Sheria mpya ya PSSSF Itaathiri watu ambao wameshafungua madai ya claims kwenye NSSF

Sheria mpya ya PSSSF Itaathiri watu ambao wameshafungua madai ya claims kwenye NSSF

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,154
Reaction score
4,184
Habari wana Jamvi;
Ningependa kuuliza swali,iwapo imetungwa sheria mpya ambayo ama inafanya jambo lilitokea au ambalo liko katika process ya kutokea kuwa ni kinyume cha sheria mfano:

Iko hivi,Iwapo kuna mtu ama amestaafu na yuko anafuatilia mafao yake NSSF ama ameachishwa kazi na yuko anasubiria malipo yake ya NSSF ama ameacha kazi na anadai mafao ya kujitoa NSSF ama amefiwa na mwenzi wake na yuko anafuatilia mafao yake NSSF.

Na Iwapo mtu huyu kabla ya kutoka katika ajira alikuwa ni mwajiriwa serikalini lakini alikuwa ni mwanachama wa NSSF au alikuwa mtumishi wa sekta binafsi na alikuwa mwanachama wa GEPF au PPF au PSPF.

Na Iwapo mtu huyu ameshawakilisha nyaraka zote za madai yake kwenye mfuko wake na kwamba anachosubiri na kupewa malipo tu.

Na Iwapo katika sheria hii mpya kuna ama marekebisho ambayo yamebadili kwango cha malipo anayostahili ama,fao analodai limeondolewa kabisa.

Swali je madai yake yatashughulikiwa kwa mujibu wa sheria ipi?

Wataalamu wa sheria tujuzane
 
I hope sheria hii itawahusu wale ambao hawakufungua madai wakati au kabla sheria hii kupitishwa
 
Natamani lipige bonge la tetemeko tufe nchi nzima!!!!!!
Naichukia hii nchi balaaa
 
Back
Top Bottom