Tetesi: Sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii inayolenga kuua kabisa ustawi wa wafanyakazi

Tetesi: Sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii inayolenga kuua kabisa ustawi wa wafanyakazi

KingKacha

Senior Member
Joined
Jun 15, 2016
Posts
118
Reaction score
119
Wakuu nimeona mjadala huu na nkaona una mapungufu makubwa nabya kinyonyaji sana kiasi kwamba kuajiriwa sasa kutakuwa ni utumwa zaidi ya ilivyo sasa.

Sijazama kuona ukweli wa haya hapa chini lakini naguswa sana na ninauona udikteta unajidhihirisha katika hili.

Kwamba
http://
Bill hiyo inaenda kuua wastaafu.
1. Mafao utalipwa 38% na 62% utakuwa unalipwa monthly. Mfano kama ilikuwa ulipwe milioni 100 maana yake kwa mswada mpya utalipwa pension ya mkupuo 38 milioni halafu milioni 62 ulipwa kila mwezi. Ubaya wa hili siku ukifa malipo kila mwezi hukoma. Hivyo hela nyingi zitabaki kwenye mifuko maana rekodi inaonyesha wastaafu wengi hawaishi muda mrefu na hasa ukizingatia mafao yatapungua.

2. Mume akifa Mke na wategemezi watahudumiwa miaka 3 tu kisha huduma itakoma.

3. March 2018 mifuko itaunganishwa kubaki mifuko 2 tu.

4. April 2018 sheria itaanza kutumika.

Kwa ufupi muswada huu utaumiza watumishi wote. Wabunge wetu wasipoliona hili kuwasemea watumishi basi tutaumia.
 
Aisee.This is hell

Yaani hawa jamaa kweli wanaamua kuwamaliza watu hivi hiviiiii

Yaani hawataki kuwapa watu fedha zao.

Wabunge wa CCM muwe na akili japo kidogo basi.Saidieni wananchi katika hili
 
Aisee huo ni unyonjaji, ukabaila, ubeberu, umangimeza, ugabacholi n.k.
 
Ipo siku.

People Mark my words..... Ipo siku.
 
kweli nimeamini kuajiriwa ni utumwa mamboleo..

maisha yako unapangiwa na wengine wanavyojisikia
 
Aisee huo ni unyonjaji, ukabaila, ubeberu, umangimeza, ugabacholi n.k.

Mkuu don't just complain! do something. Organize. Mobilize or anything. Kuwatukana hawa jamaa doesn't make any difference!
 
Back
Top Bottom