Suala la mpangaji na mwenye nyumba(landlord and tenant) linaongozwa na sheria mbili, ya kwanza ni sheria ya ardhi namba nne ya mwaka 1999, na sheria ya mikataba (law of contract). Kimsingi sheria ya ardhi upande wa upangaji imeweka minimum or principle issues ambazo zitaongoza suala lolote linalohusu upangaji katika mainland tanzania. Hivyo, hata kama mmeingia kwenye mkataba na ukawa na mapungufu, sheria ya ardhi upande wa lease huyajazia mapungufu hayo. Hivyo basi, kwa suala tajwa hapo juu, kama mkataba wenu haukuongelea notisi, kwa mujibu wa sheria, notisi ni siku 30, japo kwa sasa sikumbuki kifungu halisi. Hata hivyo, kama nlivyosema,suala la upangaji pia linaongozwa na sheria ya mkataba ndio maana wahusika husaini MKATABA WA UPANGAJI. Ni nini maana yake? Maana yake wahusika kwa kutumia sheria ya mkataba wanaweza kuweka vipengele vyao vya kuwaongoza na vipengele hivyo vinakuwa na nguvu baina yao. Kwa mfano, kama eneo ni la biashara, haiwezekani kutoa notisi ya siku thelasini kwa kuwa mpangaji lazima apewe muda wa kutafuta eneo la kibiashara kama analohama. Kama mpangaji alikodishwa eneo la hoteli ghorofa tano, lazima ajikinge dhidi ya notisi fupifupi kwa kuweka kipengele katika mkataba. Hivyo ni muhimu sana kutafakari kila kipengele kwa kina na kwa kuangalia mbele. Lastly, kwa wapangaji na wenye nyumba, .notisi inatolewa ndani ya muda wa mkataba, mfano kama mkataba unasema notisi ni mwezi mmoja, .notisi hiyo itolewe kabla mkataba haujaisha, si baada ya mkataba kuisha kwa kuwa utamruhusu mpangaji kukaa bure one more month after the expiry of the contract