Sheria hii ni wazi imelenga kumfanya mwajiriwa kuwa mtumwa wa ajira hadi atakapozeeka.Mwajiriwa anapolazimika kusubiri hadi miaka 55 ili achukue mafao yake,ni mateso na yanaleta uchungu usiomithilika kwa wengi.
Kuna mazingira ya kazi ambapo unatumikishwa kama mtumwa bila kujali masaa ya kazi na wakati mwingine matusi juu.Mtu anaamua aache kazi za ajira atoe nafasi kwa wengine wanaotafuta hiyo kazi.
Unaacha kazi una akiba yako ulikuwa unakatwa kila mwezi,na mwajiri anayokuongezea,unaambiwa huichukui hadi ufikishe miaka 55!Hii ni dhuluma ya wazi sana.
Fikiria una miaka 40,mtu anakaa na milioni 10 yako kwa miaka 15! Halafu anakuja kukupa bila riba hata senti tano!
Hii pesa ungeikopa wewe benki tena ya serikali,ungelipa riba usiyopungua milioni 20 katika kipindi hicho.
Huu ukatili dhidi ya wanyonge ni sawa na ugaidi tu unaofanywa na serikali kwa msaada wa wabunge na hakuna lugha nyingine unayoweza kusema.
Kuna pesa mamilioni zinachepushwa kwenda kugharamia timu na kulipa wachezaji wa nje huku watanzania waliofanya kazi halali wakidhulumiwa mafao yao.
Hizi pesa zingekuwa dola za kimarekani angalau zingebaki na thamani yake,lakini fikiria nguvu ya milioni 10 miaka 15 iliyopita inaweza kulingana thamani na milioni 10 ya miaka 15 ijayo?Pesa inashuka thamani kila siku,lakini pesa yako inabaki kuwa ile ile umetunziwa huku inaisha thamani!
Hakika suala hili linatia uchungu sana,sijui hawa wanafanya maamuzi wanafurahia nini kudhulumu pesa za wafanyakazi.Ni bora mngeifanya iwe kwa wafanyakazi wa serikalini tu kuliko kuwajumuisha na wafanyakazi wa kampuni binafsi.
Maana manyanyaso ya serikalini ni nafuu sana kuliko manyanyaso ya kampuni nyingi binafsi.Tunawaomba sana,hatuna silaha ya kupigania haki yetu,bali roho za utu ziwaingie angalau kwa jambo hili tu,mruhusu watu wachukue pesa zao,ili wapambane kujitafutia kwa kujiajiri.Sio kuwalazimisha wakatafute ajira tena, na ajira zenyewe ni ngumu kupatikana