Sheria kuhusu kumshika mke wa mtu maungo yake hadharani

mahirtwahir

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Posts
613
Reaction score
313
Naomba waungwana muhusike na kichwa cha habari kisha mutowe maoni na msaada wa kisheri.

**** mke wa mtu ni muajiriwa wa muda katika taasisi ya Serekali na nafasi yake ni meneja mauzo ( muuza duka la serekali) mnamo mwezi wa 7 / 2016 alishushwa bosi wake alimuita na kumuagiza kua aingie ndani ya gari kwa safari ya kikazi dereva wa boss huyo aligoma kuendesha gari baada ya kuingia msichana huyo na kuanza kumtukana hafi kifikia kumuambia kua ni paka na kwa vile ana mimba alimuambia kua ananuka ujusi kama wa mbwa maneno yote hayo aliokua akiyukana msichana alibakia kulia na boss wake hakuweza kumkemea dereva wake kwa hilo zaidi ya kumuambia endesha gari kwa masikitiko safar ilikwendwa.

Jana yarehe 5/10/2018 alikuja yule dereva na kuingia ndani ya ofisi ya huyo binti na kusalimia "Asalamu alaikum Bikombo ndio nani hapa" akimaanisha yule mgovi wake aliuliza kwa kumjejea maaana alikua anamjua vizuri na kumuambia kua "nimeambiwa nije nikuombe razi kwa yaliotokea nyuma" bila ya kujibiwa chochote alizungunga nyuma ya yule binti na kumkumbalia kwa nyuma huku mikononyake akiwa ameishika vizuri matiti yake binti kurusha mikono jamaa alikua ameshabonyeza maziwa zamani " na waliokuwemo humu dukaninndio mashahidi" alisema yule kijana na kuondoka.

Bint alilia sana na kuomba ushauri kwangu hatua ya mwanzo nilimshauri aandike barua na kumuadisia muajiri wake ambaye ndio anaendeshwa na huyo kijana.

Naomba ushauri na muelekezo wa sheria kwa kosa kama hilo katika utumishi na makosa ya jinai na jeee kunpeleka mahakamani ni vipi na sheria ya wanawake ama utumishi inasemaje na naweza kupatiwa kipengele kinachoonesha adhabu yake jeee mahamani naeza kulipwa fidia
 
Mkuu uzi wako haujaupangilia vizuri kwa maelezo, na kuuelewa ni mtihani. Ila alipaswa kufanya haya,
1) Kutoa report police kwa alichofanyiwa na huyo jamaa.

2) Police kuanzisha file/case na kuanza upelelezi wa hayo makosa.

3) Police wangemfungulia mashtaka (chini ya Sheria Ya Makosa Ya Jinai, CAP 16) haya;
a) Kosa la jinai chini ya Kifungu namba 123- Kudharau sheria za wajibu (Disobedience of Statutory Duty).
b) Kosa la jinai chini ya Kifungu namba 135 - Kumshambulia kinyume na maadili na kumtusi mwanamke (Indicent assault and indicently insultulting women).
c) Kosa la jinai chini ya Kifungu namba 233 - Uzembe na matendo ya makusudi (Reckless and negligence acts).
d) Udhalilishija (Defamation) hapa anaweza kudai fidia ya kudhalilishwa kimwili na kisaikolojia, mbele ya hadhara kwa matendo ya huyo jamaa.
 
Hayo ni makosa ya udhalilishaji wa kijinsia.. Jela fasta tu
 
nafurahi kujua uko vizuri kisheria
 
Huyo ni mtu na mpenzi wake, acha kudanganywa ndugu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…