Sheria ya ardhi /msaada

Sheria ya ardhi /msaada

mikononyuma

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2015
Posts
641
Reaction score
600
1. Ardhi katika nchi hii inamilikiwa na dola ao mwananchi?
2. Ardhi kuwa shamba, kiwanja cha makazi /biashara n.k hurasimishwa na mamlaka husika, je sisi tuliojenga,kuendesha kilimo n.k huku kijijini kwenye maeneo ya kurithi ambapo mamlaka inayorasmisha matumizi husika haijatufikia wala hatuijui, tunatumia ardhi ya nani?
3. Umiliki wa ardhi iliyorasimishwa matumizi yake na mamlaka husika /kupata hati ni kujihakikishia umiliki wa milele na maana kizazi adi kizazi, na kama ni ivyo sisi wa huku kijijini tumekuwa tunarithi kisichokuwa chetu kwani mamlaka akifanikiwa kufika atarasimisha na kutupokonya sisi vilembwe wa mmiliki aliyerithisha kizazi kwa kizazi adi nasi wa miliki wa sasa kuwa katika mnyororo huo ?
 
1. Ardhi inamilikiwa na dola kwa maana ya Rais ameaminiwa kwa kupewa mamlaka ya kusimamia ardhi. kwa hiyo ndiyo maana hakuna mtu anamiliki ardhi, bali anakuwa mpangaji tu kwa kipindi fulani kilichoainishwa.
2. Maeneo ya vijijini ardhi humilikiwa na halmashauri ya kijiji (village council) chini ya sheria ya Ardhi vijijini sura ya 114 (Vilage Land Act) na inatoa hati za kimili (customary rights).
3. Kwanza kulingana na sheria za ardhi Tz, huwezi kupata umiliki wa ardhi wa milele (fee simple) maana hii (land tenure) imeshafutwa (abolished) kwa Tz, lakini bado unaweza kuirithisha maana ni free hold but not certain.

hapa mmiliki ni kijiji, na ndiyo maana serikali inaweza kukuhamisha lakini kwa kukufidia, ardhi za kijiji zimetengwa na za mijini kwa sababu maalumu ya kulinda jamii husika inayoishi hapo.
 
Back
Top Bottom