Elections 2010 Sheria kumi za uchaguzi mkuu

Elections 2010 Sheria kumi za uchaguzi mkuu

mojoki

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
1,313
Reaction score
290
Jumapili, Octoba 31, tunapokwenda kupiga kura kuwachagua rais,wabunge na madiwani tufanye hivyo kwa kuzingatia sheria kuu kumi zifuatazo:

1.Tambua kwamba kura ni silaha takatifu inayokuwezesha kumchagua yule unayeamini kwamba unaweza kumkabidhi sehemu ya maisha yako na ukawa salama.Tumia busara

2.Jua kwamba ni usaliti kwako mwenyewe na kwa wananchi wengine iwapo utapiga kura kwa misingi ya rushwa.Anayekununua hakuthamini.Kwake wewe ni Bidhaa tu,kama maharage

3.Usiruhusu hisia za ubaguzi wa kabila,rangi,dini,jinsia,au ubaguzi wa aina yoyote nyingine ile utawale uamuzi wako katika kupiga kura

4.Tenda haki kwa wengine,na pia dai haki yako kutoka kwa wengine.Usimwonee yeyote na wala usimruhusu yeyote akuonee

5.Watetee na walinde wanyonge na wasiojiweza.Wasaidie ili waweze kutumia haki yao ya kupiga kura.

6.Imarisha uhuru wako na uhuru wa nchi yako kwa kuhakikisha kwamba uchaguzi unakuwa na maana,na kwamba kila kura inayopigwa ina maana.

7.Epuka vurugu,vitisho na ugomvi.Kura ni jambo la raha si karaha

8.Kumbuka kwamba amani ni mwana wa haki.Penye haki,aliyeshindwa akubali kushindwa,na aliyeshinda bado atende haki kwa aliyeshindwa

9.Tambua kwamba uchaguzi unakuja na kwisha,viongozi huja na kuondoka,lakini taifa na watu wake hudumu milele.Tuliza hamasa,epuka chuki na uwe na ustahimilivu

10.Hii ni fursa adhimu;ifurahie
 
Back
Top Bottom