Sheria ya dhana ya kifo. (death in abscentia)!

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Posts
5,056
Reaction score
10,721
Kisheria, Mahakama kuu inaweza kumtangaza mtu aliyepotea kwa muda mrefu bila kujulikana alipo na jitihada za kumpata kushindikana, kuwa amekufa.
Hii inaitwa dhana ya kifo au DEATH IN ABSENTIA.

Sheria za Tanzania haziko wazi sana, (I STAND TO BE CORRECTED), kuhusu ni muda gani ukipita bila mtu kujulikana alipo, Mahakama kuu, inaweza kuombwa kutoa tangazo (declaration) la kifo chake. Hata hivyo nchi nyingi za Jumuiya ya Madola ambazo mifumo yetu ya kisheria inalandana zikiongozwa na Uingereza, na USA, zanakubaliana kuwa kipindi cha miaka saba (07) ni muafaka kabisa kupeleka ombi la Tangazo Mahakama kuu.
(Kwa China ni miaka 2).

Kwa ujumla muombaji (applicant), atapaswa kuithibitishia mahakama kwa "BALANCE OF PROBABILITY", mambo yafuatayo:-

- Mhusika kutooneka nyumbani au eneo lolote kwa kipindi kirefu bila maelezo kwa miaka isiyo pungua saba continously.

- Kuwa hakuna ushahidi wowote kama mhusika anaishi au anaweza kuwa anaishi.

- Kuwa ndugu, jamaa, marafiki na jamii aliyoishi nao hawana mawasiliano yoyote naye kwa kipindi chote hicho

- Kwamba kuwekuwepo na jitahada mahususi za kumuulizia na kumtafuta lakini hakuna mafanikio yoyote.
 
Reactions: ARV
Andiko murua hili..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…