Sheria na fine za barabarani

dyuteromaikota

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2013
Posts
5,929
Reaction score
8,327
Habari wanajf,

Kwa wale wajuzi wa mambo ya sheria msaada wenu hapa.
Nikiwa barabarani mara kadhaa trafk akinikamata huwa nashangaa maana utakuta mi najijua labda nimefanya kosa moja, lkn trafk anakuhesabia makosa hata matatu!! Kwa uelewa wangu mdogo wa mambo nakuja kuona kwamba katika hayo makosa matatu ambayo trafki ananihesabia mengine yanakuwa ni matokeo(effect) ya kosa kuu. Lakini trafk anakuja anataka akuandikie makosa matatu wakati mimi najua nimefanya kosa moja.
Kwa mfano, unaweza pita taa nyekundu kwenye mataa. Kosa nnalolijua mimi hapo ni moja tu ambalo ni kutosimama wakati taa nyekundu inapowaka. Kutana na trafki sasa atakwambia umefanya makosa matatu! Moja hujasimama taa nyekundu wakati inawaka, mbili atakwambia umesababisha obstruction (yaani kumzuia ambaye aliwashiwa taa ya kijani), tatu atakuandikia kosa lingine la kutaka kusababisha ajari[emoji23][emoji23] hata hiyo ajari haijatokea.

Sasa naomba kueleweshwa kwa wataaramu wa sheria, hayo makosa ambayo trafki anakuwa anayasema kwa kutumia mfano huo hapo juu ni sahihi!? Je hawa ndugu zetu trafki wanapelekwa hata semina ili kuzijua hizi sheria!?

Ahsanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…