Sheria Ya Ajira

Sheria Ya Ajira

Mwinjilist mtume nabii

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2015
Posts
2,437
Reaction score
1,097
Jamani Naomba Ufafanuzi, Kwa Wanaojua Sheria Ya Ajira Kifungu Cha 20(4) Kinachohusu "Saa Za Usiku" Namna Inavyotakiwa Kulipwa?
 
Jamani Naomba Ufafanuzi, Kwa Wanaojua Sheria Ya Ajira Kifungu Cha 20(4) Kinachohusu "Saa Za Usiku" Namna Inavyotakiwa Kulipwa?
saa za usiku kwa maana ya shift kwamba mchana hufanyi kazi lakini unafanya usiku au ni overtime. Kama ni shift basi unalipwa kama kawaida inakuwa tu umebadili masaa ya kufanya kazi badala ya kufanya mchana masaa manane unafanya usiku masaa manane (mfano).
 
Ufafanuzi wa malipo ya ziada unapofanya kazi saa za usiku upo hivi.
1. Kwanza saa zinazohesabika kuwa za usiku ni kuanzia saa 2 usiku hadi saa 12 asubuhi ya siku inayofuata.
2. Ukokotoaji wa malipo hayo ni kuwa utalipwa ziada ya asilimia 5 kwa kila saa utakayofanya usiku huo.
3. Mathalani malipo yako kwa saa 1 ni shilingi 1000, kwa maana hiyo kwa kila saa utakayofanya usiku huo, utalipwa ziada ya shilingi 50.
 
Back
Top Bottom