Sheria inasemaje Tanesco Inaposema haina meter za luku wakati mteja kaharibikiwa na LUKU

Sheria inasemaje Tanesco Inaposema haina meter za luku wakati mteja kaharibikiwa na LUKU

babayah67

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2008
Posts
493
Reaction score
79
Ndugu wanasheria, naomba kueleweshwa sheria inasemaje katika tatizo langu na Tanesco.
Mimi ni mteja wa Tanesco kwa muda mrefu, na meter ninayotumia ni ya LUKU. Sasa ni Alhamisi iliyopita meter yangu ilikata umeme, yaani umeme ukawa hauingii ndani ya nyumba, wakati unit zinasomeka kwenye meter. Nilienda reporti tatizo hilo Tanesco na jibu walilonipatia ni kuwa meter hiyo imeharibika na hivyo inatakiwa ibadirishwe. Nilipouliza lini watakuja badilisha, walinijibu kuwa kwa sasa hawana akiba ya meter, hadi hapo zitakapokuja ndio nitapatiwa.

Toka hiyo Alhamisi leo ni siku ya sita sina umeme. SWALI ni Je sheria inasemaje Tanesco inaposhindwa nipatia meter wakati ni jukumu lao la msingi??? Je naweza washitaki ????

NB: Naomba Tanesco au Serikali wajaribu kutoa ukiritimba katika suala hili la LUKU, wajaribu kuruhusu watu binafsi waingize Luku madukani watuuzie kama TRA walivyofanya kwenye EFD.
 
Back
Top Bottom