Sheria mpya za Ligi kuu ya English (EPL) 2019/2020

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2018
Posts
24,314
Reaction score
38,919
Sheria mpya za Ligi kuu ya Uingereza 2019/2020.

HANDBALL.

Sheria ya zamani: Kushika mpira lazima iwe maksudi . Ili itafsiriwe maksudi vitu viwili lazima vizingatiwe, Movement ya mkono wa mchezaji kuelekea kwenye mpira na umbali kutoka kwa mchezaji aliyeshika na yule wa mwisho kupiga mpira.

Sheria Mpya : Kama mchezaji akishika mpira maksudi ataadhibiwa , lakini pia adhabu ndogo itatolewa kama mchezaji akitengeneza nafasi au kufunga goli kwa kushika mpira bahati mbaya . Lakini pia kama mkono utanyanyuliwa juu ya urefu wa bega basi pia itahesabiwa adhabu au mkono ukawa katika naafsi ambayo itafanya uwe mpana zaidi kuliko kawaida.

:Lakini kama mpira utagonga mkono wa mchezaji akiwa karibu kabisa na tukio wakati anaanguka chini na mkono upo karibu yake na mwili au alitumia mkono kumsaidia ku-control mwili wake wakati anaanguka hatoadhibiwa kama madhambi.

SUBSTITUTIONS;

Sheria ya mpya: Wachezaji wanatakiwa kutoka uwanjani katika eneo la karibu ambalo yupo kwa muda huo labda kama Mwamuzi atawaruhusu watoke eneo la katikati ya uwanja kwasababu za usalama au kama ameumia.

GOAL KICKS:

Sheria ya Zamani : Pindi ' Goal Kick ' inapopigwa wachezaji wote kutoka pande zote mbili kasoro yule mpigaji tu wanatakiwa kuwa nje ya eneo la 18 , na mchezo hauhesabiwi kama upo hai mpaka mpira utoke nje ya 18 .

Sheria Mpya : Mpira upo mchezo pindi tu utakapopigwa na kuanza kutembea . Kama kuna wachezaji / mchezaji wa timu pinzani kama bado yupo ndani ya 18 anaruhusiwa kuucheza .

YELLOW na RED CARDS .

Sheria ya Zamani : Mchezo hautakiwi kuanza tena mpaka pale Mwamuzi atakapomaliza kutoka kadi ya Njano au Nyekundu kama ameamua kutoa.

Sheria Mpya : Kama timu inayoshambulia imeamua na kupenda kuanzisha mpira wa faulo haraka ( Quick FreeKick ) na Mwamuzi bado hajatoa kadi yoyote ili mradi hiyo faulo ya haraka itengeneza nafasi ya kwenda kufunga . Basi mwamuzi atatoa ile kadi pindi mpira utakapotoka mchezoni .

Hata hivyo kama Mwamuzi alikuwa anataka kumtoa nje kwa kadi nyekundu mchezaji ambaye alicheza rafu ya kuzuia nafasi ya kufunga , watapewa kadi ya Njano kama timu iliyokuwa inashambulia ikaanzisha faulo ya haraka ( Quick Free Kick ) .

KWANINI: Watunga sheria IFAB wamesema kwamba haitokuwa haki pindi shambulizi limepotea , halafu utoe kadi ya njano au nyekundu wakati wale waliopotelewa na shambulizi waliamua kuanzisha faulo ya haraka haraka . Haki ni kwamba wachague kimoja Mwamuzi atoe kadi halafu ndio waanzishe mpira au waendelee na faulo ya haraka lakini badala ya kadi nyekundu atatoa ya njano.

SHERIA ZINGINE .

- Timu ambayo shilingi ikirushwa juu na wao wawe upande wa ushindi wa shilingi hiyo kwenye kuanza mpira , wana nafasi ya kuchagua kuanza wao mpira au mpinzani aanze.

- Wachezaji wote wa timu pinzani wanatakiwa kuwa angalau mita mbili kutoka kwenye mstari pindi mpira unaporushwa.

- Kushangalia kwa kuvunja sheria Mfano kuvua jezi bado utaadhabiwa hata kama goli ulilofunga limekataliwa .

- Kama mpira ukimpiga mwamuzi na ukapelekea kubadili umiliki wa mpira kwa timu ambayo ilikuwa inamiliki mpira , au ikatangeneza nafasi au goli , basi mwamuzi atachukua mpira na kuushika na kuangusha chini ugombaniwe ( dropped balls )

Ulimwengu wa soka Tz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…