Mndundu
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 233
- 34
Wakuu ninaomba kupewa maelezo kuhusu sheria na taratibu zinazo simamia suala la kujenga nyumba mbili katika kiwanja kimoja. Kwamfano mtu mwenye kiwanja cha mita 30 (30m) kwa mita 50 (50m), je ni sheria au taratibu gani zinatakiwa kufuatwa ili kuweza kujenga nyumba mbili au tatu katika kiwanja hicho? Siulizii kuhusu kujenga servant quarter bali nyumba mbili za kuishi familia mbili tofauti katika kiwanja kimoja. Kuhusu kutosha ka nyumba hizo tuchukulie kila nyumba ina upana wa mita 9 na urefu wa mita 13.