gereza moja, Mara kwa mara huwa wanahamishwa unaweza kufungwa Mwanza ila ukahamishwa magereza hata 10, kutokana na hali hiyo ndugu huwa wanachoka hawawendi tena magerezani kufatilia ndugu zao maana kila wanapoenda wanaambiwa alishahamishwa.

Hali hiyo huenda na mwisho mawasiliano huwa yanakata baadae anapoteza maisha na huko ndo anazikwa na serekali bila ndugu zake kufahamishwa kutokana na kutokua na mawasiliano, siku mkifatilia ndo mtapewa taarifa kuwa alishafariki
 
hiyo ndugu kupewa mwili ni kwa mahabusu tu lakini kwa mfungwa hampewi mwili ila ndugu wawili wa mfungwa watakuwepo kushuhudia mwili wake na kuhudhuria mazishi kama ushahidi pia kuwakilisha familia..lakini kisheria anazikwa na magereza wakitumia wafungwa ambao ni waislam au wakristo kwani masheikh na walokole wapo wengi magerezani watazika chini ya usimamizi wa askari
Kifungo kikiisha hawawezi kukabidhiwa mwili wakauzike tena?
 
Hali hiyo inawakuta sana Wafungwa waliofungwa vifungo vya muda mrefu huwa hawakai gereza moja, Mara kwa mara huwa wanahamishwa unaweza kufungwa Mwanza ila ukahamishwa magereza hata 10, kutokana na hali hiyo ndugu huwa wanachoka hawawendi tena magerezani kufatilia ndugu zao maana kila wanapoenda wanaambiwa alishahamishwa.

Hali hiyo huenda na mwisho mawasiliano huwa yanakata baadae anapoteza maisha na huko ndo anazikwa na serekali bila ndugu zake kufahamishwa kutokana na kutokua na mawasiliano, siku mkifatilia ndo mtapewa taarifa kuwa alishafariki
siku mkifatilia ndo mtapewa taarifa kuwa alishafariki🥺🥺🥺😪
 
hiyo ndugu kupewa mwili ni kwa mahabusu tu lakini kwa mfungwa hampewi mwili ila ndugu wawili wa mfungwa watakuwepo kushuhudia mwili wake na kuhudhuria mazishi kama ushahidi pia kuwakilisha familia..lakini kisheria anazikwa na magereza wakitumia wafungwa ambao ni waislam au wakristo kwani masheikh na walokole wapo wengi magerezani watazika chini ya usimamizi wa askari
Hata kama kafungwa wiki 2?
 
Hali hiyo inawakuta sana Wafungwa waliofungwa vifungo vya muda mrefu maana huwa hawakai gereza moja, Mara kwa mara huwa wanahamishwa unaweza kufungwa Mwanza ila ukahamishwa magereza hata 10, kutokana na hali hiyo ndugu huwa wanachoka hawawendi tena magerezani kufatilia ndugu zao maana kila wanapoenda wanaambiwa alishahamishwa.

Hali hiyo huenda na mwisho mawasiliano huwa yanakata baadae anapoteza maisha na huko ndo anazikwa na serekali bila ndugu zake kufahamishwa kutokana na kutokua na mawasiliano, siku mkifatilia ndo mtapewa taarifa kuwa alishafariki
Aisee.. hata kama ni sheria lakini sio haki wala vizuri.
 
atapelekwa mortuary ndugu watapewa taarifa wasipofika within 14 days anazikwa na magereza. Wengi wakiumwa wanawahishwa hospital ni kosa kubwa sana mfungwa kufia jela wengi wanafia hospital, kuhusu gharama magereza watalipa kila kitu kupitia kwa afisa ustawi wa jamii wa hosp husika
Huku mtaani sijawahi kuona msiba halafu tukaambiwa marehemu alikuwa mfungwa!!
 
Back
Top Bottom