Tetesi: Sheria na kanuni za Utumishi nchini ni kandamizi. Hii ndio sababu kuu ya wafanyakazi kuendelea kulia. Na watalia kila mwaka endapo......

Tetesi: Sheria na kanuni za Utumishi nchini ni kandamizi. Hii ndio sababu kuu ya wafanyakazi kuendelea kulia. Na watalia kila mwaka endapo......

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Posts
5,056
Reaction score
10,721
Mengi yamesemwa kuhusu vilio vya wafanyakazi lakini naamini vilio hivi havitakaa yaishe.

Tatizo kubwa according to My views, ni SHERIA na TARATIBU mbovu zisizo na haki zinazosimamia utumishi wa umma Nchini.

Embu fikiria eti watu hawa wafuatao ndio Mtumishi anayelipwa kati Tshs 135,000/= kuendelea, anatarajia wamkomboe kwa utashi wao:-
1) RAISI:-
Huyu anakula mshahara wa Tshs 9,500,000/= kwa mwezi. Ukiweka na marupurupu anakwenda hadi Tshs 40,000,000/= kwa mwezi. Yaani kila siku analipwa zaidi ya milioni moja ya mshahara na posho
Hanunui chakula chake wala cha familia, hanunui nguo. Hajitibu kwa pesa yake wala familia yake, na Mke analipwa mamilion vilevile n,k na bado anaweza ku diverte pesa yoyote akaitumia anavyotaka

Yaani mapato ya raisi kwa mwezi yanaweza kulipa mafao ya mwalimu wa shule ya Msingi aliyetumikia kazi kwa miaka 40.

2) WAZIRI:-

Huyu anakula mshahara na posho za ubunge takribani Tshs 12,000,000/= kwa mwezi. Ukiweka na za Uwaziri anakwenda takriban Tshs 20,000,000 /= kwa mwezi. Bado ana matibabu ya bure hadi India!!!!

3) MBUNGE:-

Huyu afanye kazi asifanye, ahudhurie vikao au asihudhurie, ana malipo ya jumla ya zaidi ya Tsh 12,000,000/= kwa mwezi. Ana bima ya matibabu ya kutibiwa hadi India na mwenza wake.

Hapa sijazungumzia Makatibu wakuu na wakurugenzi Wizarani, Wakuu wa Ulinzi na Majeshg, Spika na Naibu Spika.

The baseline is, kama hatuta pigania katiba mpya ikaweka utaratibu kwa mambo mbalimbali ikiwepo utumishi wa Umma nchi hii, Tutaendeiea kulia kila Mei Mosi.
 
naomba kuuliza tuu hivi katika hali ya kawaida mbunge au waziri anaweza kumzidi rais mshahara???
 
Back
Top Bottom