Ufafanuzi wa malipo ya ziada unapofanya kazi saa za usiku upo hivi.
1. Kwanza saa zinazohesabika kuwa za usiku ni kuanzia saa 2 usiku hadi saa 12 asubuhi ya siku inayofuata.
2. Ukokotoaji wa malipo hayo ni kuwa utalipwa ziada ya asilimia 5 kwa kila saa utakayofanya usiku huo.
3. Mathalani malipo yako kwa saa 1 ni shilingi 1000, kwa maana hiyo kwa kila saa utakayofanya usiku huo, utalipwa ziada ya shilingi 50.