Sheria na taratibu za kupata umiliki na kuanzisha "enterprises company"

Nguvu Yetu

New Member
Joined
Sep 13, 2017
Posts
4
Reaction score
1
Habari wana-Jf.
Kulingana na namna ya kumiliki shughuli au jambo fulani nchini mwetu, yatupasa kuzifahamu sheria na taratibu katika jambo husika. Pia kutokuzifahamu taratibu hizo na sheria ni kosa kisheria.

Nimeingia mtandaoni mara nyingi nikizitafuta taratibu na sheria za "ENTERPRISES COMPANY" ili niweze kuzifahamu kulingana na wazo nililo nalo ili kupunguza msukosuko wa kutokuijua sheria nimezikosa. Hapa nina maanisha sheria na taratibu za nchini mwetu JAMHURI Tanzania bara na visiwani

Naomba mwana-Jf anaefahamu kuhusu taratibu na sheria za "enterprises company" anisaidie.

Asante sana.

[HASHTAG]#MAENDELEO[/HASHTAG] NI WATU.
 
Hakuna kitu kama enterprise company kisheria.

Enterprise ipo kwenye jina tu waliloamua kutumia wamiliki kampuni zenyewe ni LTD/Limited kisheria.
 
An enterprise kama alivyosema mdau Kang hapo juu ni jina au sehemu ya jina la biashara lakini hakuna aina ya kampuni inayosimama kama enterprise. Kampuni inakuwa na ukomo yaani limited. Kwa ufafanuzi mzuri kutoka katika kamusi ya oxford soma hapa chini[emoji116][emoji116][emoji116]
What is the difference between a company and an enterprise? The cambridge dictionary defines an enterprise as 'a business', and gives an example, 'a commercial enterprise', Oxford defines it, among other things as 'a business or company', and gives the example of a state-owned enterprise, the EU provides money for 'Small and medium-sized enterprises' (= businesses), yet we would not say: 'my father has set up an enterprise making chocolate bars' or 'the enterprise where I work employs 3 people'. If you look up 'enterprise' on google images, you get pages of space ships, a few aircraft carriers and a car rental firm, if you google image 'company', you get, well, companies.
 
Mkuu funguka zaidi.
Unaweza ukaita kampuni yako Julius Milla Enterprises LTD au Julius Milla LTD hizi hazina tofauti kisheria au katika ufunguzi wake, cha muhimu ni LTD/Limited maana yake hii kampuni ni entity yake yenyewe kisheria madeni yake ni yake na sio ya wamiliki etc.
 
Kuhusu Madeni Ya kampuni Utadaiwa kutokana na hisa zako mfano una hisa 100 umelipia 60 hapo kama kampuni ikifilisika na kushindwa kulipa madeni yake kwa creditors lazima wewe mwenye hisa ulipie hizo 40 kama liability.
 
ENTERPRISES ni Jina tu likiwa na maana ya shughuli za biashara Sio Aina Ya kampuni, kwa sheria ya Kampuni namba 22 ya mwaka 2002. Tanzania kuna aina mbalimbali za kampuni e.g kutokana na umiliki(ownership). Kwenye aina hii kuna aina mbili ambazo ni kampuni binafsi(Private ) na kampuni ya umma (Public). Kampuni binafsi (private company) haiwezi kuuza hisa kwa umma na idadi ya wanahisa haitakiwi kuzidi watu hamsini.

Kampuni ya umma (public company) wanahisa wake hawana ukomo kwa idadi na yanauwezo wa kuuza hisa kwa umma au mtu yoyote kw uhuru pia wanaruhusiwa kuuza hisa zao kwenye soko la hisa la Dar es Salaam, hii haina maana kuwa ni kampuni ya serikali. Aina kutokana ukomo wa madai (liability) kuna ukomo wa hisa na ukomo wa dhamana.


Kampuni yenye ukomo wa hisa (Limited by shares) ni kampuni ambayo katiba yake imeeleza kuwa wanahisa wake watalazimika kuchangia hisa ili kampuni iendelee na kuzilipia, endapo kampuni itakuwa imeelemewa na madeni watatakiwa kuchangia kiasi kile cha fedha ambacho hawajakilipia kwenye hisa zao kwa mujibu wa idadi ya hisa walizochukua.


Kampuni yenye ukomo kwa dhamana (Limited by guarantee) hizi ni kampuni ambazo yanaendeshwa na kusajiliwa kama taasisi zisizokuwa za serikali (NGO) na kampuni inakuwa haina hisa ila ni dhamana tu kwa wamiliki wake, pale wamiliki wake watatakiwa kuchangia kile kiasi walichoweka kama dhamana ni kampuni inapoelemewa na madeni. Aina hii ya kampuni inakuwa haina hisa ila inategemea misaada na ufadhili kutoka kwa watu mbalimbali.


Kampuni isiyo na ukomo (unlimited company) Hii ni aina ya kampuni ambayo wanahisa wake hawana ukomo wa madai endapo kampuni itakuwa imekumbwa na madeni.
 
Kuhusu Madeni Ya kampuni Utadaiwa kutokana na hisa zako mfano una hisa 100 umelipia 60 hapo kama kampuni ikifilisika na kushindwa kulipa madeni yake kwa creditors lazima wewe mwenye hisa ulipie hizo 40 kama liability.
Sio kweli, hauwezi kudaiwa madeni ya kampuni LTD unless ulijiweka mwenyewe (co-sign) wakati wa kuomba huo mkopo. Au kama ulikuwa unachanganya ghrama za kampuni na zako binafsi kwa kiasi kikubwa.
 
Sio kweli, hauwezi kudaiwa madeni ya kampuni LTD unless ulijiweka mwenyewe (co-sign) wakati wa kuomba huo mkopo. Au kama ulikuwa unachanganya ghrama za kampuni na zako binafsi kwa kiasi kikubwa.
Maana ya limited (LTD) ni kwa mwenye hisa unakuwa limited by share au guarantee ina maana kama umelipia hisa zako zote kwenye kampuni hauwez kudaiwa chochote hicho unachosema katika sheria inafahamika kama lift of corporate veil na mara nyingi ni kwa wale viongozi kama directors lakin kampuni nyingi zinakuwa na uncalled/unpaid share hasa hizi za LTD
 

Huu ndiyo ukweli. Well explained. Kuwa ikiwa kampuni ina face winding up..liability ya shareholder inakuwa limited only to the amount of unpaid shares katika jumla ya hisa alizonazo mwanahisa. Kama alikuwa na hisa 30 lakini when the shares were called alilipa 20 basi katika winding up atalipa 10 iliyobakia tu.
 
SHIKAMOO MKUU,NI KILZA TU NDIYE ATASHINDWA KUKUELEWA! UMEMALIZA
 
Kweli kabisa. Mimi bado nazidi kuwapa credits wana-jf kwa kufumbua macho yale ya fikra. Nimeyapata mengi nitayafanyia kazi. ninauzi mưingine nitauleta mbele yenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…