Sheria na kanuni za nchi zinaruhusu kutumia Jeshi kudhibiti ghasia za wananchi?

Sheria na kanuni za nchi zinaruhusu kutumia Jeshi kudhibiti ghasia za wananchi?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Hivi kwa mujibu wa katiba,kanuni na sheria za nchi ni sahihi kwa serikali kutumia jeshi la wananchi kudhibiti fujo au ghasia za wananchi?

Kama sheria na taratibu za nchi kweli zinaruhusu,kulikuwa na ulazima wa kutumia jeshi au nia na madhumuni ni kutisha raia?

Watawala mnapaswa kutambua kuwa hakuna mahali popote duniani nguvu za dola ziliwahi kushinda nguvu ya umma.
 
Nijuavyo mimi kazi ya Jeshi letu tiifu ni kulinda mipaka ya Tanzania, suala la vurugu na fujo za ndani ni kazi ya Jeshi la Polisi, hata hivyo inawezekana mkuu wa mkoa hakuwa na imani na hawa wazee wa magunia 18 ya ''majani ya kijamaica'' kama wangeweza kutuliza hii ghasia, mwenye uelewa zaidi katika hili atujuze tafadhali wakuu.
 
Back
Top Bottom