Sheria ya jeshi la Polisi na huduma saidizi na Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai

Sheria ya jeshi la Polisi na huduma saidizi na Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Heshima kwenu wakuu,

Hapa chini nimewawekea viambatanisho vya sheria mbili.Sheria ya jeshi la Polisi na huduma saidizi na Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai. Hii itaweza kuwasaidia Polisi wenyewe kujua haki zao na wajibu wao na kuwaongezea Ufahamu. Vilevile Inasaidia kumuongea Ufahamu Mwananchi wa kawaida kuzijua haki zake na taratibu za kufuata. Inamuongezea mwananchi ufahamu wa nini cha kufanya na kujua taratibu za kimahakama na kipolisi.

Kwenye hii Sheria ya jeshi la Polisi na huduma saidizi wamezungumzia mambo mengi sana. Hivyo ni bora ukafungua PDF ili kujisomea zaidi.

Kwenye hii Sheria ya jeshi la Polisi na huduma saidizi yaliyozungumziwa ni pamoja na;

MUUNDO, UTAWALA NA WAJIBU WA JESHI LA POLISI

1. Uanzishwaji wa Jeshi la polisi.

2. Muundo wa Jeshi la Polisi.

3. Wajibu wa Jeshi la Polisi.

4. [Imefutwa.]

5. Mamlaka ya Mrakibu Mkuu

6. Utawala wa Jeshi.

7. Uwakilishi wa Mrakibu Mkuu

8. Maafisa wasimamizi wa kituo cha polisi kutunza vitabu husika na kupeleka marejesho

9. Maafisa wasimamizi wa polisi kuwajibika kwa maghala.



SEHEMU YA TATU INAONGELEA UTEUZI, UANDIKISHWAJI, UTUMISHI NA KUONDOLEWA


10. Uteuzi wa maafisa polisi.

11. Kipindi cha kuwaajiri marakibu

14 Uandikishwaji wa askari polisi, wafualitiliaji na wanafunzi katika Jeshi la Polisi

15. Tangazo la kujiunga na Polisi

16. Masharti ya likizo.

17. Kuajiriwa upya

18. Kuajiriwa upya baada ya kuondolewa

19 Utumishi katika Jeshi la Polisi jingine yaweza kuhesabika kama utumishi katika Polisi

20. Maafisa polisi kutokujiuzulu bila ruhusa.

21. Wanachama wa Jeshi kutokujihusisha na ajira nyingine

22. Kuongeza muda wa utumishi pale panapokuwa na vita

23. Kuondolewa

24. Masharti katika kuhesabu makosa ya utumishi kwa ajili ya kuondolewa.

25. Kuondolewa baada ya kipindi cha utumishi kumalizika

26. Silaha na vifaa vya askari kuwasilishwa vitakapoacha kuwa mali ya Jeshi.


SEHEMU YA NNE INAONGELEA MAMLAKA NA WAJIBU WA MAAFISA POLISI


27. Mamlaka ya jumla na wajibu wa maafisa polisi

28. Askari polisi kuchukuliwa kama afisa magereza katika mazingira fulani.

29. Maafisa polisi wanaweza kutumia silaha katika jambo fulani.

30. Mamlaka ya kuweka habari na malalamiko

31. Dhamana ya polisi

32. Mahudhurio ya shahidi

33. Kumbukumbu ya mahojiano

34. Hati ya dhamana ya shahidi

35. Upekuzi na afisa polisi

36. Uwezo wa kuchukuwa alama za vidole, picha n.k

37. Uchunguzi wa kitabibu

38. Gwaride la utambuzi

39. Mamlaka ya kukagua leseni na kupekuwa magari

40. Jeshi kuweka amri kwenye barabara za umma.

41. Vikwazo vya barabara

42. Mamlaka ya kudhibiti muziki na vitendo vya mikusanyiko n.k

43. Mikusanyiko na maandamano sehemu za hadhara

44. Mamlaka ya kutawanya mikusanyiko na maandamano popote inapofanyika

45. Wakati mikusanyiko au maandamano ni kinyume na sheria

46. Adhabu


SEHEMU YA TANO INAONGELEA MALI ZISIZODAIWA


47. Kuachiwa kwa mali zisizodaiwa.


SEHEMU YA SITA INAONGELEA MASHTAKA DHIDI YA MAAFISA POLISI


48. Kutokuwajibika kisheria kwa kitendo kilichofanyika chini ya mamlaka ya hati.

49. Mshahara wa maafisa polisi fulani kutokuchukuliwa kwa ajili ya pesa zilizokopwa au bidhaa zilizopelekwa.



SEHEMU YA SABA INAONGELEA NIDHAMU

50. Makosa ya nidhamu

51. Mamlaka ya afisa kufanya uchunguzi

52. Taratibu za uchunguzi

53. Adhabu za makosa ya nidhamu

54. Mamlaka maalum ya Mrakibu Mkuu

55. Mamlaka ya afisa anayefanya uchunguzi

56. Rufaa ya adhabu ya makosa ya nidhamu

57. Kuzuia kukisubiri uchunguzi na kusimamishwa.

58. Afisa aliyezuiwa au kusimamishwa kuendelea kuwa afisa polisi.

59. Kufukuzwa au kushushwa cheo kwa maafisa polisi wanapotiwa hatiani.

60. Faini kupatikana kwa kuzuia malipo.

61. Hasara au uharibifu wa silaha na vifaa vya askari kulipwa kwa kuzuia malipo.

62. Kutokuwepo na malipo wakati wa kukosa kazini bila livu, kifungo au kuwekwa kizuizini

63. Sehemu ya kuwafunga wahalifu.

64. Namna ya malalamiko la afisa polisi

65. Katazo dhidi ya afisa polisi kuwa mwanachama wa chama cha wafanyakazi.


SEHEMU YA NANE INAONGELEA MFUKO WA TUZO WA POLISI


66. Kuanzishwa kwa Mfuko wa Tuzo wa Polisi.



SEHEMU YA TISA INAONGELEA VIINUA MGONGO NA STAHILI AMBAZO ZINAWEZA KUTOLEWA KWA WANACHAMA FULANI WA JESHI AMBAO SIO MAAFISA WANAOSTAHILI MALIPO YA UZEENI.

67. Utumikaji wa vifungu vya 68 hadi 72.

68. Viinua mgongo vinavyolipwa baada ya miezi kumi na mbili au zaidi ya utumishi.

69. Viinua mgongo vyenye uwiano vinavyolipwa katika mazingira fulani.

70. Viinua mgongo vilivyopatikana kuchukuliwa kuwa kama sehemu ya mali ya afisa.

71. Viinua mgongo visivyolipwa mpaka kifo: mpangilio uko je.

72. Fidia panapotokea kifo, dhara au uharibifu unaotokea akiwa kazini.

73. Kiinua mgongo kwa waliopata tuzo.



SEHEMU YA KUMI INAONGELEA MPANGILIO/MGAWANYO WA MALI ZA MAREHEMU


74. Masharti ya mpangilio/mgawanyo wa mali ya maafisa waliokufa bila wosia.

SEHEMU YA KUMI NA MOJA INAONGELEA AJIRA YA MAAFISA POLISI KWA KAZI MAALUMU NA KUDUMISHA AMANI SEHEMU ZENYE GHASIA

75. Ajira ya maafisa polisi kwa kazi maalumu kwa gharama za watu binafsi.

76. Ajira ya nyongeza ya polisi katika mazingira maalumu.

77. Ajira ya nyongeza ya polisi katika sehemu zenye ghasia.

78. Tuzo ya fidia kwa walioumia kutokana na vitendo vibaya vya wakazi wa sehemu zenye ghasia.

79. Tafsiri ya"wakazi".

80. Upatikanaji na mgawanyo/ mpangilio wa pesa zilizolipwa chini ya Sehemu ya XI.

SEHEMU YA KUMI NA MBILI INAONGELEA AFISA POLISI MAALUMU

81. Mamlaka ya kuteua maafisa polisi maalumu.

82. Mamlaka ya kusimamisha kwa muda na kubainisha utumishi wa maafisa polisi maalumu.

83. Raisi anaweza kuanzisha jeshi la maafisa polisi maalumu.

84. Tafsiri ya “afisa polisi maalumu".

85. Kukataliwa/kukataa kwa mtu aliyeteuliwa kutumika

86. Mamlaka na wajibu wa maafisa polisi maalumu.

87. Mrakibu Mkuu kuwapatia maafisa polisi maalumu vifaa muhimu.

88. Sare, n.k, kurudishwa baada ya kumalizika kwa kipindi cha uteuzi.

89. Mrakibu Mkuu kusimamia/kutoa amri.

90. Kulipwa pale panapotokea kifo, dhara, uharibifu wa mali akiwa kazini.


SEHEMU YA KUMI NA TATU INAONGELEA TUMISHI NJE YA JAMHURI YA MUUNGANO


91. Waziri anaweza kuwapeleka maafisa polisi nchi jirani.

92. Kupeleka maafisa polisi nchi jirani wakati wa dharura ya muda.

93. Maafisa polisi wanaotumikia nje ya Jamhuri ya Muungano kuwa chini ya maafisa wao wenyewe na kwa kufuata sheria na amri zao wenyewe.

94. Masharti tangulizi kutimizwa na sheria ya nchi husika.

95. Maafisa polisi kutoka nchi jirani wanaotumikia Jamhuri ya Muungano kuwa chini ya sheria zao, amri na maafisa wao wenyewe.

96. Utekelezaji wa mkataba uliofanywa na Serikali ya nchi jirani.

97. Mamlaka ya wanachama wa jeshi la polisi la nchi jirani.

98. Mamlaka ya mahakama za Jamhuri ya Muungano.

SEHEMU YA KUMI NA NNE INAONGELEA MASHARTI YA JUMLA

99. Mamlaka ya kuendesha mashtaka chini ya sheria nyingine kutodhurika.

100. Uasi.

101. Maafisa polisi walioondolewa kati ya tarehe fulani kutakiwa kuripoti.

102. Kutelekeza.

103. Kumiliki kusiko halali kwa vifaa walivyopewa afisa polisi na uhuishaji kinyume na sheria.

104. Kuwaweka katika nyumba za umma maafisa polisi wakati wakiwa kazini

105. Watu wanaosababisha chuki, n.k.

106. Vitendo visivyokubalika katika kituo cha polisi, ofisini au mahabusu 107. Adhabu ya jumla.


SEHEMU YA KUMI NA TANO INAONGELEA AKIBA YA POLISI

108. Kuanzishwa kwa Akiba ya Jeshi.

109. Muundo wa Akiba

110. Udhibiti wa Akiba

111. Tangazo kutolewa wakati wa uandikishwaji

112. Kipindi cha utumishi katika Akiba

113. Cheo kugawiwa kwa askari wa akiba

114. Haki ya kujiondoa katika mazingira fulani

115. Malipo na posho

116. Wajibu wa askari wa akiba

117. Kuondoa Akiba ya polisi kwa mafunzo ya mwaka

118. Kuondoa Akiba ya polisi kwa ajili ya kutumika wakati wa dharura.

119. Wanapoitwa kwa ajili ya mafunzo au utumishi, taarifa kutolewa kwa akiba ya polisi.

120. Pale ambapo Akiba ya polisi wanaondolewa chini ya masharti ya Sheria hii.

121. Adhabu.

122. Kuondolewa kwa Akiba ya polisi.

123. Inspekta Jenerali Mkuu anaweza kuacha kutumia utumishi wa Akiba ya polisi

124. Viinua mgongo.



SEHEMU YA KUMI NA SITA INAONGELEA JESHI LA POLISI SAIDIZI

125. Tafsiri

126. Kuanzishwa kwa Jeshi la Polisi Saidizi.

127. Kazi za Jeshi la Polisi Saidizi.

128. Mamlaka ya Jumla ya Mrakibu Mkuu.

129. Kutangazwa kwa sehemu maalumu.

130. Jeshi la Polisi Saidizi kuwekwa katika maeneo maalumu.

131. Kuanzishwa na kudumishwa kwa vituo vya polisi katika maeneo maalum.

132. Maeneo maalum kuchukuliwa kuwa moja ya mazingira fulani.

133. Utawala na udhibiti wa jeshi la polisi saidizi katika maeneo maalum.

134. Kuteuliwa kwa maafisa wa jeshi la polisi saidizi.

135. Kujiuzulu.

136. Kufutwa kwa mwongozo

137. Malipo ya polisi saidizi.

138. Vifaa.


139. Mamlaka, Wajibu na kinga ya polisi saidizi.

140. Makosa ya nidhamu.

141. Mamlaka ya kukamata kwa utendaji makosa.

142. Adhabu zinazoweza kutolewa.

143. Kuwasilisha begi, mwongozo,na sare baada ya kujiuzulu, n.k.

144. Kurudishwa kwa begi, mwongozo na sare zilizowasilishwa

145. Makosa.

146. Afisa polisi kwa madhumuni ya kifungu cha 243 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu

147. Mamlaka ya Jeshi la Polisi chini ya Sehemu hii kuwa nyongeza. n. k

Na kwenye hii Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, yaliyozungumziwa ni Pamoja na;

SEHEMU YA KWANZA INAONGELEA MASHARTI YA UTANGULIZI


1. Jina

2. Tafsri.

3. Mipaka ya matumizi.

4. Taratibu ya kufuata kuendesha mashtaka.

SEHEMU YA PILI INAONGELEA UTARATIBU UNAOHUSIANA NA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI

A. – Ukamataji, Utoro, Ukamataji tena, Hati ya Upekuzi na Ukamataji mali


(a) Masharti ya Utangulizi


5. Mtu akiwa kizuizini na katika mahabusu halali kisheria.

6. Matumizi ya Sehemu hii kwa maafisa polisi.

7. Wajibu wa kutoa taarifa za makosa ya jinai na vifo vya ghafla.

8. Uchunguzi wa vifo.

9. Taarifa zinazohusiana na kutendeka kwa kosa kutolewa kwa mdomo au kwa maandishi.

10. Upelelezi wa afisa polisi.


(b) Ukamataji na Hati ya Kukamata



11. Ukamataji unavyofanywa.

12. Kuzuia vizuizi visivyo vya lazima.

13. Hati ya kukamata.

14. Ukamataji na afisa polisi bila hati.

15. Utaratibu endapo afisa polisi anakaimisha ukamataji bila hati

16. Ukamataji unaofanywa na watu binafsi bila hati.

17. Ukamataji unaofanywa na hakimu.



yake.


18. Hakimu anaweza kumkamata mtu kwa kosa lolote linalotendeka mbele


19. Haki ya kuingia sehemu yoyote kwa ajili ya kufanikisha ukamataji

20. Uwezo wa kuvunja sehemu yoyote kwa ajili ya kukomboa.

21. Utumiaji wa nguvu katika ukamataji.

22. Baadhi ya ukamataji kutokuchukuliwa kuwa kinyume na sheria.

23. Mtu kujulishwa sababau za kukamatwa.

24. Upekuzi wa mtu aliyekamatwa.

25. Uwezo wa polisi kuzuia na kukagua magari, n.k.

26. Jinsi ya kupekuwa wanawake.

27. Uwezo wa kutwaa silaha za hatari.

28. Ukamataji wa wazururaji, majambazi wazoefu, n.k.

29. Kukataa kutoa jina na makazi.

30. Udhibiti wa watu waliokamatwa na afisa polisi.

31. Udhibiti wa watu waliokamatwa na watu binafsi.

32. Uzuiaji wa watu waliokamatwa.

33. Polisi kutoa taarifa za ukamataji.

(c) Utoro na Ukamataji tena


34. Ukamataji tena wa watu waliotoroka.

35. Masharti ya vifungu vya 19 na 20 kutumika katika ukamataji chini ya kifungu cha 34.

36. Wajibu wa kumsaidia hakimu au afisa polisi katika kuzuia utorokaji wa mtu aliyekamatwa.

37. Fidia kwa maumivu, hasara au kifo kutokana na kumsaidia polisi, nk.


(d) Hati za upekuzi na ukamataji mali



38. Uwezo wa kutoa hati ya upekuzi au kuruhusu upekuzi

39. Vitu vinavyohusiana na kosa.

40. Utekelezaji wa hati ya upekuzi.

41. Upekuzi na ukamataji.

42. Upekuzi wakati wa dharura.

43. Wasimamizi na sehemu zilizofungwa kuruhusu kuingia na kutoka.

44. Kushikiliwa kwa mali iliyotwaliwa.

45. Vifungu vinavyotumika katika hati ya upekuzi.


B. – Uwezo na wajibu wa maafisa polisi wanapopeleleza makosa


(a) Masharti ya Utangulizi

46. Matakwa ya kutaja jina na anuani.

47. Polisi kuzuia kuvunjika kwa amani au kutendeka kwa makosa yanayoweza kusababisha kukamatwa


kukamatwa.

(b) Muda wa upelelezi chini ya ulinzi wa polisi

48. Mipaka katika kuhoji mtu, nk.

49. Wakati gani mtu asichukuliwe kuwa kuzuizini.

50. Muda unaotakiwa katika kumhoji mtu.

51. Pale ambapo upelelezi chini ya ulinzi hauwezi kukamilika ndani ya saa nne.

(c) Wajibu wakati wa kuwahoji watuhumiwa

52. Kuhoji watu waliotuhumiwa.

53. Watu walio kizuizini kuelezwa haki zao.

54. Mawasiliano na mwanasheria, ndugu au rafiki.

55. Jinsi ya kuwatendea watu walio kizuizini.

56. Wajibu maalum wakati wa kuhoji watoto.


(d) Kuweka kumbukumbu ya mahojiano



57. Kumbukumbu ya mahojiano.

58. Maelezo ya watuhumiwa.


(e) Matendo mengine ya upelelezi

59. Uwezo wa kuchukua alama za vidole, picha, nk, vya watuhumiwa

60. Gwaride la utambulisho.

61. Watu waliohukumiwa kutokana na kutambuliwa kimakosa kulipwa fidia

62. Waziri kutengeneza kanuni za gwaride la utambulisho,nk.

63. Uchunguzi wa kitabibu.

(f) Kuachiwa na Dhamana

64. Dhamana ya polisi kwa mtuhumiwa.

65. Vigezo vya kutoa dhamana ya polisi.

66. Masharti ya dhamana ya polisi.

67. Kukataa kutoa dhamana ya polisi.

68. Kutangua dhamana ya polisi.

69. Ukiukwaji wa masharti ya dhamana.

SEHEMU YA TATU INAONGELEA UZUIAJI WA MAKOSA

(a) Dhamana ya kutunza amani na tabia njema

70. Uwezo wa hakimu kumtaka mtu kutekeleza dhamana.

71. Dhamana ya tabia njema kutoka kwa watu wanaosambaza mambo ya uchochezi.

72. Dhamana ya tabia njema kutoka kwa watu waliotuhumiwa.

73. Dhamana ya tabia njema kutoka kwa wahalifu wazoefu.

74. Amri kutolewa.

75. Utaratibu kuhusu kuwepo mahakamani.

76. Utaratibu kuhusu kutokuwepo mahakamani.

77. Nakala ya amri kuambatanishwa na wito au hati.

78. Uwezo wa kutohitaji mahudhurio binafsi.

79. Uchunguzi wa ukweli wa taarifa.

80. Amri ya kuweka dhamana.

81. Kuachiwa kwa watu ambao taarifa imetolewa dhidi yao.


(b) Mwenendo baada ya Amri ya kuweka dhamana

82. Kuanza kwa muda ambao dhamana inahitajika.

83. Yaliyomo kwenye dhamana.

84. Uwezo wa kukataa wadhamini.

85. Utaratibu kutokana na kushindwa kuweka dhamana.

86. Uwezo wa kuwaachia watu waliofungwa kwa kushindwa kuweka dhamana.

87. Uwezo wa Mahakama Kuu kufuta dhamana.

88. Kuachiwa kwa wadhamini.

SEHEMU YA NNE INAONGELEA USIMAMIZI WA MWENENDO WA JINAI

A. – Mkurugenzi wa Mashtaka

89. [Imefutwa].

90. [Imefutwa].

91. Uwezo wa Mkurugenzi wa Mashtaka kuweka kufuta mashtaka

92. Ukaimishaji wa uwezo wa Mkurugenzi wa Mashtaka.

93. Taarifa za jinai za Mkurugenzi wa Mashtaka.

94. Makosa ya wageni yaliyotendeka ndani ya mipaka ya maji ya nchi kuendeshwa kwa ruhusa ya Mkurugenzi wa Mashtaka tu.

B. – Uteuzi wa Waendesha Mashtaka na Uendeshaji wa Mashtaka

95. [Imefutwa].

96. [Imefutwa].

97. Uwezo wa waendesha mashtaka.

98. Kuondolewa kwa mashitaka katika mahakama za chini.

99. Ruhusa ya kuendesha mashtaka na jina la mwenendo wa mashitaka kwa muhtasari.

SEHEMU YA TANO INAONGELEA UFUNGUAJI WA MASHTAKA

A. – Utaratibu wa kulazimisha mahudhurio ya watuhumiwa

(a) Wito

100. Muundo na yaliyomo kwenye wito.

101. Uwasilishaji wa wito.

102. Uwasilishaji pale mtu anayeitwa hawezi kupatikana.

103. Utaratibu pale uwasilishaji hauwezi kufanyika kwa mtu mwenyewe.

104. Uwasilishaji kwa mtumishi wa Serikali.

105. Uwasilishaji kwenye kampuni.

106. Mahudhurio kwa kampuni na kuandika kukana kosa wakati mwakilishi hajahudhuria.

107. Uwasilishaji nje ya mipaka ya mamlaka ya mahakama.

108. Uthibitisho wa uwasilishaji wakati afisa aliyepeleka hayupo.

109. Mahudhurio ya kampuni.


(b) Hati ya Ukamataji

110. Hati baada ya kutolewa wito.

111. Kutotii wito.

112. Muundo, yaliyomo na muda wa hati ya ukamataji.

113. Uwezo wa kuamuru kuwekwa kwa dhamana.

114. Hati ielekezwe kwa nani.

115. Hati inaweza kuelekezwa kwa mmiliki wa ardhi, n.k.

116. Utekelezaji wa hati inayoelekezwa kwa afisa polisi.

117. Taarifa ya kiini cha hati.

118. Mtu aliyekamatwa kupelekwa mbele ya mahakama bila kuchelewa.

119. Pale hati ya ukamataji inaweza kutekelezwa.

120. Upelekaji wa hati ya utekelezaji nje ya mipaka ya mamlaka ya mahakama.

121. Utaratibu ikiwa hati imeelekezwa kwa afisa polisi kwa utekelezaji nje ya mamlaka.

122. Utaratibu wa kukamata mtu nje ya mipaka ya mamlaka.

123. Makosa katika hati.

(c) Masharti mengine kuhusu mchakato

124. Uwezo wa kuchukua dhamana kwa ajili ya mahudhurio.

125. Ukamataji kwa kuvunja dhamana ya kuhudhuria.

126. Uwezo wa mahakama kuamuru mfungwa kuletwa mbele yake.

127. Masharti ya Sehemu hii yanayotumika kwa ujumla kwa wito na hati; na Uwezo wa mlinzi wa amani.

B. – Mashtaka

(a) Kutoa Lalamiko

128. Kuanzisha mashtaka.

129. Uwezo wa hakimu kukataa lalamiko au shtaka rasmi.

130. Kutolewa kwa wito au hati.

(b) Shtaka Rasmi

131. Watu walioshitakiwa kutahadharishwa

132. Makosa kuainishwa kwenye hati ya mashtaka na maelezo muhimu.

133. Uunganishaji wa makosa katika hati ya mashtaka au taarifa.

134. Uunganisha wa watuhumiwa wawili au zaidi kwenye hati ya mashtaka au taarifa.

135. Muundo ambao makosa yanatakiwa kuandikwa katika hati ya mashtaka.

136. Kesi ya watu wawili au zaidi walioshitakiwa.

(c) Kutiwa hatiani au kuachiwa kwa makosa ya zamani

137. Mtu aliyetiwa hatiani au kuachiwa kutoshtakiwa tena kwa kosa lilelile

138. Mtu anaweza kushitakiwa tena kwa makosa tofauti.

139. Madhara yanayozuka au ambayo hayakujulikana wakati wa kuendesha mashtaka yaliyopita.

140. Pale ambapo mahakama ya awali haikuwa na mamlaka ya kuendesha mashtaka yanayofuata

141. Jinsi ya kuthibitisha kutiwa hatiani kwa makosa ya zamani..

(d) Kulazimisha mahudhurio ya mashahidi

142. Wito kwa shahidi.

143. Hati kwa shahidi asiyetii wito.

144. Hati kwa shahidi katika hudhurio la kwanza.

145. Jinsi ya kushughulikia shahidi aliyekamatwa kwa mujibu wa hati.

146. Uwezo wa mahakama kuamuru mfungwa kuletwa kwa mahojiano.

147. Adhabu kwa kutokuhudhuria kwa shahidi.

(e) Masharti kuhusu dhamana, mdhamana na hati ya dhamana

148. Dhamana.

149. Uwezo wa Mahakama Kuu kubadilisha masharti ya dhamana yaliyotolewa na mahakama za chini.

150. Kubadilika kwa mazingira baada ya kutolewa dhamana.

151. Utekelezaji wa hati za dhamana.

152. Kutolewa chini ya ulinzi.

153. Amana badala ya hati ya dhamana.


154. Uwezo wa kuamuru dhamana inayojitosheleza baada ya ile kwanza kutojitosheleza.

155. Kuachiwa kwa wadhamini.

156. Kufa kwa mdhamini.

157. Watu waliofungwa na dhamana wakiiruka au kukiuka masharti ya dhamana wanaweza kukamatwa tena.

158. Watu wanaoruka au kukiuka masharti ya dhamana kutofikiriwa kupewa dhamana nyingine.

159. Adhabu kwa kukiuka masharti ya dhamana au kutohudhuria.

160. Kutaifishwa kwa mali iliyowekewa dhamana.

161. Rufaa na mapitio ya amri za mahakama.

162. Uwezo wa kutoza ushuru wa kiasi kinachodaiwa katika mali iliyowekewa dhamana.

163. Usuluhishi katika mazingira fulani.

SEHEMU YA SITA INAONGELEA USIKILIZAJI WA KESI

MASHARTI YA JUMLA KUHUSIANA NA USIKILIZAJI WA KESI

A. – Uwezo wa Mahakama

(a) Uwezo kwa Ujumla

164. Makosa chini ya Sheria ya Kanuni za Adhabu.

165. Makosa chini ya sheria nyingine tofauti na Sheria ya Kanuni za Adhabu.

166. Adhabu ambazo Mahakama Kuu inaweza kutoa.

167. Kuunganisha adhabu.

168. Adhabu katika hukumu ya makosa mawili au zaidi katika shtaka moja.

169. Kuachwa kwa ushahidi uliopatikana kinyume cha sheria.

(b) Mahakama za Chini

170. Adhabu ambazo mahakama za chini zinaweza kutoa.

171. Wakati ambao mahakama za chini zinaweza kupeleka shtaka Mahakama Kuu kwa kutoa adhabu..

172. Kuachiwa kwa dhamana kusubiri uthibitisho na uwezo wa mahakama inayothibitisha.

(c) Mamlaka ya Ziada ya Mahakama za Chini

173. Mamlaka ya ziada.

174. Usikilizaji wa kesi kufanywa kwa msaada wa wazee wa baraza.

175. [Imefutwa.]

176. Kumbukumbu na ripoti kupelekwa kwa Rais.

B. – Usikilizaji wa Kesi kwa Ujumla

(a) Sehemu ya Uchunguzi au usikilizaji wa kesi

177. Mamlaka ya jumla ya Mahakama za Tanzania.

178. Uwezo wa Mahakama Kuu kuchunguza na kusikiliza kesi.

179. Mahali na tarehe za vikao vya Mahakama Kuu.

180. Sehemu ya kawaida ya uchunguzi na usikilizaji wa kesi.

181. Usikilizaji wa kesi mahali kosa au mahali matokeo ya kosa yalipojitokeza.

182. Usikilizaji wa kesi pale kosa linahusiana na kosa jingine.

183. Usikilizaji wa kesi pale mahali kosa lilipotendeka hapajulikani.

184. Kosa lililotendeka safarini.

185. Mahakama Kuu inaweza kuamua mahakama inayofaa kukiwa na mashaka.

186. Mahakama kuwa mahakama ya wazi.

187. Kuzuiwa kwa watoto kuhudhuria usikilizaji wa kesi mahakamani.

188. Mahakama inaweza kuzuia kutangazwa kwa majina, nk., ya wahusika au mashahidi.

(b) Kuhamishwa kwa Kesi

189. Kuhamishwa kwa kesi pale kosa limetendeka nje ya mamlaka.

190. Kuhamishwa kwa kesi kati ya mahakimu.

191. Uwezo wa Mahakama Kuu kubadili sehemu.

(c) Usikilizaji kesi mchapuko na namna ya uendeshaji wa Kesi

192. Usikilizaji wa awali katika kuamua mambo yasiyobishaniwa.

193. Mtuhumiwa wa makosa ya kibali anaweza kukiri kosa bila kufika mahakamani.

194. Utaratibu pale mtuhumiwa anataka kukiri kosa lisilo la kibali au anatarajia kutoa utetezi wa alibi.

C. – Kuhojiwa kwa Mashahidi

(a) Masharti ya jumla

195. Uwezo wa kuita shahidi muhimu au kumhoji mtu aliyepo.

196. Ushahidi kuchukuliwa mbele ya mtuhumiwa.

197. Ushahidi unaweza kuchukuliwa bila kuwepo mtuhumiwa katika mazingira fulani.

198. Ushahidi kutolewa kwa kiapo.

199. Shaidi kigeugeu.

200. Utaratibu pale mtuhumiwa ni shahidi pekee aliyeitwa katika utetezi.

201. Haki ya kujibu.


202. Hati kuhusiana na utayarishaji wa alama za picha, nk., zinazopokelewa katika ushahidi.

203. Taarifa ya Mchambuzi wa Serikali.

204. Taarifa ya mtaalamu wa alama za vidole.

205. Taarifa ya mtaalamu wa maandishi.

(b) Kutolewa kwa Idhini ya Kuwahoji Mashahidi

206. Kutolewa kwa idhini.

207. Wahusika wa kesi wanaweza kuwahoji mashahidi.

208. Kurudishwa kwa idhini.

209. Kuahirishwa kwa kesi.

(c) Kuchukua na Kuweka Kumbukumbu ya Ushahidi

210. Jinsi ya kuweka kumbukumbu ya ushahidi mbele ya hakimu.

211. Tafsiri ya ushahidi kwa mtuhumiwa au wakili wake.

212. Maoni kuhusiana na mwonekano wa shahidi.

213. Utaratibu kwa makosa madogo.

214. Kutiwa hatiani au upelekaji wa kesi ikiwa imesikilizwa kwa sehemu na hakimu mmoja na sehemu nyingine na hakimu mwingine.

215. Jinsi ya kuweka kumbukumbu ya ushahidi Mahakama Kuu.


D. – Utaratibu kuhusu Mtuhumiwa mwenye Ulemavu wa Akili au Udhaifu


216. Mwendesha mashtaka kutoa au kuleta ushahidi kabla mahakama haijafanya uchunguzi kuhusiana na ulemavu wa akili wa mtuhumiwa.

217. Utaratibu wakati mtuhumiwa amethibika kuwa na uwezo wa kujitetea.

218. Kurudiwa kwa usikilizaji wa kesi au uchunguzi.

219. Utetezi wa ulemavu wa akili katika usikilizaji wa kesi.

220. Uwezo wa mahakama katika kuchunguza ulemavu wa akili.

221. Utaratibu wakati mtuhumiwa haelewi mwenendo wa kesi.

SEHEMU YA SABA INAONGELEA UTARATIBU WA KUENDESHA KESI MBELE YA MAHAKAMA ZA CHINI

(a) Masharti yanayohusiana na Usikilizwaji na Uamuzi wa Kesi

222. Kutokuhudhuria kwa mlalamikaji siku ya kusikiliza kesi.

223. Kuhudhuria kwa pande zote.

224. Kuondolewa kwa lalamiko.

224A. Kukoma kwa shauri katika mahakama za chini.

225. Kuahirishwa na kuwekwa ndani kwa mtuhumiwa.

226. Kutokuhudhuria kwa pande zote baada ya kuahirisha.

227. Mtuhumiwa anaweza kutiwa hatiani na kuhukumiwa adhabu hata kama hayupo.

228. Mtuhumiwa kuitwa kujibu mashitaka.

229. Utaratibu iwapo shitaka linakanwa.

230. Kuachiwa kwa mtuhumiwa kama hakuna kesi ya kujibu.

231. Utetezi.

232. Ushahidi katika majibu

233. Utaratibu wa hotuba.

234. Kutofautiana kwa mashitaka na ushahidi na kusahihishwa kwa mashitaka.

235. Uamuzi

236. Ushahidi unaohusiana na adhabu au amri muafaka.

237. Kuzingatia makosa mengine.

238. Kuandaa amri za kutiwa hatiani au kuachiwa.

239. Amri ya kuondolewa mashitaka mengine.

240. Maelezo ya mashahidi wa kitabibu.

(b) Ukomo na misamaha kuhusiana na uendeshaji wa kesi katika mahakama za chini

241. Ukomo wa muda kwa mashitaka ya muhutasari katika mazingira fulani.

242. Utaratibu kwa kosa ambalo halifai kuendeshwa kwa muhtasari.

(c) Kupeleka Watuhumiwa Kwa Ajili ya Mashtaka Mahakama za Chini kwenda Masharti Mahakama kuu kwa usikilizaji

a) Masharti yanayohusiana na kupelekwa Watuhumiwa kwa ajili ya Mashtaka Mahakama Kuu

243. Uwezo wa kupeleka shaurii

244. Mahakama kuendesha mashauri yaliyoletwa

245. Utaratibu wa kukamata

246. Kupelekwa kwa ajili ya kusilikizwa na mahakama.

247. Mashahidi wa upande wa mashitaka na upande wa utetezi.

248. Kuahirishwa kwa shauri.

249. Mtuhumiwa ana haki ya kupewa mwenendo wa kesi.

250. Mahakama inaweza kumlazimisha shahidi kuhudhuria kwenye shauri

251. Kukataa kulazimishwa.


(b) Kutunzwa kwa ushahidi katika mazingira fulani

252. Kuchukua ushahidi wa watu wanaoumwa sana na wasioweza kuhudhuria shauri.

253. Taarifa kutolewa

254. Nafasi ya kuhoji ushahidi na kuhamisha maelezo.

255. Matumizi ya maelezo katika ushahidi.


(c) Mwenendo baada ya Kuhamishwa kwa ajili ya kusikilizwai.

256. Kuhamisha kumbukumbu kwenda Mahakama Kuu. 256A. Kusikilizwa na hakimu mkazi mwenye mamlaka ya ziada.

257. Taarifa ya shauri.

258. Nakala ya habari na taarifa ya kusikilizwa kuwasilishwa.

259. Kurudishwa kwa uwasilishaji.

260. Kuahirishwa kwa shauri.

261. Taarifa isainiwe na Mkurugenzi wa Mashitaka.

262. Muundo wa taarifa.

263. Mashahidi kuitwa.

SEHEMU YA NANE INAONGLEA UTARATIBU WA KUSIKILIZA MBELE YA MAHAKAMA KUU

(a) Utendaji na jinsi ya Kusikiliza

264. Utendaji wa Mahakama Kuu katika mamlaka yake ya jinai.

265. Usikilizaji mbele ya Mahakama Kuu lazima uwe na msaada wa wazee wa baraza.

(b) Wazee wa Baraza

266. Wajibu wa kutumikia kama Mzee wa Baraza.

267. Misamaha.

268. Hakuna msamaha wa kijinsia au kindoa katika wajibu wa kutumikia kama Mzee wa baraza.

(c) Mahudhurio ya Wazee wa Baraza

269. Kuwaita Wazee wa Baraza.

270. Muundo wa wito.

271. Pingamizi kuitwa kutumikia kama Mzee wa Baraza.

272. Udhuru wa kutofika.

273. Orodha ya Wazee wa Baraza wanaohudhuria.

274. Adhabu kwa kutohudhuria kwa wazee wa Baraza.

(d) Tuhuma

275. Kujibu taarifa.

276. Amri za kurekebisha taarifa, usikilizaji tofauti na uahirishaji wa usikilizaji.

277. Kutupiliwa mbali kwa taarifa.

278. Utaratibu ikiwa mtuhumiwa alitiwa hatiani zamani.

279. Jibu la ‘kukana shitaka’.

280. Jibu la ‘autrefois acquit’ na ‘autrefois convict’.

281. Kukataa kujibu.

282. Jibu la ‘kukubali kosa’.

283. Mwenendo baada ya kukana shitaka.

284. Uwezo wa kuahirisha mwenendo wa kesi. 284A. Kukoma kwa shitaka mbele ya Mahakama Kuu.

(e) Uteuzi wa Wazee wa Baraza

285. Uteuzi wa Wazee wa Baraza.

286. Kutokuwepo kwa Wazee wa Baraza.

287. Wazee wa Baraza kuhudhuria baada ya kesi kuahirishwa.

(f) Kesi ya Upande wa Mashitaka

288. Kufungua kesi ya upande wa mashitaka.

289. Mashahidi wa nyongeza kwa upande wa mashitaka.

290. Kuhojiwa mashahidi wa upande wa mashitaka.

291. Maelezo ya mashahidi wa kitabibu.

292. Maelelezo ya ushahidi ya mtuhumiwa.

293. Kufunga kesi ya upande wa mashitaka.

(g) Kesi ya Upande wa Utetezi

294. Kesi ya upande wa utetezi.

295. Mashahidi wa nyongeza wa upande wa utetezi.

296. Majibu ya upande wa mashitaka.

297. Pale ambapo mtuhumiwa hatoi ushahidi.

(h) Kufungwa kwa Usikilizaji kesi

298. Wazee wa Baraza kutoa maoni yao na kutolewa kwa hukumu.

299. Kutiwa hatiani kama kesi ilisikilizwa na majaji wawili kwa nyakati tofauti.

SEHEMU YA TISA INAONGELEA KUTIWA HATIANI, HUKUMU, VIFUNGO NA UTEKELEZAJI WAKE KATIKA MAHAKAMA ZA CHINI NA MAHAKAMA KUU

A. – Masharti mbalimbali yanayohusiana na Kutiwa Hatiani

300. Kama kosa lililothibitishwa limejumuishwa katika mashitaka

301. Mtu aliyeshitakiwa kwa kosa anaweza kutiwa hatiani kwa kujaribu kufanya kosa hilo.

302. Hukumu mbadala katika mashitaka mbalimbali yanayohusu mauaji ya watoto.

303. Hukumu mbadala katika Sheria ya Usalama Barabarani katika baadhi ya makosa ya kuua bila kukusudia.

304. Hukumu mbadala katika mashitaka ya ubakaji na makosa yanayofana nayo.

305. Mtu aliyeshitakiwa kwa uvunjaji nyumba usiku, nk, anaweza kutiwa hatiani kwa makosa yanayofanana nayo.

306. Hukumu mbadala kwa mashitaka ya wizi na makosa yanayofanana nayo.

307. Hukumu mbada katika mashitaka ya kukutwa na mali zinazodhaniwa kuwa zimepatikana kwa nia ya rushwa.

308. Tafsiri ya vifungu vya 300 mpaka 307.

309. Mtu aliyeshitakiwa kwa kosa la kibali asiachiwe kama kosa lisilo la kibali limethibitishwa.

310. Haki ya mtuhumiwa kutetewa.


B. – Hukumu kwa Ujumla


311. Jinsi ya kutoa hukumu.

312. Yaliyomo kwenye hukumu.

313. Nakala ya hukumu, n.k, kutolewa kwa mtuhumiwa au mtu mwingine mwenye maslahi ikiwa ataomba.


C. – Hukumu

(a) Kutoa Hukumu Mahakama Kuu

314. Kumwita mtuhumiwa.

315. Mwenendo katika kukamatwa kwa hukumu.

316. Hukumu.

317. Uwezo wa kuweka akiba uamuzi wa maswali yaliyojitokeza katika usikilizaji wa kesi.

318. Uwezo wa ya kuweka akiba maswali yaliyojitokeza katika usikilizaji wa kesi.

319. Pingamizi zilizowekwa kuponywa na hukumu.

320. Ushahidi wa kufikia hukumu sahihi.

321. Kutilia maanani makosa mengineyo.

(b) Hukumu ya Kifo

322. Hukumu ya kifo.

323. Mtuhumiwa kuambiwa haki ya kukata rufaa.

324. Mamlaka ya kumweka mtu kizuizini.

325. Taarifa na kumbukumbu kupelekwa kwa Rais.

(c) Hukumu nyingine

326. Kuachiwa kwa masharti.

(d) Kutekelezwa kwa Hukumu

327. Kibali kama ni hukumu ya kifungo.

328. Kibali kwa kulipa faini.

329. Pingamizi katika kukamata mali.

330. Kusimamishwa kwa utekelezaji wa hukumu ya kifungo kwa kushindwa kulipa faini.

331. Kushikiliwa endapo mtuhumiwa hana mali za kukamata ili kulipa faini.

332. Kushikiliwa kama mbadala wa kuuza mali za mtuhumiwa.

333. Malipo yote baada ya kushikiliwa.

334. Malipo kidogo baada ya kushikiliwa.

335. Nani anaweza kutoa kibali.

336. Mwisho wa kifungo baada ya kushikiliwa.

D. – Masharti mbalimbali katika kuwashughulikia wakosaji

(a) Wakosaji wa kwanza

337. Uwezo wa kumuachia kwa matazamio badala ya kuhukumu kwa adhabu.

338. Masharti kama mkosaji atashindwa kufuata masharti ya dhamana.

339. Masharti kuhusu makazi ya mkosaji.

339A. Kumuachia mkosaji kwa masharti ya kuitumikia jamii.

340. Vifungu vya 337, 338 na 339 kutotumika katika mazingira fulani.

(b) Mkosaji aliyewahi kutiwa hatiani

341. Uwezo wa kuamuru kuwa chini ya uangalizi wa polisi.

342. Matakwa kutoka kwa mtu aliyewekwa chini ya uangalizi wa polisi.

343. Kushindwa kukidhi matakwa chini ya kifungu 342.

(c) Dosari katika Amri au Kibali

344. Makosa na vitu vilivyorukwa kwenye amri na vibali.

E. – Uwezo mbalimbali wa Mahakama kuamuru Fidia, gharama, kutaifisha, n.k.

(a) Gharama na Fidia

345. Gharama dhidi ya mtuhumiwa.

346. Amri ya kulipa gharama inaweza kukatiwa rufaa.

347. Fidia katika mashitaka yasiyo na msingi au ya kuudhi.

348. Uwezo wakuamuru mtuhumiwa alipe fidia. 348A. Fidia katika kesi za kujamiiana.

349. Gharama na fidia zionyeshwe kwenye amri na jinsi ya kuzipata.

350. Uwezo wa mahakama kutoa gharama au fidia ndani ya faini.

(b) Kutaifisha

351. Uwezo wa kutaifisha mali.

352. Kibali cha upekuzi kwa mali iliyotaifishwa.

(c) Udhibiti wa vielelezo

353. Udhibiti wa vielelezo.

354. Udhibiti wa wa machapisho yanayodhalilisha au kashfa au vyakula vyenye madhara au visivyofaa, nk..

355. Mtu aliyenyang’anywa mali anaweza kurudishiwa.

356. Afisa wa umma anayehusiana na uuzwaji wa mali hatakiwi kununua au kuonesha nia ya kununua mali hiyo.

F. – Kukomboa Mali

357. Mali iliyokutwa kwa mtuhumiwa.

358. Mali iliyoibwa.

SEHEMU YA KUMI INAONGELEA RUFAA

(a) Rufaa kwa Ujumla

359. Rufaa kwenda Mahakama Kuu.

360. Hakuna rufaa katika jibu la kukubali kosa.

361. Kikomo

362. Ombi la Rufaa.

363. Muomba rufaa aliye gerezani.

364. Kukataliwa kwa rufaa kwa muhtasari.

365. Taarifa ya muda na mahali pa kusikiliza.

366. Uwezo wa Mahakama Kuu katika rufaa na haki ya mkata rufaa kuhudhuria.

367. Amri ya Mahakama Kuu ithibitishwe kwenda mahakama za chini.

368. Kusimamishwa kwa hukumu na kupatiwa dhamana kusubiri rufaa.

369. Ushahidi wa ziada.

370. Idadi ya majaji katika rufaa ya mkata rufaa.

371. Kuondolewa kwa rufaa.

371A. Kukoma kwa rufaa baada ya mkata rufaa kufariki.


(b) Mapitio

372. Uwezo wa Mahakama Kuu kuita kumbukumbu.

373. Uwezo wa Mahakama Kuu katika mapitio.

374. Uamuzi wa Mahakama kuwasikiliza wahusika wa kesi.

375. Idadi ya majaji katika mapitio.


376. Amri ya Mahakama Kuu ithibitishwe kwenda mahakama ya chini.

(c) Rufaa ya Mkurugenzi wa Mashitaka

377. Tafsiri.

378. Rufaa za Mkurugenzi wa Mashitaka.

379. Kikomo

380. Ombi la rufaa.

381. Taarifa ya muda na mahali pa kusikiliza kesi.

382. Mkurugenzi wa Mashitaka anaweza kutoa hoja mbele ya mahakama.

383. Kutofika kwa wahusika.

384. Ushahidi wa zaida.

385. Idadi ya majaji katika rufaa ya Mkurugenzi wa Mashitaka.

386. Kuondolewa kwa rufaa na Mkurugenzi wa Mashitaka. 386A. Kukoma kwa rufaa mjibu rufaa akifariki.

SEHEMU YA KUMI NA MOJA MASHARTI YA ZIADA

(a) Mwenendo wenye Makosa

387. Mwenendo kwenye sehemu isiyo sahihi.

388. Maamuzi au hukumu, wakati gani yaweza kubadilishwa kwa sababu ya makosa au kuruka vitu kwenye mashitaka au mwenenendo.

389. Kukamata vitu sio kinyume na sheria wala mkamati wa vitu sio mvamizi kutokana na makosa katika mwenendo.

(b) Maelekezo katika asili ya amri ya Habeas Corpus na Writ

390. Uwezo wa kutoa maelekezo yenye asili ya Habeas corpus.

391. Uwezo wa Mahakama Kuu kutoa Writs.

(c) Mengineyo


392. Watu ambao viapo vinaweza kuapwa mbele yao.

393. Nakala ya mwenendo wa kesi.

394. Fomu.

395. Gharama ya wazee wa baraza, mashahidi, n.k.

396. [Imefutwa.]

Wakuu, hizi PDF zimezungumzia mambo mengi yenye manufaa. Unaweza ukapakuwa ukawa unajisomea unapopata nafasi. Itasaidia kuwa na jamii bora. Nmeweka pdf na DOCX, hivyo unaweza kupakuwa kwa mfumo uupendao.

Asanteni
 

Attachments

Mkuu nadhani hili bandiko kuna baadhi ya vitu hapa ni kwa matumizi ya polisi tu...haviruhusuwi kwa raia wa kawaida ...anyway sijui utaratibu wake vizuri
 
Mkuu hii imefanyiwa amendment au??? Ninayo CPA cap 20 act ya mwk 1985 lakini sec ,89,90 hazijafutwa na hapo zinaonyesha replied inakuwaje nipe ufafanuzi na imekuwa updated lin???
 
Mkuu hii imefanyiwa amendment au??? Ninayo CPA cap 20 act ya mwk 1985 lakini sec ,89,90 hazijafutwa na hapo zinaonyesha replied inakuwaje nipe ufafanuzi na imekuwa updated lin???
Mkuu hiyo unayosema sijawahi kuiona. Ambazo zimefuta zimebainishwa kwa maneno imefutwa. Jaribu kufuatia hiyo yako kama haijawahi ganyiwa marekebisho.
 
Back
Top Bottom