Sheria ya kulinda watoto!

Aaronium

Senior Member
Joined
Oct 31, 2011
Posts
129
Reaction score
9
Wadau nawasalimu!

Nimetembelea wavuti ya The global Publisher leo tarehe 11-11-11 kujaribu kupata habari mbalimbali za yaliyojiri katika sehemu hii ya wadau wa habari pamoja na wengine, nimepata mfadhaiko na mshtuko kuiona habari moje inayo husu mabinti kupachikwa mimba na wasanii kisha kutelekezwa, suala tata hapa si hiyo habari kwa ujumla isipokuwa habari picha ambazo zimetumika na kuwaangaza akina mama hao wahusishwa na habari wakiwa na watoto wao bila kufichwa utambulisho wao!

Kikiwa ni chombo ambacho kinawajibika kufuata sheria ya nchi na kutovunja maadili ya habari naona Global Publishers hapa wamepotoka na kuvuka mipaka mpaka kupitiliza kwa uroho wa kuuza magazeti yao, natumaini wahusika wataliona hili na ku-regulate hawa wanaojiita waandishi wa habari wasioijua na kuidhalilisha taaluma hii na kuleta fedheha kwa hao viumbe wasio husika na hizo habari!

Kwa kosa hili tu natumaini watapata adhabu itakayowafunza namna ya kuchanganua mambo pale wanapotaka kufikisha ujumbe kwa  jamii, swali gumu ni kwamba, hii habari je inamaana ya kuelimisha, kuburudisha au kukejeli tu watu bila kuwa na simile!

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…