GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Kwenu wajuvi wa Sheria!
Kwenye clip hapo chini ni malalamiko ya mtu anayedai kutapeliwa. Tukio lilitokea Arusha. Mlalamikaji aliuziwa shamba la ekari 2 kwa milioni hamsini na nne. Lakini alipotaka kuanza kulitumia shamba lake, alilikuta limeuzwa kwa mtu mwingine.
Mtuhumiwa alifunguliwa kesi ya jinai, na baada ya kushindwa mara kadhaa, kesi ilibadilishwa na kuwa ya madai na bado akashindwa. Pamoja na mlalamikaji kushinda, ilibainika kuwa mlalamikiwa hakuwa na mali za kumfidia mlalamikaji. Nyumba yake aliiandikisha familia yake.
Mlalamikaji akaamua kupunguza "machungu" ya kutapeliwa kwa kumfunga gerezani. Lakini huko nako kukawa ni kichekesho.
Utaratibu unamtaka amhudumie mfungwa wake kwa muda wote atakaokuwa gerezani:
1. Kifungua kinywa
2. Mlo wa Mchana na Jioni
3. Maji
Gharama ya mahitaji ya kila siku ni sh 22,000/=
Atahusika pia kumpatia godoro na blanketi, pamoja na kugharamia matibabu yake na mahitaji mengine.
Nitakosea nikisema Sheria ya madai Tanzania inawapendelea matapeli?
Kuna haja ya kuendelea kuwa na Sheria ya vituko kama hiyo?