kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,677
...Kabla ya kuileta "SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA"
Sura ya 83 (toleo lililorekebiwa la mwaka, 2012)
...kuna haya yaliyowapeleka wapinzani hadi Ikulu wakakutana JK, wakitoa shindikizo hasiweke sahihi sheria hiyo ya mwaka 2011..., na sasa imejitokeza tena mwaka..., je tutafika kwa mwendo huu?
Kwanza tuanze na hii ya mwaka 2011
sheria Mama tuliyonayo
ndio chanzo cha matatizo yote haya. Tusipoteze focus na
kuacha kushughulika na mzizi hasa
wa tatizo letu. Utawala mbovu na
mifumo mibovo inayolindwa na
Katiba mbaya ambayo haileti
uwajibikaji na kuwapa mamlaka na nguvu wananchi ndio msingi wa
matatizo yetu. Inawezekana
wajanja wachache wanaleta
masuala haya ili tuache kujadili
masuala ya msingi. Wana shift goal
post. Tuwe focus na consistent. Tusiwe na mada za wakati, zinakuja
na kuondoka, consistency ni
muhimu sana. Mpaka jambo lifike
mwisho wake. Jukwaa la Katiba
mmekuwa kimya sana. Pia wasomi
na wanaharakati wengine. Vipi? Kulikoni? au wamepenyeza ahadi
tamu tamu? Kwani nimeanza kuona
makundi mbalimbali, kila mmoja
kwa wakati wake yanakutana na
serikali yakiomba kushirikishwa
katika Tume na kadhalika.
Tanzania kiboko, yaani Kila jambo ni
kuchumia tumboni tu. Wengi
tunafikiria tumboni tu. Mwishoni mwa mwezi Novemba,
Rais Jakaya Kikwete alisaini
muswada wa sheria ya Mabadiliko
ya Katiba ya Mwaka 2011. Pamoja
na kusaini muswada huo, taarifa ya
Ikulu ilisema kuwa: kwa mwananchi yoyote mwenye maoni ama mawazo ya namna ya kuboresha sheria hiyo, ajisikie yuko huru kutoa maoni yake na Serikali itasikiliza na kuchukua hatua zipasazo.Kwa bahati mbaya taarifa hiyo
haikusema namna au utaratibu gani
wananchi wanaweza kuutumia
kufikisha maoni yao ili sheria hiyo
iweze kubadilishwa. Nimeisoma sheria hiyo na
nimetatizwa na vipengele kadhaa,
kwa kuwa mimi si mwana sheria,
nimeona kuwa ni vyema nilileta
kwenu ili niweze kuelimishwa. (1) "Tume itaongozwa na misingi mikuu ya kitaifa na maadili ya jamii ya kuhifadhi na kudumisha mambo yafuatayo: mojwapo ni (g) ukuzaji na uhifadhi wa haki za binadamu." Ninavyoelewa mimi, moja ya haki za binadamu ni uhuru wa kujieleza,
kutoa maoni yako, kupinga au
kuunga mkono, kubadilishana
mawazo na wenzako na
kujiorganize kama asasi, chama au
kikundi. Kama niko sahihi kwa hili, kwa nini tena uwe na kipengele
ambacho kinanyang'anya uhuru
huo?!! {Angalia kipengele
kinachotajwa katika para
zinazofuata, kipengele 'a' na 'c'}: a)
atakayefanya shughuli ya kukusanya na kuratibu maoni ya
wananchi kinyume na Sheria hii; c)
atakayeendesha programu ya elimu
juu ya mabadiliko ya Katiba
kinyume na masharti ya Sheria hii.
Hapa naona kuna mkanyiko na vipengle kupingana. Naomba
mnisaidie. "Kutakuwa na Sekretarieti ya Tume itakayoongozwa na Katibu akisaidiwa na Naibu Katibu. (2) Katibu na Naibu Katibu watateuliwa na Rais baada ya kushauriana na kukubaliana na Rais wa Zanzibar . (4) Katibu na Naibu Katibu watawajibika kwa Tume na watafanya kazi na kutekeleza majukumu ya Sekretarieti." Hapa ninashangazwa na utaratibu
huu, yaani watendaji hawa
wanateuliwa na Rais lakini
wanawajibika kwa Tume!! Jee hiyo
ndio njia bora ya uwajibikaji? Ni
kweli watawajibika kwa Tume wakati wameteuliwa na Rais? "Tume inaweza: (a) Kwa Tanzania Bara, kumtaka Mkuu wa Wilaya, Afisa Mtendaji wa kata au Mtaa au Afisa Mtendaji wa Kijiji kuitisha mkutano wa wakazi wa mji, kata, mtaa au kijiji, kwa vyovyote itakavyokuwa;" Je Wakuu wa Wilaya ambao
wengi wao ni makada wa
chama tawala na wateuliwa
wa Rais, kweli watakuwa
impartial kufanya kazi hii?? ("8) Mtu au asasi yoyote itakayotaka kuendesha programu ya kutoa elimu juu ya mchakato wa mabadiliko ya katiba, kabla ya kuanza kutoa elimu hiyo, sharti iwe imesajiliwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania Bara au Tanzania Zanzibar na itawajibika kueleza kwa Tume chanzo cha fedha ya kuendesha programu hiyo." Sina tatizo na suala la usajili, lakini
nashindwa kuelewa mantiki ya
kuwa itawajibika kuleza kwa Tume
chanzo cha fedha ya kuendesha
programu hiyo. Mantiki yake hapa
ni nini? "(4) Kwa madhumuni ya kifungu kidogo cha (3), Mwenyekiti wa Tume hatokuwa mjumbe wa Bunge Maalum na mara baada ya kuwasilisha Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum atapaswa kutoka kwenye Bunge Maalum." Naona ni jambo la ajabu sana kwa
mtu anayewasilisha rasimu
kutokupewa nafasi ya kutoa
ufafanuzi juu ya masuala na hoja
kadhaa. Nilidhani kuwa mtu
aliyeshiriki kuandaa rasimu ni vyema pia akapewa nafasi ya kutoa
ufafanuzi wa masuala kadhaa pale
itakapolazimika. Kwa sababu yapo
mengine labda yatahitaji ufafanuzi
tu. "MAKOSA NA ADHABU 21-(1) Mtu yeyote atakayemkwamisha au kumzuia kwa makusudi- (a) Mjumbe wa Tume au Sekretariati kutekeleza majukumu au mamlaka ya Tume; (b) Mtu au kundi la watu kutoa maoni kwenye Tume, atakuwa ametenda kosa. (2) Mtu yeyote- (a) atakayefanya shughuli ya kukusanya na kuratibu maoni ya wananchi kinyume na Sheria hii; (b) atakayejifanya kuwa mjumbe wa Tume au Sekretaria; au (c) atakayeendesha programu ya elimu juu ya mabadiliko ya Katiba kinyume na masharti ya Sheria hii, Atakuwa ametenda kosa. (3) mtu atakayetiwa hatiani kwa kutenda kosa kinyume na Sheria hii, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tano na isiyozidi shilingi milioni kumi na tano au kifungo kwa muda usiopungua miaka mitatu na usiozidi miaka saba au adhabu zote mbili." Kumkwamisha au kumzuia
makusudi?? maana yake
nini? Kutoa maoni kwenye tume,
maana yake nini? Je iwapo
mwananchi akijenga hoja
kwa wananchi wenzake au
akiandika makala au akitoa
mhadhara na kuwaambia wananchi wenzake kuwa
wasiende kutoa maoni
kwani mchakato
haukuwashirikisha
wananchi, akijenga hoja
kuwa waikatae rasimu ya katiba wakati wa kura ya
maoni atakuwa amevunja
sheria? Kama ni hivyo
uhuru wa kupingana na
kujieleza na kutoa maoni
ambao unalindwa na hata hii katiba ya viraka upo
wapi? Mh. Kafulila aliwahi kusema
wao wanafikiria kuandaa
utaratbu utakaokwenda
sambamba na huu, kwa
kipengele (a) atakuwa
ametenda kosa. Aidha hairuhusiwi hata
kuendesha elimu juu ya
mabadiliko ya Katiba
kinyume na sheria hii. Je ina
maana yake ni nini? Ina
maana hata ninachoandika hapa ni kosa na ninastahili
kwenda jela na kulipa faini? Sishangai ndio maana kuna
wakati Mwanasheria mkuu
wa Serikali aliwahi
kupendekeza kuanzisha
sheria ya kudhibiti
maandamano. Yapo mengi sana, lakini
labda tuanza na hayo.
Sheria hii inapatikana katika
dula la Serikali ni muhimu
tukaisoma.
KARIBUNI KWA MICHANGO