Bunge limepitisha muswada unaoanzisha Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ambayo sasa sasa itakuwa na jukumu la kusimamia viwanja vyote vya ndege hata vile vidogo ‘airstrip’.
Muswada huo uliopitishwa na Bunge jana Agosti 28, 2024 ukisubiri kutiwa saini na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa sheria kamili, pia unataka marekebisho ya sheria, ili TAA iwe na wafanyakazi wake wa zimamoto.
Kwa sasa ilivyo TAA inamiliki vifaa vya zimamoto, lakini wafanyakazi wanatoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, hali inayosababisha ugumu katika masuala ya kinidhamu na kiutawala.
Soma Pia: Serikali yatangaza kuanza kuchunguza Mifumo Viwanja vya Ndege
Kabla ya muswada huo, TAA ilikuwa ikitekeleza majukumu yake kama wakala chini ya Sheria ya Wakala wa Serikali, Sura ya 245, na kusimamiwa na Bodi ya Ushauri ambayo ina mamlaka finyu.