SoC01 Sheria Uzembe na Uzururaji inabagua walala hoi na wenye kiu ya maendeleo. Ipo kinyume na Katiba ya nchi

SoC01 Sheria Uzembe na Uzururaji inabagua walala hoi na wenye kiu ya maendeleo. Ipo kinyume na Katiba ya nchi

Stories of Change - 2021 Competition

my nation

Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
71
Reaction score
96
MTOA MADA:-

##JURUDYIZA##

Sheria hii kwetu Tanzania kama ilivyo kwa nchi baadhi za Afrika ililetwa na meli kutoka ulaya hasa kipindi cha muingereza miaka ya 1930 kabla hatujapata uhuru wetu, lengo kubwa lilikuwa ni kuwanyima watu weusi uhuru wa kutembelea maeneo yaliyokuwa yanakaliwa na watu weupe(wazungu) hata hivyo walilenga sana kuwabana waafrika kutoroka kutoka kwenye miradi yao ya mashamba waliyokuwa wameanzisha katika maeneo mbalimbali hapa Afrika ikiwemo Tanzania, sehemu zilizokuwa na ubaguzi na mateso ya kila aina. Kwa mwafrika aliyeweza kukimbia kutoka kwenye miradi hiyo ya mashamba alikuwa ni shujaa mkubwa ila akikamatwa hapo alifungwa na kuteswa kama mzembe na mzururaji.

Cha kushangaza ni kwamba baada ya kupata uhuru tuliendeleza sheria hii iliyo kinyume na haki za binadamu kupitia kifungu namba 177 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyorejewa upya mwaka 2019 na kuwa sehemu ya sheria zetu na kusahau ya kwamba kupitia Katiba yetu ya mwaka 1977 ibala ya 17 imeweka wazi kwamba ni haki ya kila mtanzania kutembea atakako, kuishi atakako, wala hapangiwi muda wa kuingia na kutoka ndani ya nchi yake, kwa ufupi ni kwamba mtu hapaswi kupangiwa muda wa kulala au kupangiwa muda wa kufanya jambo fulani na kumnyima mtu uhuru wa kutembea ni kukiuka katiba yetu.

Sasa tujiulize mzembe na mzururaji wa Uingereza ndio huyu huyu wa kwetu Tanzania?

Kule uingereza sheria hii ililenga sana

kuzuia Ombaomba mitaani lakini hapa kwetu tanzania sheria hiyo imelenga watu wafuatao:-

(a) mtu aliyepatikana na makosa kwa mujibu wa fungu la 176 baada ya kuwa alipata kuonekana na makosa zamani ya kuwa mzembe na mzururaji;

(b) mtu anayetangatanga kwa ukusanyaji sadaka au kujaribu kupata mchango au msaada wa namna yoyote kwa njia ya kujisingizia au hadaa;

(c) mtu aliyetuhumiwa au mwizi mashuhuri ambaye hana njia zinazoonekana bayana za kupata maisha na hawezi kujieleza sawa sawa;

(d) mtu anakayeonekana ndani au kwenye au karibu na nyumba yoyote au katika njia au barabara yoyote au mahali popote karibu na njia au barabara, au katika mahali popote pa hadhara katika wakati na hali ambayo yapelekea kana kwamba mtu huyo yupo hapo kwa jambo lisilo halali au la kikorofi;

(e) mtu ambaye bila ya ruhusa ya maandishi ya Mkuu wa Wilaya au ikiwa ni manispali au mji, afisa mkuu wa polisi wa manispaa hiyo au mji huo, atakusanya au kuomba michango ya fedha ya jambo lolote katika mahali popote pa hadhara ndani ya wilaya hiyo, manispaa au mji huo atahesabiwa kuwa ni muhuni na atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha miezi mitatu jela, na kwa kila kosa litakalofuata kifungo cha mwaka mmoja jela.

Tukumbuke tu ya kwamba Dunia imebadilika sana, kwa sasa watu wanafanya kazi usiku na mchana na pia watu wanatafuta mageuzi ya kiuchumi na kisiasa. Lakini inavunja moyo kwa mtu anayehangaika usiku na mchana katika kupambania maendeleo yake binafsi na nchi kwa ujumla anakamatwa eti tu ni mzembe na mzururaji na hii ni kwa sababu sijawahi ona mtu mwenye mali na wadhifa mkubwa akisumbuliwa kwa makosa haya,

Wanaosumbuliwa ni ni walalahoi na maskini ambao wanahangaikia familia zao kesho wale nini. Na zaidi wanaosimamia utekelezaji wa sheria hii mara nyingi hushughulikia wahanga ambao zaidi ni wauza baa, na wanywaji wa pombe na vijana wanaoonekana kuwa wachafuwachafu, wenye nywele zilizosokotwa na wakati mwingine mwonekano wao tu ndio huwaponza.

Kwa bahati mbaya zaidi nchi ya uingereza iliyoileta sheria hiyo kwao wameshaifuta haitumiki tena pamoja na nchi nyingine kubwa duniani kama vile Urusi, Ujerumani, Uholanzi, Marekani, Ubeligiji na nyinginezo ila kwetu bado inatumika.

Hata hivyo mashauri ya uzembe na uzurulaji yamekuwa hayana mafanikio kwa kufunga watu kwani hata ikitokea wakafikishwa mahakamani huwa wanaachiwa huru rejea kesi ya JUMA BAKARI DHIDI YA JAMHURI YA MWAKA 1985 Hivyo kuna ulazima wa kuiangalia sheria hii upya ili kutengeneza mazingira rafiki kwa raia wa Tanzania. Kwani linapokuja suala la utekelezaji wa sheria hii wanaoathirika ni baadhi ya watu tu lakini pia kuendelea kuitumia ni kuzidi kuimarisha na kuendeleza ukoloni mamboleo.

Ushauri wangu ni kwamba sheria hiyo imepitwa na wakati inapaswa kuondolewa kwani uwepo wake ni kukiuka katiba yetu badala yake serikali iboreshe mazingira yaafya na elimu kwa watoto, kutengeneza uchumi jumuishi kwa watanzania wote na kuwezesha ajira kwa vijana ili kuondokana na dhana hii ya wazembe na wazururaji.

##SISI NI WATANZANIA TUFANYE KAZI KWA BIDII NA TUPAMBANE ILI KUONDOA VIKWAZO/VIZUIZI VYA MAGEUZI YA KIUCHUMI NA KISIASA ##

ASANTENI SANA.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom